Ushauri wangu Kwa watumiaji wa hii lugha naomba waibadilishe

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
2,737
2,000
Habari za kazi wakuu na poleni Kwa majukumu ya kila siku ndugu zanguni.

Husika na kichwa cha habari hapo juu najua kila mmoja wetu anataka kujua Ni kauli Gani???

Kauli hii "Tumemuhifadhi mahala salama"

"Utakaa mahali salama ili ulisaidie jeshi kutoa ushahidi"

Nakumbuka kipindi nipo mdogo nilikua nadhani kuwa mahali salama Ni sehemu Moja amazing sana kumbe ilikua Ni tofauti na jinsi nilivyokua nikifikiri.

Unaweza ukaingizwa mahali salama Kwa vitasa moto pamoja na mikong'oto ya ugoko.

Hiyo nilijionea mwenyewe Kwa kupashwa mabapa ya mgongo mpaka nikahisi ganzi mwili mzima aiseee.

Ushauri wangu Kwa watumiaji wa hii lugha naomba waibadilishe , maana kuna vijana wengine wanafanya makusudi mitaani wakidhani kuwa watakwenda kuhifadhiwa mahali salama kumbe vice versa is true.


Nawasilisha hoja wakuu.
 

bright platnumz

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
2,743
2,000
Ata apa ulipo andika ni mahala salama
tapatalk_1541774253379.jpeg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom