Ushauri wangu kwa walioowa au kuolewa na wasiokuwa na wake au waume

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
UHUSIANO MZURI.jpg


1. Kama upo SINGLE na umekazana kusema "SIAMINI MTU KATIKA MAPENZI" kumbuka rafiki zako wanaoa na kuolewa kila siku. Acha mawazo hasi omba Mungu akujalie mwenza wa maisha ambae unaendana nae.

2. Kama upo ndani ya ndoa na umekazana kusema "NAICHUKIA HII NDOA" huoni wanandoa wengine ambao wanasheherekea jubilei ya miaka 20 ya ndoa zao? Omba Mungu aiponye ndoa yako.

3. Kama umekazana kusema "NAMWACHA MUME WANGU, KWANI ANANISALITI" tafadhali hebu nenda mjini pita maeneo ya Kona Bar, Kimboka na maeneo kama hayo uone wanawake malaya wenye uchu ambao wanamsubiri kwa hamu mumeo wamchune vizuri ambao kwao hawajali haya ku share mwanaume. Omba Mungu aitengeneze ndoa yako.

4. Usikazane kusema "NAICHUKIA KAZI YANGU" angalia maelfu ya vijana ambao hawana ajira wanazunguka kila siku na mabahasha maofisini! Vipi unataka kujiunga nao? Kuwa na shukrani!

5. Umekazana kusema unapachukia unapoishi, tafadhali sana nenda kawatembelee watoto wa mitaani uone mazingira magumu wanayoishi! Mshukuru Mungu walau unalala hata kwenye godoro.

6. Wengine husema "NIMECHOKA NA HAYA MAISHA" sawa nenda mahospitalini na uone watu wanavyopigania maisha yao, nenda mochwari na utizame na uniambie unafikiri nini! Cha Mihimu ni kushukuru Mungu

Hebu nisikilize kwa makini......

Kutambua thamani ya miaka minne au mitatu, muulize mhitimu wa chuo kikuu

Kutambua thamani ya mwaka mmoja, muulize mwanafunzi aliyefeli mtihani wake wa mwisho, kutambua umuhimu wa miezi tisa muulize mama aliejifungua mtoto aliye njiti!

Kutambua thamani ya wiki moja muulize mhariri wa gazeti linalotoka kila wiki.

Kutambua thamani ya dakika moja muulize abiria aliyechelewa safari ya ndege, basi au treni.

Na kutambua thamani ya sekunde muulize mtu yeyote aliyenusurika katika ajali!

Furahia kila dakika ambayo Mwenyezi Mungu amekupa kuendelea kuishi kuvuta pumzi yake! acha kulalamika maisha ni Jinsi wewe unavyoishi.

Kama upo hai mpaka leo shukuru kwa kusema "ASANTE MUNGU.

Mshauri wa mema Herbalist.Dr.MziziMkavu
 
Mzizi mkavu,
Kila mtanzania anahaki ya kuishi at akavyo,
Wengi wetu hatujaoa na tulikuwa na wapenzi lakini tumeamua kuvunja mahusiano na kuamua kubaki single.

Kwa nini?

Kwa sababu hawa mabinti wa siku hizi ni pasua kichwa,
Afadhari enzi zenu angalau palikuwa na mapenzi ya ukweli ndio maana mama zetu wamedumu na baba zetu mpaka sasa,

Kwa hali ya sasa kukaa bila mpenzi ni raha sana tena bila karaha wala bugudha,
Ndio maana yesu hadi anakufa msalabani hakuwa na mke wala mpenzi licha ya baadhi ya wanawake kujipendekeza kwake hata hakuj ali,
Kuishi single ni raha sana tena ukiwa na kazi za kufanya huongeza ufanisi kazini.
 
Back
Top Bottom