Ushauri wangu Tanesco; Wakati huu wa mgao Futeni kwa muda ma group yote ya whatsapp kwa wateja wenu! Mtanishukuru baadae

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,276
21,395
Huduma ni pamoja na kujua kuzichanga karata!

Cha msingi lengo ni huduma bora!
Dakitali mzuri ni yule anaepambana OP room halafu akitoka inje anarudi na jibu la kueleweka kwamba mgonjwa kafa au kapona!

Lakini dakitali anaetoka O.P room kila muda kuongea na ndugu kwamba mgonjwa kapiga chafya, kakonyeza, sijui what what what! HAISAIDII! Bingwa ni yule anaepambana kisayansi na kuja na majibu ya kisansi full stop!

Wakati huu wa mgao siyo muda wa kufurahisha mtu!
TOENI TAARIFA KWA MFUMO WA PRESS CONFERENCE, RADIO, TV Na special page tu kupitia TANESCO YETU!
Vituo vidogo vitarusha taarifa call center kwa taarifa ili sisi wananchi tupate huko!

ACHANENI NA BLAAH BLAAH UPDATES KWENYE MAKUNDI YA WHATSAPP! MTACHAFUKA BURE! Kwanza mnajipa kazi bure kutuelewesha wengine wala hatuhitaji hayo ma mbambamba Mengi ya MEGAWATTS!

TUNACHOTAKA UMEME UPO AU HAUPO!
CHONDECHONDE TANESCO FUTENI MAGROUP YA WHATSAPP YANACHOCHEA HASIRA KWA WANANCHI.
Huduma ikirejea VYEMA NDIPO MTAUNGA UPYA!
Sasa hivi pambaneni kimyakimya!
 
Kuna magroup ya WhatsApp ya TANESCO ?

Au unamaanisha kurasa za Facebook, Twitter na Instagram?
Yapo kwa ajili ya huduma kwa wateja, lakini kwa maoni yangu bora YAFUTWE HADI MGAO UKIISHA! Yatawachafua pasipo sababu wakati wamepiga hatua nzuri kiasi chake upande wa huduma kwa mteja!
 
Tanesco ipi unayoongelea? Hii ya Maharage na Makamba au nyingine?
Basi kwa taarifa yako wenzio watakata umeme kesho Mara tu mechi ya kwanza ya world cup itakapoanza.
Ni wakati muafaka wa kufunga solar.
Yaani hivi hivi uone mechi za world cup? Kirahisi rahisi tu?
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, MAHARAGE Amejitahidi kiasi chake! Mambo mengine Yapo inje ya uwezo wake! Hajafanya vizuri kwa 100% lakini ukilinganisha na watangalizi wake angalau kathubutu kiasi chake!
Kiasi anajitahidi huyu kijana
 
Ni bora wakae kimya tuu.wakitoa taarifa itakuwa ni ramli tuu
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, MAHARAGE Amejitahidi kiasi chake! Mambo mengine Yapo inje ya uwezo wake! Hajafanya vizuri kwa 100% lakini ukilinganisha na watangalizi wake angalau kathubutu kiasi chake!
Kiasi anajitahidi huyu kijana
Eneo gani kajitahidi?! Yaani mtu ndio anatumika kuboronga halafu wewe upo busy kumtetea kuwa ndie anajenga?!
 
Yapo kwa ajili ya huduma kwa wateja, lakini kwa maoni yangu bora YAFUTWE HADI MGAO UKIISHA! Yatawachafua pasipo sababu wakati wamepiga hatua nzuri kiasi chake upande wa huduma kwa mteja!
Tatizo mkurugenzi na waziri ni watu wa mbambba sana.
Hamna kitu pale
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, MAHARAGE Amejitahidi kiasi chake! Mambo mengine Yapo inje ya uwezo wake! Hajafanya vizuri kwa 100% lakini ukilinganisha na watangalizi wake angalau kathubutu kiasi chake!
Kiasi anajitahidi huyu kijana

Huyo maharage ameifanyia kipi cha maana tanesco zaidi ya mismanagement na wizi?Ameikuta hakuna mgao wa umeme Tanzania, ameingia yeye mgao umeanza, sasa ni kipi unachomsifia nacho huyo incompetent maharage?
 
Huyo maharage amefanyia nini tanesco? Ameikuta hakuna mgao wa umeme Tanzania, ameingia yeye mgao umeanza, sasa ni kipi unachomsifia nacho huyo incompetent maharage?
Mkurugenzi ni mtumishi kama watumishi wengine! Anasimamia,anaomba! Anashauri!

Mambo ya mitambo na ununuzi ni ya kiserikali !
Mkurugenzi ni msimamizi wa namna ya kutoa huduma!
Kama huduma HAIPO Mkurugenzi anabakia mtazamaji kama Mimi na wewe!
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, MAHARAGE Amejitahidi kiasi chake! Mambo mengine Yapo inje ya uwezo wake! Hajafanya vizuri kwa 100% lakini ukilinganisha na watangalizi wake angalau kathubutu kiasi chake!
Kiasi anajitahidi huyu kijana
Kipimo chake Ni Mimi kuona mechi zote za wedikap.
 
Mkurugenzi ni mtumishi kama watumishi wengine! Anasimamia,anaomba! Anashauri!

Mambo ya mitambo na ununuzi ni ya kiserikali !
Mkurugenzi ni msimamizi wa namna ya kutoa huduma!
Kama huduma HAIPO Mkurugenzi anabakia mtazamaji kama Mimi na wewe!

Lakini bado haujasema alichokifanya cha maana hadi ukamsifia hivyo!
 
Huyo maharage ameifanyia kipi cha maana tanesco zaidi ya mismanagement na wizi?Ameikuta hakuna mgao wa umeme Tanzania, ameingia yeye mgao umeanza, sasa ni kipi unachomsifia nacho huyo incompetent maharage?
Mkurugenzi anapoingia ofisini haingii na mvua!
Anakuja na vyeti kusimamia kilichopo, ambacho akiona atashauri! SERIKALI NDIYO ITAAMUA!

Mkurugenzi tumulaumu kwa makosa ya kihuduma, mengine Yapo inje ya uwezo wake!
NI YA KISERIKALI
Mkurugenzi hawezi nunua mitambo ya UPEPO Kama Mitambo ya maji imefeli au kukaukiwa maji!

Yeye atashauri tu kama mtaalam
 
Kuna magroup ya WhatsApp ya TANESCO ?

Au unamaanisha kurasa za Facebook, Twitter na Instagram?
Yapo; na kwa sasa watu wanaotoa maoni ambayo administrator anaona hayafai anayafuta!
Wanategemea watu wawapongeze kwa kwa kukatiwa katiwa umeme bila mpangilio?!

Wayafute tu ma-group kama alivyoshauri mtoa mada!
 
Back
Top Bottom