Ushauri wangu kwa viongozi wa Tanzania.

St Lunatics

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,644
11,166
Ushauri wangu kwa Magufuli na viongozi wote wa Tanzania pamoja na jeshi la polisi. Kwasasa tunaweza kusema tupo kwenye mwendo kasi wa kuleta maendeleo nchini na kuwazuwia wapinzani na harakati za kufanya siasa. Mnaweza kuona mmefanikiwa kila kona ndani ya nchi lakini msisahau walio nje ya nchi.

Hapa nazungumzia majirani wetu na Majangili wa mali za nchi yetu wapo macho kuangalia wapi watapenyeza mkono wao na kufanikiwa lengo lao. Leo Tanzania ina majeshi Congo na Burundi wale wanaominywa na majeshi wetu huko wanaweza kuja kupenyeza ushauri kwa mlango wa kwetu na kuwafunza vijana waliokata tamaa ya maisha.

Na wakiona hawana samani kwenye nchi yao hii, Hao watakao watumia vijana wetu wanajua ikitokea vurugu Tanzania basi wao watapata nguvu kuondoka kwa jeshi la Tanzania nchini mwao. Na kutuacha wenyewe na vurugu letu hapo hapatakuwa na kiongozi wa serikali wala wa upinzani mwenye kusikilizwa. Watakuwepo viongozi wenye kuasi na kuangalia masilahi yao tu na kikundi chao. Na hapo makundi kama ya wafugaji na wakulima,Makabila na Makundi ya dini wataanza kupambana pia.

Ushauri wangu naomba viongozi wasiwe wagumu kuwasikiliza Wapinzani,Wananchi na kukaa pamoja kuwasikiliza nini wafanye ili kuleta maendeleo nchini mwetu. Kuna familia zilishikamana na kuwa matajiri sana lakini dharau ilipozidi na wazee wao kufariki mali zao zote ziligawanyika na kuishia kununiana mpaka kwenye mazishi na harusi,kufanyiana ushirikina au kuuwana kabisa.
 
Back
Top Bottom