Ushauri wangu kwa TBC kuongeza rates ya watazamaji

St Lunatics

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,647
11,148
TBC ni baba wa habari kwa Tanzania yetu lakini baba huyu anategemea msaada kwa serikali(ruzuku) badala ya kujitegemea mwenyewe kwa uboreshaji wake wa vipindi. Huu ni ushauri wangu kwa TBC juu ya vipindi vyao:-

1 Irushe Bunge live na iwe tv pekee yenye kurusha nchi nzima.

2 Ligi kuu za mpira wa Ulaya iwe tv pekee yenye kurusha live. Hapa nakusudia ikifika robo fainali mpaka fainali ya ligi

3 Kuwe na vipindi vya kuwahoji wabunge na madiwani kila kona ya Tanzania juu ya maendeleo waliyoyaleta wakati wa mihula yao.

4 Kuwe na kipindi cha kuwahoji Mawaziri/Wakuu wa mikoa kila wiki juu ya changamoto za kazi zao na nini wanahitaji ili kutatua matatizo yao.

5 Kuwe na kipindi chenye kuonesha matatizo yanayoyakabili jiji na vijijini mfano:- takataka,maji taka,maradhi,usumbufu wa usafiri,matatizo ya maji,upungufu wa mazao na mengi wanaweza kuongezea kila siku zikiendelea.

6 Mwananchi kuijua haki yake juu ya sheria akiwepo hospitalini, makazini na jinsi ya kulitatua kisheria.

7 Kuwe na kipindi cha mtu atakae ongelea matatizo(changamoto) za ndoa na jinsi ya kutatua, pia kuruhusiwa kupiga simu na kuuliza maswali.

8 Kuwepo kipindi cha polisi na wanasheria kuongelea sheria kila utata wa sheria ukitokea.

9 Pawepo kipindi cha polisi live hiki kipindi kinaonesha jinsi polisi inavopambana na wahalifu kama majambazi, majangili, wizi, rushwa na mengi wanaweza kuongezea.

10 Kuwepo kipindi cha kushindanisha cha maswali na majibu na mshindi kushinda hela taslimu au kupewa vacation ya kutembelea sehemu flani kwa kila mshindi. mfano unaweza kuwaalika wanafunzi wa UDSM na UDOM ukawashindanisha au watu wa mtaa huu na ule. hapa unaweza kutumia njia ya kuja studio au njia ya skype. lakini njia ya studio ndio nzuri zaidi.

Mkiwa na vipindi vizuri vitawavutia wananchi na kuongeza rates ya watazamaji, bila ya kusahau musiwe mnaonesha vipindi vya siasa kiushabiki bali muwe fair kwenye mambo ya siasa.
 
hawa TBC ni Bure Kabisa. Hati waonyeshe Ligi za Ulaya! wakati Hata Mechi za Timu ya Taifa Wanashindwa Kuonyesha?

Hii TBC ni Bora hata Tv1 kuliko hawa Jamaa yaani toka Aondoke Tido Mhando ni Hovyo Kabisa hii Tv.
Ndio nikawataka wabadili vipindi ili kuwavutia watazamaji, Tv kupelekeshwa kisiasa haiwezi kukizi kiu ya watazamaji.
 
Ushauri mzuri.
Pia....
Wafanye kazi kama kituo binafsi.
Siasa imechangia pakubwa kuwauwa..... waangalie na upande wa upinzani.
Waweke series za kijanja.
Waruhusu viongozi kuja na kuulizwa maswali ya papo kwa papo.
Waendeshe mijadala huru katika maswala mbali mbali ya kijamii, siasa, afya, uchumi nk..
 
