Ushauri wangu kwa serikali kuhusu kupanda bei ya mafuta

Tanzanite klm

JF-Expert Member
May 7, 2013
441
500
Nawasalimu nyote.

Kwanza kabisa serikali mnafanya mengi mazuri.

Kuhusu suala la kupanda kwa bei ya petroli imekuwa pigo kubwa kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri kitu ambacho kinaumiza wengi.
Tanzania tuligundua gas nyingi huko kusini mwa Tanzania.

Nashauri serikali ianzishe na kuongeza mchakato wa upatikanaji wa gesi hii asilia ipatikane kwa urahisi zaidi.

TANGAS ipewe uwezo wa kufungua sheli nyingi zaidi za CNG na pia huduma ya kufunga mfumo wa gas katika magari uongezeke au serikali itoe ruzuku kwa DIT pia watu binafsi waweze kufunga mfumo wa GAS katika magari tuachane na mifumo hii ya petroli.

Hii itasaidia kwanza kupunguza upotevu wa fedha kwa wananchi.

Serikali kujiongezea mapato kwa kuuza gas yake.

Kusaidia usafi wa mazingira.

Wanaotumia mfumo wa gas CNG katika magari wanasema kwamba gas ni nafuu zaidi na inaenda kilimeter nyingi kuliko petroli mkuu.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,736
2,000
... nishati imekuwa bidhaa adimu sana Tanzania kwa sasa; kuanzia mkaa haushikiki bei. Kabla ya kukimbilia huko kwenye ma-CNG sijui nini watujazie gas yetu kwenye mitungi kwa ajili ya matumizi ya majumbani kwanza.

Hii itawalenga watanzania wengi na matokeo ni ya muda mfupi sana. Bei ya sasa mtungi wa 30 kg. kwa TZS 50,000/= ni kiama kwa walalahoi tulio wengi na of course bei itakuwa imepanda sambamba na mafuta.

Waachane na "white elephant project" ya kusambaza mabomba ye gesi majumbani ambako walengwa ni mijini hususan Dar-es-Salaam tena Masaki na Mbezi Beach huko; watuwekee kwenye mitungi na watuuzie kwa bei rahisi; savings tutapeleka kwenye mafuta wakati CNG ikija baadaye.
 
ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
3,250
2,000
Nawasalimu nyote.

Kwanza kabisa serikali mnafanya mengi mazuri.

Kuhusu suala la kupanda kwa bei ya petroli imekuwa pigo kubwa kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri kitu ambacho kinaumiza wengi.
Tanzania tuligundua gas nyingi huko kusini mwa Tanzania.

Nashauri serikali ianzishe na kuongeza mchakato wa upatikanaji wa gesi hii asilia ipatikane kwa urahisi zaidi.

TANGAS ipewe uwezo wa kufungua sheli nyingi zaidi za CNG na pia huduma ya kufunga mfumo wa gas katika magari uongezeke au serikali itoe ruzuku kwa DIT pia watu binafsi waweze kufunga mfumo wa GAS katika magari tuachane na mifumo hii ya petroli.

Hii itasaidia kwanza kupunguza upotevu wa fedha kwa wananchi.

Serikali kujiongezea mapato kwa kuuza gas yake.

Kusaidia usafi wa mazingira.

Wanaotumia mfumo wa gas CNG katika magari wanasema kwamba gas ni nafuu zaidi na inaenda kilimeter nyingi kuliko petroli mkuu.
Umeandika nadharia umewaandikia misamiati na kibablish tupu.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,826
2,000
Bei ya mafuta ikipanda, na bidhaa(consumer goods) lazima zipande bei kwasababu ya usafirishaji.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom