Ushauri wangu kwa Serikali ya Tanzania kuhusu namna bora ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma muhimu kwa wananchi kupitia mashirika yake mbalimbali

kanyembwe

Member
Apr 17, 2017
94
222
Nimefikiri Sana kuhusu nanna bora ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma muhimu kwa wananchi kupitia mashirika mbalimbali ya Serikali. Lengo hasa na kuondoa ukiritimba unaonekana katika mashirika hayo.

Leo niongelee kuhusu huduma ya umeme, maji, na hifadhi ya jamii

1. UMEME
Tumeshuhudia juhudi za Serikali kutengeneza bwawa la kuzalisha umeme la Stigllers Geoge kwa lengo lla kuongeza kiwango Cha uzalushaji wa umeme nchini jambo litakalosaidia kupunguza Bei ya umeme hivyo kuchochea uanzishwaji wa viwanda nchini, pia Serikali imekuwa ikisimamia uzalishaji wa umeme katika mabwawa mbalimbali Kama vile Kidatu, Mtera, Nyumba ya Mungu nk

Ni Jambo jema Sana Ila mfumo uliopo wa uzalishaji umeme na usambazi wake unaruhusu ukiritimba unaoondoa ufanisi wa upatikanaji wa umeme nchini, Shirika la TANESCO ndilo pekee linalohusika kusimamia uzalishaji na usambazaji wa umeme kwa walaji, hii kwa mtazamo wangu sio sawa, ushauri wangu ni kuwa TANESCO ihusike katika uzalishaji tu na swala la usambazaji yawepo mashirika mengine ambayo yatahusika katika kutafuta wateja, kuongeza miundominu rahisi, kuwawekea umeme na kutoza bill kulingana na huduma waliyotoa.

Jambo Hilo litachochea ushindani ambao kwa nanna Moja au nyingine utaongeza ufanisi, utaongeza ajira na kupunguza ukiritimba Sana, Serikali ichukue Kodi na kuwekaa vigezo katika usajili wa mashirika hayo, ninaamini utafiti muhimu ukifanyika hapa Serikali itapunguza majukumu na fedha zinazotumika Sasa katika usambazaji wa umeme zingeelekezwa katika kuboresha elimu,afya na huduma nyingine muhimu kwa wananchi.

2. MAJI

Mfumo uliopo Sasa umegawanyika katika sehemu mbili kwa mtazamo wangu, Moja Serikali kuu inahusika katika kutafuta vyanzo vya maji na kuweka miundo mbinu ya uzalishaji wa maji katika Kila mkoa na hata usambazaji wa miundombinu hiyo katika maeneo mbalimbali.

Pili Serikali inakabidhi kazi ya kusimamia miundominu hiyo ambayo hukabidhiwa kwa mamlaka za.maji Mjini na za vijijini kwa mfabo, Mwanza Kuna Mwuwasa na Ruwasa, Iringa Kuna Iruwasa na Ruwasa Arusha Kuna Aruwasa na Ruwasa nk. Mfumo huu una kasoro kidogo kwa kuwa una ukiritimba kaatika upatikanaji wa maji kwa wananchi. Ushauri wangu ni kutokuwa na mamlaka badala yake Serikali ihusike katika uzalishaji wa maji na kuyauza maji hayo kwa mashirika ya usambazaji wa huduma za maji kwa wananchi ambayo yanaweza kuwa zaidi ya Moja

Mashirika haya yatakuwa na wajibu wa kutunza miundombinu na kuongeza mingine itakayowezesha upatikanaji wa maji kwa wananchi, Jambo Hilo litaongeza ufanisi na kuondoa ukiritimba uliopo, lakini pia litaongeza ajira kwa wahitimu wa ufundi katika njanja za maji. Lakini pia Kuna kasoro kubwa kwa jumuiya za maji vijijini ambazo Sasa zinasimamiwa na Ruwasa, hizi jumuiya hazina wataalamu wa kusimamia huduma za maji.

Jambo Hilo linazorotesha juhudi za Serikali na kuongeza migogoro katika maeneo husika, Naamini mashika hayo yatakuwa na wataalamu na mwananchi atabaki kuchagua Shirika lenye ufanisi katika utoaji wa huduma, nashauri utafiti ufanyike ili kufanya mapinduzi makubwa katika upatikanaji wa huduma hii muhimu.

3. HUDUMA ZA UHIFADHI WA JAMII
Hapa nashauri Serikali irudie mfumo uliokuwepo awali wa kufufua mashirika ya NSSF, NPF, LSSF nk mfumo wa Sasa umemfanya mfanyakazi kutokuwa na Uhuru wa kuchagua Shirika linalomfaa kutokana na huduma inayotolewa,

Naamini inawezekana Kama vile ilivyo kwa huduma za Barabara, Serikali inatengeneza miundombinu na wasafirishaji wa mizigo na abiria imebaki kwa wafanyabiashara, huduma Kama za mawasiliano nk Serikali iweke vigezo na itoze kodi kwa mashirika hayo.

Naamini inawezekana, mwisho naunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha huduma mbalimbali kwa wananchi wa Tanzania.

Ahsanteni
 
Haya mambo yanawezekana sana bila hata kuhitaji mabilioni ambayo tunadhani hatuna lakini Hawa watu sijui wanafeli wapi
Siyo kila kitu kinahitaji pesa wakati mwingine akili tu
 
Mada nzuri sana .. Hoja ya Tanesco kuvunjwa vipande vipande si ngeni tena mwanzo mawazo yalikuwa kuwe na shirika linalizalisha umeme, halafu wawepo wasambazaji umeme na tatu liwepo shirika la kujenga na kukarabati miundombinu mikubwa (yale manjia makubwa ya umeme etc). Hii hoja ikapigwa pini maana watu enzi hizo walikuwa wanapiga mpunga kupitia mgao wa umeme.

Kwenye maji hata mimi huwa nashangaa maana wangeweza kabisa kuruhusu watu wenye uwezo wavute maji na kuwauzia wasambazaji. Kuna jamaa nilikuta kachimba visima vya uhakika, kaweka matanki na anasambazia watu kwa bei below ile ya mamlaka, halafu maji yake hayana chumvi kabisa.

So wanakijiji wakawa wanahamia kwake na kukimbia maji ya mamlaka, sasa badala ya kumuunga mkono wakaanza figisu za kumbania, sema jamaa yuko njema anajua sheria na kanuni zote kazifuata.
 
Umenena vyema Sana, Mimi nilishuhudia pia uzalishaji na usambazaji umeme katika kijjij Cha Bomangombe wilayani Kilolo mkoa wa Iringa kazi iliyofanywa na kampuni ya Cefa nadhani, watu walipata umeme kwa Bei poua Sana na hata TANESCO walivyofika bado baadhi wameendelea na huduma ya Cefa, nadhani Kuna haja ya kufanya utafiti wa Kina ili kuboresha ufanisi wa huduma hizi na kuipunguzia mzigo Serikali Kuu
 
Back
Top Bottom