Ahsante mdau kwa kuwapa wazo hawa ndugu zetu, kuna wakati unaona aibu hata kusema hiki ni chombo chetu chenye dhamana ya kusambaza habari nchini na hata nje ya nchi.
katika kuongezea hapo pia wanaweza kuwa na vipindi vifuatavyo:-
1. Kipindi kitakachoelezea historia ya Mkoa mmoja mmoja na wilaya zake, jiografia yake, mazao yanayopatikana huko, shughuli za kibiashara zinazoendeshwa huko n.k.
2. Kipindi kitakachochambua baadhi ya vitu toka kwa wenzetu ambavyo tunaweza fanya hapa kwetu. kwa walioangalia documentary ya Where to Invade Next wanaweza nielewa Zaidi.
3. Kuwa na kipindi kitakachowashirikisha wanasayansi na watafiti kutoa maoni juu ya changamoto zinazowakabili wananchi wa sehemu mbali mbali.
4. kuwa na kipindi kitakachochagiza ukuaji wa taaluma kwa watoto wa shule za msingi na sekondari kwa maana ya debates,quiz n.k

nawashauri wachangamke na wajifunze toka vyombo vya nchi nyingine kuliko kukaa huku wakipoteza dira. Nchi yetu tuipende na tuitangaze.
 
Asante mkuu kwa kuongeza vipindi vizuri zaidi
 
TBC ni baba wa habari kwa Tanzania yetu lakini baba huyu anategemea msaada kwa serikali(ruzuku) badala ya kujitegemea mwenyewe kwa uboreshaji wake wa vipindi. Huu ni ushauri wangu kwa TBC juu ya vipindi vyao:-

1 Irushe Bunge live na iwe tv pekee yenye kurusha nchi nzima.

2 Ligi kuu za mpira wa Ulaya iwe tv pekee yenye kurusha live. Hapa nakusudia ikifika robo fainali mpaka fainali ya ligi

3 Kuwe na vipindi vya kuwahoji wabunge na madiwani kila kona ya Tanzania juu ya maendeleo waliyoyaleta wakati wa mihula yao.

4 Kuwe na kipindi cha kuwahoji Mawaziri/Wakuu wa mikoa kila wiki juu ya changamoto za kazi zao na nini wanahitaji ili kutatua matatizo yao.

5 Kuwe na kipindi chenye kuonesha matatizo yanayoyakabili jiji na vijijini mfano:- takataka,maji taka,maradhi,usumbufu wa usafiri,matatizo ya maji,upungufu wa mazao na mengi wanaweza kuongezea kila siku zikiendelea.

6 Mwananchi kuijua haki yake juu ya sheria akiwepo hospitalini, makazini na jinsi ya kulitatua kisheria.

7 Kuwe na kipindi cha mtu atakae ongelea matatizo(changamoto) za ndoa na jinsi ya kutatua, pia kuruhusiwa kupiga simu na kuuliza maswali.

8 Kuwepo kipindi cha polisi na wanasheria kuongelea sheria kila utata wa sheria ukitokea.

9 Pawepo kipindi cha polisi live hiki kipindi kinaonesha jinsi polisi inavopambana na wahalifu kama majambazi, majangili, wizi, rushwa na mengi wanaweza kuongezea.

10 Kuwepo kipindi cha kushindanisha cha maswali na majibu na mshindi kushinda hela taslimu au kupewa vacation ya kutembelea sehemu flani kwa kila mshindi. mfano unaweza kuwaalika wanafunzi wa UDSM na UDOM ukawashindanisha au watu wa mtaa huu na ule. hapa unaweza kutumia njia ya kuja studio au njia ya skype. lakini njia ya studio ndio nzuri zaidi.

Mkiwa na vipindi vizuri vitawavutia wananchi na kuongeza rates ya watazamaji, bila ya kusahau musiwe mnaonesha vipindi vya siasa kiushabiki bali muwe fair kwenye mambo ya siasa.
11. Wabadili muonekano wao kuwa HD angalau na hata muonekano wa studio yao ya habari na mahojiano.
 
Kwa kweli kutokurushwa kwa bunge ndiyo kitu pekee kitakachonifanya nisiwape kura yangu.na walivyoanza nilijua ni masihara ama kweli binadamu ni noma
 
Bonge la mawazo!! Ki ukweli wakiaandaa hivyo vipindi na vikawa na uhalisia, heshima itakuwepo, tatizo sasa,,,,,, wenye ruzuku yao (muhimili uliojichimbia zaidi kuliko yote) watakubali maana hayo yote yataanika changamoto zake
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom