Ushauri wangu kwa Waheshimiwa Wabunge, hasa wa Upinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wangu kwa Waheshimiwa Wabunge, hasa wa Upinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAMMAMIA, Jul 3, 2012.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Tumekuwa tukisikia mara kadhaa, Mh. Mbunge, hasa kutoka kambi ya upinzani, akitoa shutuma juu ya suala ambalo hata kama ni la kweli, lakini wamekuwa wakinyamazishwa kwa kutakiwa watoe uthibitisho wa kile wanachodai.

  Sasa ikiwa mbunge amepeleka bungeni shutuma hizo kwa suala la kweli lakini hakujitayarisha na ushahidi kamili, hii ni kuwapa kichwa CCM na kuwafanya wapinzani waonekane hawako makini. Pia ni kuwapa nafasi washukiwa kutoka mbio hapo na kwenda "kufukia mashimo yao".

  Ili kuepusha hayo, ninawashauri waheshimiwa wetu watayarishe makombora yao kisawa sawa, ili linapokuja suala la "lete ushahidi", ushahidi huo uwepo na wa ziada. Msigeuke kama CCM wa kukimbilia "tupeni muda". Ni bora kulifuatilia suala hata kama litachukua muda gani, lakini siku likitinga bungeni liwe ni kombora la kweli. Hii itawaongezea kuaminika zaidi kwa wananchi na kuwakosesha raha CCM na kimbilio lao la sasa la "Lete ushahidi".
   
 2. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  After all, bungeni hususani kipindi hiki cha bajeti ni wakati wa kuchambua bajeti zinazowasilishwa badala ya kuibua hoja ambazo hazipo mezani. Sasa bajeti ya utumishi na ufisadi wa mchemba vina uhusiano gani? Manchali jana ndo kachangia bajeti maana ananukuu na ukurasa wa kitabu cha bajeti husika. Hawa wengine naona hamna lolote kazi kusemana tu, mara oh fulani yuko hivi mara kafanya hivi. Watu wazima na akili zenu manadiscuss watu bungeni badala ya issues!. Especially mnyika, usemi wa ngoma ikilia sana hupasuka waweza kutimia. Take care
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Unataka Muchemba na Manyanya wakitoa allegations zisizo za ukweli zinazoingia kwenye Hansard wasikanushe ,kweli wewe unaubongo wa bung'o
   
 4. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ushauri huu ni kwa Waheshimiwa Wabunge wote lakini hasa kwa wapinzani kwa sababu wao ndio wanaosakamwa zaidi. Kwa Mhe. Mbunge wa CCM akisema lolote hakuna tatizo. Unakumbuka jana yule Bi. Engineer (Esther Manyanya) aliyesema CDM inahusika na upigwaji wa Ulimboka, alitakiwa kutoa ushahidi?
   
 5. Third Eye

  Third Eye JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 331
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  kuna hili kuvunja sheria ukiwa na nyaraka za siri za serikali, sasa mtu anawezaje kutoa ushahidi wakati nyaraka zinahatarisha "usalama wa taifa"
   
 6. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  sasa wapinzani lazima walijue hilo, kwamba refa yupo upande wa timu mwenyeji. Wapinzani lazima walijue hilo, waepuke kufanya faulo zisizo za lazima au kucheza offside trick wakidhani refa atapuliza filimbi, haipo
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Why wakati nchi hii ni yetu wote yaani waanze kusuccumb na kuruhusu sheria na kanuni za bunge kupindishwa duh hii ni kali
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hilo ndilo nililokusudia Mkuu wangu Polisi.

  Bungeni popote ulimwenguni ni pahali pa misuguano baina ya chama tawala na upinzani, hivyo, kanuni moja ya mapambano ni kujua udhaifu wa mpinzani wako. Kwa kuwa upinzani wanaelewa udhaifu wa mchezo mchafu wa chama tawala, watumie udhaifu wao huo kupambana nao na sio tu kurushiana makombora yasiyo na mashiko. CCM wamekamata mpini lakini kama upinzani watavaa gloves, hakiwezi kuwakata.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Gloves gani hizo zimekuwa za chuma ,hapana zinaweza kukatwa kwa kuwambia ukweli kwa sababu CCM na wabunge wao wanataka kutumia bunge kudown grade immage ya wapinzani kuwaonyesha kwamba hawana uwezo lazima wapinzani wahakikishe wanaweka mambo sawa
   
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Hata akileta ushahidi wala huto usikia.
  umesha jiuliza kuhusu ishu ya lema na uongo wa pinda iliishia wapi?

  Utasikia huo ushahidi upitiwe na offisi ya spika ndio uletwe bungeni.
   
 11. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  FLORIDA Mkuu, huo ukweli ndio gloves zenyewe, lakini ukweli uwe na evidences sio ukweli unaoamini wewe tu kuwa ni ukweli.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Toka wakati Mh. Lema yuko bungeni, alilirejelea tena lilena kulikumbushia mara kwa mara? Baada ya kuondoka, walioko nyuma yake wamelisemea tena? Mapambano kamili yanakuwa endelevu, papo kwa papo kamba hukata jiwe.
   
 13. F

  Froida JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Nadhani sisi wananchi tunauwezo wa kupembua mimi siwezi tuu kuamini nina uwezo wa kutafakari na kuamini pia ninachosema ni kuwa wabunge wa CCM wanapaswa kuisaidia serikali yao ili kuboresha mapungufu badala ya kuwatukana wapinzani ambao hawana serikali wala hawakusanyi kodi kung'aninia kukosoa spelling na kutoa tafsiri potofu kwakutaka credit za kisiasa kunawaangusha zaidi wabunge wa CCM kuliko wa Chadema
   
 14. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ni sahihi wabunge wajadili hoja iliyopo mezani kwa busara, heshima na unyenyekevu. Wabunge wote bila kujali vyama vyao wanawakilisha wananchi. si busara kudhalilisha wabunge kwa lugha chafu; ni aibu kwa spika au mwenyekiti kumwambia mbunge anawashwa anapoomba mwongozo au anapotoa taarifa.

  Nafahamu Mnyika alichangia bajeti kuhusu utawala bora.
   
 15. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mamamia, umesema ukweli na ushauri wako ni wa kufaa.
  Wabunge wa CCM ni kama klabu za Arabuni kwenye home ground.
   
 16. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wanakurupuka wakisikia issue juu juu wanakimbilia bungeni wanaona kama kuna mwenzake ataisikia halafu atamuwahi kuipeleka bungeni. Nilitegemea wawe wanakaa kama chama kujadili kujipanga kwanza maana unakuta Zitto anatoa hoja Mbowe anashangaa.
   
 17. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  "Nyaraka za Siri", "Kuhatarisha Usalama wa Taifa"... hivi ni vitisho na vikwazo vinavyotumiwa na serikali kuwa "isiguswe panapouma", lakini kwa mbunge makini anajua ni kipi cha siri na kipi sio siri - There is always way out in Laws.

  Ninakubaliana na wewe Mkuu, tafauti yetu ni kuwa mimi ninaangalia pande zote. Nadhani umekuwa ukiona pia "kauli gongana" miongoni mwa viongozi wetu. Mmoja anasema hili mwengine anasema jengine kwa suala hilo hilo moja; mmoja anatoa kauli, mwengine anasema kauli hiyo ilikuwa yake binafsi sio ya chama n.k. We're all rotten!
   
 18. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Na mwenyekiti dhaifu hakuliona hilo
   
 19. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Bora kuwa kipofu wa macho kuliko kipofu wa moyo. Udhaifu ni upofu wa moyo.
   
 20. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  yule mkuu wa mkoa alivyosema cdm inahusika na mgomo wa madaktari hivi alipewa siku 7 alete ushahidi au?
   
Loading...