Ushauri wangu kwa uongozi mpya wa CCM unaotarajiwa kusimikwa rasmi tarehe 23/07/2016

raymbilinyi

Member
May 25, 2016
13
45
USHAURI KWA UONGOZI MPYA WA CCM UNAOTARAJIWA KUSIMIKWA RASMI TAREHE 23/07/2016.

Kwanza binafsi ninafuraha kuona siku zimebaki chache za kamanda wetu na Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Magufuli kukabithiwa mikoba ya kuwa Mwenyekiti mpya wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hakika itakuwa furaha kwa mwanachama yoyote ambae ni mpenda mabadiliko ya kweli ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chama kikongwe na chenye demokrasia ya kweli ya viongozi wake kupokezana uongozi. Ni nadra sana kwa vyama vingine vya siasa kuweza kufanya mambo CCM inafanya kama haya ya kupokezana kijiti cha uongozi maana vyama vingine tumeshuhudia viongozi wake wakikaa muda mrefu bila ya kukubali kuachia madaraka. Binafsi namshukuru sana Mheshimiwa Rais mstaafu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kukubali kwa hiari kumuachia nafasi ya uenyekiti wa CCM taifa kwa Mh. Rais Dr. JPM hata kabla ya muda. Hakika hii ni demokrasia ya kweli iliyojengeka ndani ya CCM.

Changamoto ndani ya chama zilikuwepo na bado zipo, japo watu kama akina Abdulrahman Kinana Katibu Mkuu wa CCM Taifa hakika amefanya kazi kubwa sana na kwa bidii na moyo mmoja kuhakikisha chama kinakubalika katika jamii na hata kushinda uchaguzi kwa kishindo mwaka 2015 licha ya upinzani kuimarika sana wakati huo.

USHAURI KWA UONGOZI MPYA UNAOTARAJIWA

Ushauri kwa uongozi mpya nikuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii kama alivyokuwa anafanya mheshimiwa Abdulrahman Kinana na team yake katika kukijenga chama kwa moyo mmoja na utashi. Ushauri mdogo kwa mwenyekiti mpya............kama ifuatavyo:-

1. Mwenyekiti aunde safu yake ambayo hatakuwa na watu wenye majukumu mazito serikalini kama uwaziri, mbunge au mtumishi maana kazi ya chama inahitaji kujitoa zaidi hasa muda wako na akili nyingi katika kukijenga chama.

2. Wale wanaotafuta uheshimiwa tu kwa dili zao hao mwenyekiti mpya asifanye kazi na watu wa aina hiyo maana kuna katabia kalijengeka cha mtu kutumia chama kujinufaisha yeye pasipo kuwa na mipango yoyote ya kukisaidia chama.

3. Pia kuachana na watu wanafiki na wakujipendekeza kwa mwenyekiti maana wataendeleza fitina na majungu matokeo yake kusababisha mpasuko ndani ya chama na wanachama wenyewe.

4. Kuwaondoa wasaliti endapo watabainika tu bila ya huruma maana walikuwepo sana na bado wapo hata sasa.

5. Kuachana na watu wapenda mafarakano, yaani unamkuta mtu ndani ya chama haelewani karibu na watu wote kitu ambacho hujenga chuki kwa wanachama na kufanya chama kishindwe kusonga mbele.

6. Kuwatumia watu wa lika zote ambao wana taaluma na elimu ya kutosha na pia wana mikakati ya kukifanya chama kipendwe na wanachama na wananchi ili kisonge mbele na kuendelea kushinda.Kupata watu wenye taaluma ya kukifanya chama kisiwe tegemezi kwa ruzuku pekee serikalini wakati kina viwanja vingi, majumba mengi, shule nyingi, miradi mingi na wanachama wengi lakini bado chama kinamatatizo ya pesa. Idara ya mambo ya nje, fedha, siasa inahitaji watu makini wenye weredi mzuri wa masuala hayo ili chama kisiwe na shida kuhusu pesa na uelewa wa siasa.

7. Tuachane na wale wanaotumia pesa au rushwa ndani ya chama kupata uongozi. Hii tabia ilishakuwa kubwa nadhani sasa kiama chao kimefika maana Mh Mwenyekiti mtarajiwa hapendi hizi tabia za rushwa rushwa.

8. Tusiwajaribishe watu waliokwisha shindwa kukiongoza chama kwa nafasi walizo kuwa nazo awali. Hapa naongelee mtu alikuwa kwenye madaraka katika idara furani na hajaonesha mafanikio yoyote ndani ya chama lakini bado anafikilia kubaki au kupata madaraka na fursa kubwa kabisa wakati ile aliyokuwa nayo imemshinda.

9. Chama kijitahidi kuibua watu wapya na sura mpya katika uongozi kuliko kubaki na sura zilezile, majina yale yale, watu wale wale wenye tabia, fikra zile zile matokeo yake chama nacho kitabaki kile kile. Tuondokane na dhana ya msemo kuwa CCM ni ile ile, lazima chama kibadilike kimtazamo na kitaswira na hii itawezekana mara tu ambapo watu wapya na majina mapya yataibuliwa kuliko kubaki na safu ileile maana watabaki kuendesha chama kwa mazoea yale yale.

10. Mwisho kwa leo lakini sio kwa umuhimu ni kuwatumia wanachama wenye mapenzi ya dhati na kweli kwa chama chao na kuachana na watu ambao hawana imani na chama chao mara mguu mmoja ndani mara mguu mmoja nje. Chama kinataka watu watakao kitetea muda wote hasa kipindi hiki ambacho uzushi juu ya serikali umekuwa mkubwa sana.

Asanteni haya ni mawazo yangu binafsi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) chama tawala kinachoongoza serikali yetu kwa sasa. Kwahiyo nivizuri CCM kikapata team sahihi ya kuweza kumsaidia Mwenyekiti wetu mpya na mtarajiwa ambae tarehe 23/07/2016 atakabidhiwa mikoba ya uenyekiti kukiongoza chama kwa miaka mitano. Nawatakia Mkutano mwema wanaCCM wote popote walipo...Historia inaenda kuandikwaaa....kama weye mwana CCM share hiiii..........Good day all

By

Richard Mbilinyi
 

magafumukama

JF-Expert Member
May 31, 2016
743
250
"Bila rushwa" uliwahi kusikia wapi? Am now 60 years old that has been our terminology. How can u change that
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom