Ushauri wangu kwa Mzee Kikwete katika siasa za Tanzania ya Rais Samia

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
3,851
2,000
Rais Mstaafu Kikwete anamsifia rais Samia kwa utendaji mzuri kama alivyofanya kwa marehemu Magufuli bila kujali machungu ya wa-TZ.

Ni tabia ya kulazimisha kutuonesha uhusiano wake na marais walioko madarakani. Wakati Magufuli akiingia madarakani, kulikuwa na marais wastaafu watatu; Mwinyi, Mkapa na yeye Kikwete. Katika hao wote ni kikwete ndo alitembelea Ikulu mara nyingi kuliko wengine. Sasa tena ni tabia hiyo, siyo kwa kutembelea ikulu, bali kusifia na kujiunga na rais ktk safari.

Asichokifahamu Kikwete ni mtazamo wa Watanzania juu ya utawala wake na tabia yake ya mitaani. Kwa ujumla Utawala wa Kikwete haukuwa mzuri au tuseme ulikuwa wa hovyo.

Ni utawala ambao kwa kipindi cha miaka 10, hakuna chochote anachoweza kuwaonesha Watanzania kwamba ndo yalikuwa matumizi ya bajeti ya takribani trilioni 130, isipokuwa makampuni ya kifamilia kwenye mafuta viwanda juisi na magari ya kusafirisha mizigo.

Ushauri wangu kwako Kiwete. Kaa kimya, hata kama una furaha ya Samia kuwa madarakani, wewe siyo tofauti na wastaafu wengine. Hata kama siyo tabia ya makuzi yako kupenda kuonekana, jilazimishe kwa faida ya rais Samia. Hukuwa na sababu ya kusifia utawala wa Samia baada ya uteuzi mpya wa mawaziri, ambao walishiriki utawala wa hovyo ktk awamu yako.

Kama kuna sababu nyingine ya kumsifia Samia, mpigie simu, keep low profile wengi hatukuoni kama ishara ya mafanikio, tangu mijini hadi vijijini. Tanzania ina wasomi wanaoona na ufahamu kuliko hata wewe mwenyewe.
 
tweenty4seven

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
13,406
2,000
Jk amejenga terminal hiyo mpya meko amekuta jengo linajengwa jk kajenga barabara za kutosha meko hakujenga barabara ...songwe airport, namanga to tengeru ni yeye,mradi mkubwa wa 500bn wa maji ni jk.

Meko amejenga kwa chato airport, kununua madege yasiyoingiza hata mia na kufisadi kwa kujenga miradi mikubwa akiwa yeye ndio mtoa pesa na tenda,ccm oyeee
 
Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
1,157
2,000
Jk amejenga terminal hiyo mpya meko amekuta jengo linajengwa jk kajenga barabara za kutosha meko hakujenga barabara ...songwe airport,namanga to tengeru ni yeye,mradi mkubwa wa 500bn wa maji ni jk...
Wote walewale kuanzia Mwinyi, mkapa,jk,jiwe na huyu hangaya.

Kila mtu hapo majanga tu, kazi kubwa wanayoweza ni kutengeneza vikundi ndani ya serikali
 
Ngigana

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
1,828
2,000
The educated differ from the uneducated as much as the living from the dead --Aristotle !!

Mmmm food for thoughts! :cool:
 
NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,707
2,000
Wote walewale kuanzia Mwinyi, mkapa,jk,jiwe na huyu hangaya.
Kila mtu hapo majanga tu, kazi kubwa wanayoweza ni kutengeneza vikundi ndani ya serikali
kwahiyo aje nani mkuu kama?!! namaanisha kwa ulimwengu huu yupo utakayeridhika nae?
 
Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
2,105
2,000
Jk amejenga terminal hiyo mpya meko amekuta jengo linajengwa jk kajenga barabara za kutosha meko hakujenga barabara ...songwe airport,namanga to tengeru ni yeye,mradi mkubwa wa 500bn wa maji ni jk...
Ajabu ni kwamba, JK anaonekana kama yeye do alianzia kutoka kwa wakoloni. Kazi kubwa ya kupika keki ilifanywa na Ben, msanii alipaka icing sugar tu.

Zaidi, tueleze mafanikio ya kiuchumi wa kinchi yaliyofikiwa na JK. Kisha utueleze uvundo unaosemwa uliotokana na yeye kuanzia akiwa waziri(IPTL) mpaka Symbion, usiache vijini vinyonya damu vyote alivyovitengeneza kwa maslahi ya tumbo lake ambavyo vinarudi kwa kasi.

Angalau tuwe na skeleton, sasa hata hiyo skeleton iliyojengwa na wakoloni, ikaanza kukandikwa kandikwa udogo ili tuje tupate angalau taswira ya mtu, ilikonyolewa konyolewa, hapa tunapojadili, nasikia imebaki miguu tu, haijulikani vipande hivyo vimetupiwa wapi ingawa tetesi zinasema kuna watu wanavyo.
 
Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,021
2,000
Jk amejenga terminal hiyo mpya meko amekuta jengo linajengwa jk kajenga barabara za kutosha meko hakujenga barabara ...songwe airport, namanga to tengeru ni yeye,mradi mkubwa wa 500bn wa maji ni jk.

Meko amejenga kwa chato airport, kununua madege yasiyoingiza hata mia na kufisadi kwa kujenga miradi mikubwa akiwa yeye ndio mtoa pesa na tenda,ccm oyeee
Nadhani umeshindwa kuelewa maana ya trilioni 130 zilizokadiliwa kwa miaka 10 ya utawala wake.
 
Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,021
2,000
NAmi naona tatizo la kukosa Busara. Tangu niliposikia Kikwete alikuwa anasifiwa kwa kuvaa suti, nikajua hatukuwa na rais. Kiwango cha rais hakihitaji tena uvaaji wa suti. Tuliwahi kusikia mzungu kumuhonga rais suti! Au!
 
RAISI AJAE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
2,291
2,000
Angalau maisha tuliyaona!ajira zikapatikana!Fedha zikajaa kitaa!tukala keki ya taifa pamoja!!!!!!Lakini jiwe ameua furaha yote tukawa maroboti yasiyo na chaji kabisa!!JK IS THE GREAT!!!!
 
misasa

JF-Expert Member
Feb 5, 2014
11,652
2,000
Angalau maisha tuliyaona!ajira zikapatikana!Fedha zikajaa kitaa!tukala keki ya taifa pamoja!!!!!!Lakini jiwe ameua furaha yote tukawa maroboti yasiyo na chaji kabisa!!JK IS THE GREAT!!!!
Unakumbuka jobless walijaza uwanja wa Mkapa kwa nafasi zilizokuwa zinahitajika watu kumi tu?

Unajua kipindi cha awamu gani?
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
35,209
2,000
🤡🤡🤡

0AIS-7z.jpg
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom