Ushauri wangu kwa Serikali

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,109
9,406
Natumai hamjambo wakuu,

Katika historia, bibi mzaa baba aliwahi kunisimulia kua enzi za ukoloni wazungu walipita nyumba hadi nyumba kujifunza tiba za magonjwa mbali mbali kwa wazee wetu kwa kuandika kisha wakapeleka kwao nakuziendeleza hivyo napenda kuishauri serikali pia katika hili.

Ikiwa serikali imewatumia watu wa tiba asilia kuleta dawa zao na kuzifanyia uchunguzi kisayansi kisha tukapata ufumbuzi wa corona, basi iwatumie tena walete dawa za magonjwa mengine mbali mbali kama ya moyo, kisukari, kansa na nk. zifanyiwe uchunguzi kitaalam kama zitafaa na hazitakua na madhara kitaalam basi zitumike kama tiba.

Hii itasaidia sana kuiimarisha sekta yetu ya afya itakapokua ikizalisha dawa zake na tutakua tumepiga hatua nyingne kama taifa kuliko kua tunaagiza madawa daily akati miti na wataalam tunao.
 
Mimi mwenyewe nimewatibu wengi sana

Jr
Nyie kama wataalam wa tiba asilia nawashauri mliwasilishe hili kwa wizara ya afya ili dawa zenu zithibitishwe kisayansi maabara ziwafae wengi na nadhani mtanufaika zaidi kiuchumi nakulipunguzia taifa gharama za uagizaji madawa.
 
Wazo zuri sana
Waafrica tunaendelea kua duni coz hatujajitegemea kifikra lakini corona kiasi fulani imetupa mwanga kua tunaweza jitegemea kifikra na tukapiga hatua kubwa mbele.

Fikiria kama tunazo dawa asili zakumtibu alievunjika mguu/mkono chini ya wiki akapona, Je hizi tiba tukizipeleka maabara zikathibitishwa kitaalam huoni kama tutapiga hatua kubwa
 
Nyie kama wataalam wa tiba asilia nawashauri mliwasilishe hili kwa wizara ya afya ili dawa zenu zithibitishwe kisayansi maabara ziwafae wengi na nadhani mtanufaika zaidi kiuchumi nakulipunguzia taifa gharama za uagizaji madawa.
Hili litawezekana tu iwapo tu tutaacha utegemezi na ombaomba kwa mabeberu. Unajua ile misaada na mikopo tunayopewa ni return ya sisi kukubaliana nao kwenye mambo yao ikiwemo kukubali kuchukua bidhaa zao kama madawa nk.

Jr
 
Hili litawezekana tu iwapo tu tutaacha utegemezi na ombaomba kwa mabeberu... Unajua ile misaada na mikopo tunayopewa ni return ya sisi kukubaliana nao kwenye mambo yao ikiwemo kukubali kuchukua bidhaa zao kama madawa nk

Jr
Ni kweli mkuu lakini huu ndo wakati serikali inapaswa kuchukua hatua madhubuti na funzo kubwa tumelipata kwa janga la corona, imagine kama karibu robo tatu ya mahitaji yakupambana na corona tumetengeneza wenyewe unadhani kipi kinashindikana?
 
ni kweli mkuu bt huu ndo wakati serikali inapaswa kuchukua hatua madhubuti na funzo kubwa tumelipata kwa janga la corona, imagine kama karibu robo tatu ya mahtaji yakupambana na corona tumetengeneza wenyewe unadhani kipi kinashindikana?
Bado hatujawa tayari wala bado hatuna uthubutu wa kujitegemea

Jr
 
Trust me bado sana.. Hakujafinywa.. Tukifinywa kidogo tu tutalegea mlenda umesingiziwa

Jr
mkuu tusiwe waoga sana kuthubutu, mbona hata wanijeria ni weusi wenzetu bt wamepga hatua kubwa sana kiuchumi akati na wao wanayo mikataba na mabeberu?

trust me shida kubwa kwetu ni kushindwa kuandaa sera na mazingira rafiki
 
mkuu tusiwe waoga sana kuthubutu, mbona hata wanijeria ni weusi wenzetu bt wamepga hatua kubwa sana kiuchumi akati na wao wanayo mikataba na mabeberu?

trust me shida kubwa kwetu ni kushindwa kuandaa sera na mazingira rafiki
Napenda uthubutu.. Napenda tujitawale.. Napenda tuondoke kwenye nira na minyororo ya mabeberu... Lakini trust me hatuna action head ya kufanya hayo kwa sasa

Jr
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom