Ushauri wangu kwa vijana mliofanikiwa kupata ajira hasa za hivi karibuni

Heaven Seeker

JF-Expert Member
May 12, 2017
478
1,047
Awali ya yote niwapongeze sana. Kama mjuavyo, hizo fursa kuna wengi walizitamani lakini hawakufanikiwa. Kwahiyo hongereni sana. Nimeamua kufungua uzi huu ili ku-share nanyi vitu angalau kwa uchache ambavyo vinaweza kuwasaidia. Hii ndio faida ya JF.

1) Kwanza kabisa, natambua vijana mlio wengi mna madeni mengi mpaka sasa. Ukweli ni kuwa mtatumia mshahara wenu na posho za kujikimu (iwapo mwajiri wenu atawalipa kwa wakati) kulipa madeni ya nyuma. Zingatieni kulipa hayo madeni maana dawa ya deni ni kulipa. Acheni kabisa ujanja janja wa kuendelea kuwazungusha waliowaamini na kuwakopesha siku za nyuma. Ukichanganya na suala la kuanza kununua mahitaji ya ndani ya kuanzia maisha, pamoja na kulipa madeni, kwa wastani, inaweza kuwachukuwa kama miezi 6 hivi ili kukamilisha hayo madeni na mahitaji muhimu. Hili ni jambo mnalopaswa kulijua mapema kabisa hasa kwa vijana wenzangu ambao mnatoka kwenye familia za wakulima. Kwa vijana wachache ambao mnatoka kwenye familia bora huu ushauri unaweza kuwa siyo wenu maana wazazi wenu wanaweza kuwa-support.

2) Kwa vijana mlio wengi mnaotokea kwenye familia za wakulima, tambueni kuwa sasa mtakuwa kwenye dira za watu hasahasa ndugu, jamaa na marafiki. Hao jamaa wanachojua ni kuwa, baada ya wewe kupata ajira, tayari umetusua. Wakati ukweli hauko hivyo. Kwahiyo mtapokea maombi mengi sana ya kutoa misaada ya hapa na pale. Hii itakuwa sehemu kubwa ya changamoto kwenu, ila nawasihi mtumie hekima sana katika kukabiliana na hii changamoto. Fanya kile kilicho ndani ya uwezo wako kadri unavyojisikia amani. Kile usichoweza usijilazimishe na usiogope kabisa kusemwa na hao ndugu maana huu ndio wakati wake wa kupewa majina yote kama vile ' umekuwa wakujisikia sana' ' ama hupendi kulipa fadhila' au umesahau ulikotoka' na kwamba 'umebadilika sana'. Unaweza kutenga kiasi kidogo cha pesa kwa ajili ya kutatua changamoto hii, na ikifikia ukomo basi inabidi uachie hapo hapo. NARUDIA TENA, UTASEMWA SANA NA KUANDAMWA, ILA USIOGOPE.

3) Katu kabisa usikimbilie kukopa. Hasahasa kwenye vitaasisi flani vya mikopo mtavikuta huko. Mtajutia endapo mtakimbilia kukopa na mtaiona kazi mbaya na utaishiwa hamu ya kuendelea na kazi kabisa. Kwa ajira za Serikalini ili ukopeshwe na bank inatakiwa mpaka upate barua ya kuthibitishwa. Hii barua unaweza kuipata baada ya mwaka mmoja au hata miwili kwa kutegemea na mwajiri wako. Sasa kwakuwa shida nazo ni nyingi, kuna vitaasisi vingi vitakufata ambavyo siyo bank, vitakushawishi ukope. USITHUBUTU KABISA. Wewe vumilia tu kwanza angalau hata miaka hata mitano hivi ili uone uelekeo wa maisha kwanza. Unweza dhani unaharaka sana na maisha, ila nakwambia pamoja na haraka zako unaweza usifike popote pale kwa miaka hata 10 ijayo. Kwahiyo kuwa mtulivu kabisa. Nakwambia hili kwakuwa ukweli ni kwamba, karibia asimilia 95 ya waajiriwa wengi wanaokopa ili eti wafanye baishara, hizo biashara huwa zinakufa na wanaambulia kulipia madeni kwa miaka mingi ambapo pesa ziliyeyukia kusikojuliakana. Kwahiyo kuwa mtulivu kabisa na uvumilie haswa.

4) Ukweli ni kuwa, kwa mlio wengi, mishahara yenu haitotosha kugharamia mahitaji hata yale ya msingi tu. Hasa ukishakopa ndio majanga kabisa. Kwahiyo kuweni wavumilivu na kwa wale mtakaofanikiwa kubakiza vijisenti baada ya kulipia mahitaji ya kila mwezi basi hakikisha mnafanya savings. Kwa wale ambao sehemu zenu za kazi zina viposho vya hapa na pale, basi jitahidi sana kutumia hivyo viposho kufanya savings maana zitakusaidia hapo baadae.

5) Kwa wale mtakaokuwa mmepangwa sehemu zenya changamoto nyingi wala msiogope. Mnaweza jikuta kuna shida nyingi kama barabara, maji, mahala pa kuishi n.k ila vumilieni huku mkisoma ramani za maisha yanavyoenda. Ukiona mambo magumu sana basi huko mbeleni unaweza kuomba kuhama au kuomba kwenda kusoma. Yaani jambo la msingi hapa ni kuwa, vumilieni tu maana kuna sehemu unakuta hata network ya simu ni changamoto. Mvumilivu hula mbivu.

6) Kuhusu suala la kukimbilia kuoa au kuolewa. Hili naomba nisitoe comment yoyote kwa sasa maana ni very complex na wajuvi wanasema hakuna formula ktk hili. Ila ushauri wangu ni kuwa tuliza sana akili unapohitaji kufanya uamuzi wa hili jambo. Kuoa au kuolewa baada tu ya ya ajira ni jambo ambalo litakuwa na positive ama negative impacts kwenye maisha yako huko mbeleni. Kwahiyo kuwa makini sana.

Naomba niishie hapa kwa sasa. Nitaendelea hapo baadae kidogo kuhusu jinsi ya kukabiliana na majungu kazini, ushirikina, wivu, kugombania vyeo kazini, n.k
 
wengine tayari wamejipanga kwa kila kitu...na hizo ajira zimewakuta waliishajipanga kimaisha ..hao unawashauri nini?
Kama walishajipanga na hawana madeni basi hongera zao sana. Hapo sasa inabidi kuanza kuweka savings. Kama unadhani wewe si mzuri wa kufanya savings basi fungua hata fixed account. Achana kabisa na habari za kukopa kwa miaka ya mwanzo. Tuliza akili na ujifunze maisha ya ajira kwanza. Fikisha angalau miaka mitatu kazini, ule mwaka wa nne ndio uanze kufanya maamuzi. Ukiweza kuanzisha biashara basi anazisha kwa mtaji wa savings zako halafu biashara itakuwa inakua taratibu. Ikiimarika huko mbeleni ndio unaweza kuikopea, ila ukiweza usipende kukopa haraka haraka. Na endapo kutakuwa na SACCOS kwenye mazingira ya kazini kwako basi jiunge huko maana riba zake ni nafuu na utakopa baadae kidogo.
 
Back
Top Bottom