Ushauri wangu kwa Waziri wa Fedha kuhusu Hotel Levy ya Halmashauri

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Kwanza pole sana. Mungu ni mwema natumaini unaendelea vizuri. Natumaini kuwa Wizara ipo mbioni kukamilisha bajeti ya 2021/22. Mimi nina ushauri kuhusu mapato ya HOTEL LEVY YA HALMASHAURI.

Kwanza ni wajibu wa kila mfanyabiashara kulipia mapato ya Serikali ili kuwepo maendeleo kwa wananchi wote. Hotel levy ya Halmashauri huwa inakadiriwa. Lakini wanapokadiria inawezekana wanamuumiza yule mfanyabiashara anayekadiriwa au mfanyabiashara anaweza kutoa taarifa ya uongo ili makadirio yake yaweze kushuka.

Mara nyingi makadirio wanayopewa wafanyabiashara inawaumiza sana hasa kipindi hiki ambacho wateja hawapo kabisa. Ili kuwe na win win situation napendekeza yafuatayo:-

(1) Kodi hii iwe flat rate kwa maana Serikali iangalie au iweke formula ya wafanyabiashara kulipa kiwango ambacho ni sawa (flat rate) bila kukadiriwa ambayo mara nyingi wafanyabiashara wanakadiriwa kiwango cha juu.

(11) Aidha kodi hii ifutwe ili kuweka kodi mbadala ili kodi hii ilipwe kwa staili nyingine.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom