Atkins Mendel
JF-Expert Member
- Feb 12, 2017
- 616
- 752
Mkuu yote kheri, swali la kujiuliza pia katika nchi nyingine za Afrika ambazo upinzani Umefanikiwa kupenya na kushika madaraka je wamefanikiwa kubadilisha hali za maisha ya watu na nchi kwa ujumla? Mm ukiniuliza nitakwambia Hapana, katika nchi ambazo upinzani Umefanikiwa kupenya au kubadilisha utawala hakuna mabadiliko sana zaidi ya vilio kutoka kwa wananchi, mfano UGANDA kabla ya Museven alikuwa Iddi Amin, Huko Rwanda kabla ya Kagame kulikuwa na utawala tofauti, huko Burundi kabla ya Nkurusinza na chama chake kulikuwa na utawala wa chama kingine, the same applies to Ghana, Ivory Coast, Madagascar, Angola, lkn mm nikifuatilia hizi nchi sioni mabadiliko ya maana ambayo hizo tawala mpya zimefanikiwa kuwaletea wananchi na nchi kwa ujumla, badala yake wote wamefata nyayo za watangulizi wao katika kuendeleza dhuluma dhidi ya wananchi na nchi kwa ujumla. Tatizo naloliona sio kubadilisha vyama, tatizo ni nani anaingia madarakani ili kuukabili mfumo ambao Ndio chanzo cha umasikini katika nchi zetu, believe me or not hata aingie nani mkuu, bila huyo mtu kudeal na mifumo inayodidimiza nchi kiuchumi yote itakuwa ni kujilisha upepo.