Ushauri wangu kwa serikali juu ya mgogoro wa madaktari

mwikumwiku

Senior Member
Jul 15, 2011
153
35
Kwa namna mambo yanavyoenda juu ya ushughulikiaji
wa mgogoro baina ya wizara ya afya na madaktari ni
wazi anayeumia ni mwananchi Wa kawaida ambaye hana haki wala uwezo wa kwenda kwa matibabu nje ya nchi.

Kinachoonekana wazi ni kwamba viongozi wa wizara wameshindwa kushughulikia mgogoro huo na kinachoendelea ni kuendelea kuitwika lawana serikali ya Kikwete....

Mh. Kikwete, Mh. Waziri Mkuu take action... wasaidieni wananchi walala hoi wanaotibiwa kwenye hospitali zetu hizi za kilala hoi ambazo ninyi hamtibiwi! Wananchi wakimbilie wapi? Wamlilie nani!

Kwa maoni yangu, huu ndo wakati muafaka kwa Rais wetu kuonyesha makucha yake... piga chini viongozi wanaoendele kudhoofisha serikali yako! Utaendele mpaka lini kuwabeba viongozi wasiobebeka kama hawa?

Hivi hakuna wabunge wengine wanaoweza kufanya kuongoza wizara ya afya zaidi ya hawa waliopo? Hivi haku mtumishi mwingine anayeweza kuwa KM zaidi ya huyu aliyopo? Hivi hakuna daktari mwingine anayeweza kuwa
mganga mkuu zaidi ya huyu aliyopo?

Eneo la tabibu ni moja ya maeneo nyeti sana! Ni eneo linalogusa maisha ya wananchi ya kila siku! Hakuna kitu kimuumiza mwananchi mlala hoi kama kuto kuwa na uhakika na uwepo Wa tiba hata hii ya kilala hoi! Tukimbilie wapi sisi tusio na haki wala uwezo Wa kwenda India kama ninyi!

Kwa nini Mh. Rais unaendelea kuwa na wema wa mshumaa! Kwa nini serikali yako iendelee kuonekana imeshindwa kwa sababu ya viongozi wabovu ambao wapo ndani ya mamlaka yako? Piga chini mawaziri, katibu mkuu na mganga mkuu weka wengine! Hii itasaidia kupeleka signal/sms kwa viongozi wengine wababaishaji kama hawa!

Bila kuchukua maamuzi magumu, serikali yako itaendelea kudhoofika siku hadi siku!

Wananchi tunaumia sana! Fanya kitu fulani ili imani yetu kwako na serikali yako irejee!
 
Rais anaamini sana kwamba madaktari wa afya wakitawala wizara yao watashughulikia mambo kwa wepesi zaidi, kumbe wapi! Japo wapo wanaoweza, lakini nadhani wanaompatia ushauri wa nani apewe wadhifa huo wanampotosha. Kila anaowateua ni magamba tu. Aachane na falsafa hiyo na awapeleke watu wa kawaida tu wasio wa Afya ataona wanafanya vema kama mifano iliyotangulia. Megji, Anna Abdalla kwa uchache. Madaktari ni viburi tu pale wizarani. Waende kutibu waone machungu waliyoyasahau. Wengine hata kuandika dawa sasa wamesahau ila mikakati ya kukandamiza na kulipiza visasi kwa walioko chini yao ndiyo kazi ya kila siku. Ukiritimba ndio wimbo wao kila kukicha. Sikiliza alichokuwa anakisema Naibu waziri jana akitoa tamko, inaonyesha anavyowakilisha uozo wa wizara usiojali watendaji wake. Na Katibu Mkuu wake alivyo sugu na haambiliki ndio basi tena. Wana majipu vichwani hao.
 
Uko sahihi kabisa Lekanjobe! Kuna haja gani ya kuendelea
kuwa na naibu waziri hopeless kama huyu! Ameonyeasha kiburi kisicho na tija yoyote
 
kinachosemwa na madaktari hawa ni kwamba uongozi wa wizara una matatizo,rais na waziri mkuu wakikaa kimya wataonyesha wao pia nisehemu ya tatizo.
 
Uelewa wa waziri ni mdogo sana, wakati wa bunge la bajeti mara mbili aliita CCBRT, CRBT na maramoja akaiita CRDB yaani niliishiwa ngunvu kabisa hata ukisikia comment zake kuhusu afya ni uozo tu. Wa pili ni BLANDINA NYONI yaani hii ni saratani , na uozo ndo maana afya imezorota! Huyu mama hafai kabisaaaaa
 
Back
Top Bottom