Ushauri wangu kwa Serikali

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Mods naomba uzi huu msiuunganishe na ule wa ushauri kwa serikali ya Magufuli wa FaizaFoxy maana ni kawaida ya nyuzi zikiunganishwa zinakosa wachangiaji, na hivyo mawazo mengi hupotea.

Nimewahi kushauri hapa kuwa ili ku-boost uchumi wa hii nchi Serikali ingeangalia uwezekano wa kuanzisha vituo vya kibiashara Viwili vya kimataifa, kama ilivyofanya Dubai na sasa inaanza kuonekana kama Ulaya ndogo.

Kwamba kama Serikali ingeweza kujenga kituo kikubwa sana cha kibiashara(international business center) pale Kahama halafu ikaweka soko la madini pale Kahama na ikahakikisha ile bandari ya nchi kavu ya Isaka inaimarika kweli kweli ili mizigo yote ya Rwanda na DRC na Uganda na South Sudan na Burundi ingekua inapakiwa na kupakuliwa pale.
Mizigo yote ingetua pale, ingekaguliwa pale na kulipiwa pale sie kazi yetu ni kusafirisha na kukusanya kodi zetu.

Leo Bakhressa anasafirisha ngano kwa maroli mpaka kigali, Kigoma wanasafirisha unga wa muhogo mpaka Bujumbura, Kagera wanauza kahawa yao Uganda na ndizi zao, kwa nini tusijenge soko??

Hii ingesaidia sana mataifa hayo yote yasiyo na bandari kugeuza Kahama kuwa soko lao na makutano yao kibiashara, kama mfanya biashara wa Uganda au Rwanda anaweza kufuata contena mpaka Mombasa huko na akalipa gharama zote atashindwaje kufuata karibu hapo ikiwa kuna soko kubwa la kimataifa ambalo anakutana na wafanyabiashara toka Tanzania na Burundi na Congo??

Wa-Congo wakiwekewa uwanja wa ndege mzuri pale Kahama na likawapo soko zuri la madini pale, ni rahisi sana wao kuja kuuza madini yao hapo na tukanufaika kweli kweli ukichanganya na madini yetu.
Leo Nairobi ndio kituo kikubwa cha uuzaji wa madini East Africa wakati Kenya hata udongo wa pemba wanazokula kina mama wajawazito sijui hata kama wanao, lakini mpaka Tanzanite yetu na dhahabu yetu inauzwa Nairobi sie bado tunakomaa na MKUKUTA na MKURABITA na BRN sijui na manini nini huko.

Kinachotakiwa hapa ni kuhakikisha bandari ya Bagamoyo au Tanga ina link na kituo hiki na wasafirishaji tunakua sisi wao wanakua wanunuzi tunaokutania sokoni, na tunakua na monopoly ya soko.

Pili kituo kingine kijengwe Mbeya pale na pa connectiwe na bandari ya Mtwara halafu ijengwe pia bandari ya nchi kavu pale ili mizigo yote ya Zambia, Malawi, DRC na kwingine itue pale na biashara zifanyike pale.

Tunafurahia kila siku ukusanyaji wa ushuru kutoka Border ya Tunduma, kwa nini tusifikirie kujenga kituo rasmi cha kibiashara Pale Mbeya ili mataifa kama matano hivi ya SADC yauze na kununua hapo na iwe ndio sehemu yao ya kukutania, tungekuwa tunakusanya shillingi ngapi kwa mwaka??

Malawi hawana chakula kila mwaka wanalialia tu, Msumbiji wao matatizo yao ya ndani na mafuriko kila siku wanalia njaa tupu, Badala ya chakula cha serikali katika ghala za taifa kuoza kila mwaka na kumwagwa kwanini msijenge kituo cha uuzaji wa chakula pale Mbeya na mkafanya biashara za taifa kwa taifa na ikajulikana kabisa kisheria??

Kimsingi kama tutaimarisha vituo hivi vya kimataifa tuta boost sana biashara za ukanda huu na kwa kuwa geografia yetu inatu -favor sidhani kama tunaweza kupata competitor yeyote hapa Afrika.

Congo wana madini lakini hawana amani, Rwanda ndiye amegeuka dalali wa madini ya Congo, Kuna kipindi NMB Kigoma(kama sijakosea) walianzisha utamaduni mzuri wa kununua madini ya Congo pale na biashara ilikua nzuri sana kabla ya wazee wa figisu kugundua kuwa ni chimbo jipya la kupiga hela wakaingiza mikono yao pale biashara ikafa Rwanda akachangamkia fursa leo tunasifia Kigali jiji zuri halafu sie tunaenda kuwa walinda amani.

Kama TISS haina kitengo cha ujasusi wa kiuchumi basi muwe mnakusanya hata ushauri wa kiuchumi wa "commons"
 
Back
Top Bottom