MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,009
- 2,171
Rais Mstaafu Kikwete anamsifia rais Samia kwa utendaji mzuri kama alivyofanya kwa marehemu Magufuli bila kujali machungu ya wa-TZ.
Ni tabia ya kulazimisha kutuonesha uhusiano wake na marais walioko madarakani. Wakati Magufuli akiingia madarakani, kulikuwa na marais wastaafu watatu; Mwinyi, Mkapa na yeye Kikwete. Katika hao wote ni kikwete ndo alitembelea Ikulu mara nyingi kuliko wengine. Sasa tena ni tabia hiyo, siyo kwa kutembelea ikulu, bali kusifia na kujiunga na rais ktk safari.
Asichokifahamu Kikwete ni mtazamo wa Watanzania juu ya utawala wake na tabia yake ya mitaani. Kwa ujumla Utawala wa Kikwete haukuwa mzuri au tuseme ulikuwa wa hovyo.
Ni utawala ambao kwa kipindi cha miaka 10, hakuna chochote anachoweza kuwaonesha Watanzania kwamba ndo yalikuwa matumizi ya bajeti ya takribani trilioni 130, isipokuwa makampuni ya kifamilia kwenye mafuta viwanda juisi na magari ya kusafirisha mizigo.
Ushauri wangu kwako Kiwete. Kaa kimya, hata kama una furaha ya Samia kuwa madarakani, wewe siyo tofauti na wastaafu wengine. Hata kama siyo tabia ya makuzi yako kupenda kuonekana, jilazimishe kwa faida ya rais Samia. Hukuwa na sababu ya kusifia utawala wa Samia baada ya uteuzi mpya wa mawaziri, ambao walishiriki utawala wa hovyo ktk awamu yako.
Kama kuna sababu nyingine ya kumsifia Samia, mpigie simu, keep low profile wengi hatukuoni kama ishara ya mafanikio, tangu mijini hadi vijijini. Tanzania ina wasomi wanaoona na ufahamu kuliko hata wewe mwenyewe.