Ushauri wangu kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale

Feb 14, 2021
61
125
Salaam,

Juzi umepokea hundi yenye thamani zaidi ya 700ml. Kutoka kampuni yenye migodi ya Buzwagi na Kakola ya Twiga Baricck Gold Mine.

Ni fedha nyingi hizo pamoja na fedha zingine unazokusanya katika vyanzo vyako vya mapato.

Ushauri wangu kwako, najua una changamoto nyingi katika wilaya yako, kv. Barabara, hosp, nk. Ukiamua kuelekeza hizi fedha ktk ujenzi wa barabara hutamaliza mtandao wote wa barabara mtk wilaya yako, kadhalika ktk ujenzi wa madarasa na hosp.

Napendekeza ununue MITAMBO MIPYA YA UJENZI WA BARABARA KV. EXCAVATOR, ROLLER COMPACTOR, NA GREADER aina ya CAT. Maana matipa waweza kukodi.

Baada ya kununua sajili kampuni ya ujenzi ambayo utaajiri wahandisi watakaolipwa kwa % ktk kazi wanazofanya. Hii maana yake, hata unapojenga barabara za ndani ya wilaya yako, kampuni hii ya halmashauri ya wilaya ya Nyang'wale muilipe lakini pia, ifanye na kazi ktk maeneo mengine haijalishi ni project za serikali au za makampuni.

Hii itasaidia:

1. Ajira
2. Kuiongezea h/mashauri mapato
3. Kujenga mtandao wa barabara zako kwa mda unaotakiwa.

Maana ukiziingiza hizo hela kulipa wakandarasi. Utajenga kweli lakini zitaisha hela na baada ya muda utahitaji pesa tena kukarabati.
Lakini ukiwa na mitambo katika mfumo wa kampuni utajenga mpaka shule na mahosp kupitia faida za hiyo kampuni.

Nawasilisha tafadhali.

By usinipite mwokozi, ukitaka ushauri zaidi ni in box.
 

The Underboss

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,582
2,000
Nyang'wale si mlikula hela za maendeleo nyie za ujenzi wa hospitali ama zahanati alizowapa Magufuli?

Nakumbuka hadi vigogo wa hapo walitupwa lupango, wametoka?
 

chazachaza

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
1,078
2,000
Mil. 700 ndio unapigia budget ya kununua vifaa vya ujenzi! Hiyo Mia 7ml labda utapata ka roller 1 tena mtumba. Budget ya hizo mashine ni ndefu mkuu, inahitaji fungu kubwa labda waandae angalau 4bln ndio at least wanaweza pata mitambo 3 Hadi 4.
 

Nyalumana originally

Senior Member
Apr 24, 2019
131
500
mil.700 ndo unapigia budget ya kununua vifaa vya ujenzi!!! hiyo Mia 7ml labda utapata ka roller 1,tena mtumba.budget ya hizo mashine ni ndefu mkuu.inahitaji fungu kubwa labda waandae angalau 4bln,ndo at least wanaweza pata mitambo 3 Hadi 4.
Aisee Excavator tena ya CAT mpya inaongelewa kwenye M900 km si 1b. Nadhan ushauri wako ni mzuri sana, mia 7m ni pesa kidogo sana kwa kununulia hizo mitambo labda km ananunua excavator aina ya Case anaweza bakiza change ya kununua angalau gari za kichina aina ya FAW TIPPER au HOWO km 2. Make akiwa na Case 1 itachimba na kupakia kwenye hizo tipper 2 halafu akodishe Grader kwa kusambazia kifusi na kugrade barabara.

Note: Vifaa vya Case vyaweza kudumu 5-10yrs km vina matunzo mazuri na FAW mwisho miaka 5 ishakuwa right off. Nadhani hapo katkati utakuwa umepata fund nyingine ya kununua kingine. Mungu akupe hekima katika utekelezaji wa miradi ya serikali kwa manufaa ya wananchi wako. Husinunue LIV8
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom