Ushauri wangu kwa Wanasiasa wa kweli walio ACT Wazalendo na CHADEMA

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
6,443
2,000
Huu ushauri wangu hauhusishi wanasiasa njaa/ Wanasiasa Maslahi, bali wanasiasa kweli wenye uchungu na nchi yao. Waliopo kwenye siasa kwa dhumuni la kuleta itikadi mbadala inayoenda kuleta mabadiliko ya kweli nchini katika maendeleo ya wananchi yanayoongozwa na demokrasia ya kweli na sio wanasiasa maslahi, wanaochukulia siasa kama ajira au sehemu ya kujijenga kimaisha na kikipato.

NAJUA CCM wamejipanga kuondoa credibility ya vyama vyenu kwa wananchi. Na hili ni kwenye mitego hii waliyowawekea ya nafasi za uwakilishi/ ubunge na kwenye serikali.

Tayari kuna wanasiasa Chadema wameingia kwenye mtego huu na wameenda kuapa leo Bungeni. Najua kuna wanasiasa wa ACT WAZALENDO nao watafanya hivyo Tanzania bara na kule visiwani. Hili litahusisha wanasiasa wakubwa na wadogo mpaka wale ambao hawakutegemewa.

Najua hili litaleta mpasuko mkubwa sana, najua hili litashusha morali ya wananchi kwa kiwango kikubwa katika kupata Tanzania njema yenye maendeleo na demokrasia ya kweli. Ila naomba msikate tamaa

Kwenye hali hii ndo mtajua nani yupo kwenye vyama kwa maslahi yake na familia yake na nani yupo kwa maslahi ya Watanzania walio wengi na Taifa hili. Mtajua nani anamini itikadi zenu na nani a naamini siasa ni fursa ya kujijenga kimaisha.

Hatua hii mnayopitia ni muhimu sana kwa sababu ndo mnaenda kupata ile cream ambayo ipo kweli katika kuangalia itikadi na wala sio maslahi. Katika hili kumbukeni pia ni lazima mpitie hili ili mjue kuwa njia ya kwenda Kupata mabadiliko ya kweli wala sio rahisi. Ni lazima mjue kweli rangi halisi za kila mmoja wenu ili kweli Taifa hili likapate ukombozi wa kweli wa kifikra na kimaendeleo. Kumbukeni ukombozi wa kweli upo kwa watu wenye nia na akili ya dhati ya kuleta ukombozi huo.

Naomba msikatishwe tamaa. Kama vyama vyenu vimekuwa corrupted jiondoeni kwenye hivyo vyama. Kama mkiweza waondoeni hao wote walio kimaslahi na mjenge kweli taasisi zenu imara ambazo zimekaa katika kuamini itikadi zenu kwa maendeleo ya kitaifa ya wananchi wote na wala sio taasisi zilizojaa watu wanaoangalia niendeshe gari gani au niwe na maisha gani binafsi .

Kama mkichagua kuwaondoa hao watu corrupt kwenye vyama vyenu sasa anzeni rasmi kuvijenga vyama vyenu katika kuamini itikadi zaidi. Andikeni proposals ziende EU na hata USA, wawape funds na mzitumie kweli kuvijenga vyama vyenu na kujenga taasisi imara zilizo na watu imara na waaminifu ambao wako ndani ya hizo taasisi kwa sababu ya itikadi na wala si vinginevyo. Nilisikiliza majadiliano ya Kamati ya Bunge la Umoja wa Ulaya. Walijadili hili suala la kutoa hela moja kwa moja kwa watu wanao advocate democracy na human rights. Sasa jiandaenii katika kuitumia hii nafasi.

Mkipata hizi hela ambazo ni nyingi kuliko hata hizo ruzuku, jengeni ofisi za maana katika kila kanda zenu, zitumieni hizo hela kujiimarisha kivifaa na kiteknolojia Kama kuanzisha television, radio au hata magazeti ambayo yataelimisha umma juu ya itikadi zenu kwa ajili ya maendeleo ya watu. Vilevile mzitumie hizo hela katika kuwajenga wanachama wenu kwenye mafunzo hasa sehemu mbalimbali duniani wakasome na kupata exposure ili waweze kuzielewa na kuziishi itikadi zenu

Kama mkichagua kujiondoa, naomba sasa mtengeneze taasisi imara zaidi ambayo iko nje ya ivyo vyama. Na muitumie iyo taasisi kufanya hayo niliyosema hapo juu.

Kuleta Mabadiliko ya kweli katika nchi yeyote si jambo jepesi. Kuleta mabadiliko ya kweli katika nchi zilizokulia mfumo wa kisocialist wala si jambo jepesi zaidi. Naomba mjijenge upya kwenye hayo na wala msiangalie waliowasaliti wala matumbo yenu, bali angalieni mustakabali mpana wa Taifa letu katika kuijenga Tanzania Nzuri yenye demokrasia ya kweli na maendeleo ya kweli yanayomnufaisha kila mwananchi na wala sio kikundi cha watu wachache.

Tanzania ya kweli itapatikana tu, Tanzania yenye watu genuine, wasioangalia matumbo yao bali wanaoiangalia Tanzania yote na wananchi wao na ustawi wao wa kweli.

Mungu awabariki!
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,566
2,000
Inashangaza sana Serikali kulalamika taifa "LINA WATU WASALITI NA SIO WAZALENDO", wakati yenyewe ndio ina "ASISI NA KUFUNDISHA NA KUZALISHA" watu kuwa "WASALITI & KUKOSA UZALENDO".

Wengine wanafundishwa kusaliti kwa "KUNUNULIWA/RUSHWA/AHADI ZA UTEUZI/TAMAA" na wengine kwa "VITISHO".

Serikali inaharibu uzalendo kwa vizazi vijavyo, inakomaza na kuzalisha "VIONGOZI WAASI" wa kesho kwa taifa letu.

YANAYOFANYIKA sio yakuchekea na kukenua meno. Ni hatari.
 

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,238
2,000
Mimi nakushauri anzisha chama chako uwe mwenyekiti utafute watu wenye itikadi kama zako....muitafute Tanzania ya kweli.

Hao unaowashauri unakuta waanzilishi wa vyama wenyewe walivianzisha kwa maslahi yao binafsi.

Yaani kweli kwenye hii era unaamini kuna binadamu watalala njaa halafu wakutetee wewe? Seriously?

Mwenye njaa kamwe hana msimamo.
 

binti kiziwi

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
4,135
2,000
Ndugu, lazima tuelewe kuwa kufanya siasa za upinzani nchi hii ni ngumu sana sababu ya mifumo ya kiutawala na kisiasa iliyopo. Nimesema hivi baada ya kusoma hiyo suggestion kuwa waandike proposal ya kupata funds EU au US kwa zamani labda yes, ila kwa sasa hizo pesa zitapita wapi ndugu?

Hata hivyo tuendelee kuwa kuwapongeza wapinzani aina ya Lissu, if you know what i mean.
 

relis

JF-Expert Member
May 24, 2015
2,637
2,000
Nawe njaa inakusukuma kuandika ukigewa mrija wa viti maalum hapa ukaungane na kina mdee utarudi kuufuta Uzi na kutokomea ukiunga mkono juhudi njaa haina baunsa.
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
6,443
2,000
Wewe baada ya muda utabadilisha hii ID na kuja na ID nyingine!

Tatizo mnazivamia siasa za Tanzania!

mnaleta Schoolboy politics!
Hizo siasa za Tanzania mnazojisifu kuwa mmezimaster na mnazijua napenda kukwambia hata nyie mnachokitengeneza hamkijui.

Najua unajua kuwa haya mnayafanya political class kwa maslahi yenu. Ila jueni umma wa Watanzania unayaona na unazidi kuyajua sana. Matokeo ya haya ndo zinaenda kuzaliwa siasa genuine zisizo na unafiki wala kujali matumbo
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
6,443
2,000
Nawe njaa inakusukuma kuandika ukigewa mrija wa viti maalum hapa ukaungane na kina mdee utarudi kuufuta Uzi na kutokomea ukiunga mkono juhudi njaa haina baunsa.
Nadhani hunijui vizuri. My conscious won’t allow me kuwa mnafiki. Never
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom