Ushauri wangu kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
Wanabodi,

Baada ya serikali kuhamishia makao makuu yake jijini Dodoma iliweka wazi kwamba, Jiji la Dar es Salaam lililokuwa makao makuu, sasa ni Jiji la Kibiashara.

Lakini cha ajabu, Jiji la Kibiashara, bado biashara zinafanywa kwa masharti. Mfano; bado baa zinauza pombe kwa muda na kufunga baa kwa masharti ya muda.

Bado maduka makubwa ya kuuza bidhaa mbalimbali, yanafungwa kwa muda wa usiku kucha na kufunguliwa baada ya jua kutoka.
Bado, daladala nyingi zinalala saa tano usiku na kuanza kazi alfajiri.

Namshauri mkuu wa mkoa wetu ambaye si mpaza sauti sana ila ni mtekelezaji, aweke mazingira mazuri ili Jiji liendane na sifa ya Kibiashara.

Endapo biashara zitakesha, daladala zitakesha (automatiki). Endapo baa zitakuwa saa 24, daladala zitakesha (automatiki). Kwa sasa baadhi ya maeneo daladala hazipo usiku kwa sababu hakuna abiria. Watapatikanaje wakati baa saa tano zimefungwa?

Abiria watapatikanaje wakati maduka Kariakoo saa moja yanafungwa?

Sifa ya Jiji la Kibiashara ni shughuli zote kuwa wazi kwa saa 24. Hao wafanyabiashara wenye jiji lao, wanasema baishara haina saa.

Ahadi ya biashara hata saa sita usiku. Mchana kutwa wamelala. Ahadi ya biashara hata saa kumi na moja alfajiri, usiku kucha wamelala.

Nakusihi RC tafakari sifa za Jiji kuwa la Kibiashara kisha waandalie mazingira wezeshi. (kidogo niseme Amina).
 
Waongeze idadi ya askari wa doria usiku,waongeze "FARASI MWEUPE" ziwe zinapaki sehemu za kibiashara ili "MAJAMBAWAZI" wasiwe wanapora fedha hasa wakati wa usiku.

Mkuu wa Mkoa amepoa sana hana amsha amsha kama za KIGANI.
 
Kune boy kazubaa sana.. wampeleke hata shinyanga huko.. dsm inataka watu wenye hamsha hamsha kama za makonda.
 
Waongeze idadi ya askari wa doria usiku,waongeze "FARASI MWEUPE" ziwe zinapaki sehemu za kibiashara ili "MAJAMBAWAZI" wasiwe wanapora fedha hasa wakati wa usiku.

Mkuu wa Mkoa amepoa sana hana amsha amsha kama za KIGANI.
Hivi Kupiga piga kelele hovyo ndio utendaji kazi? mwache afanye kazi iliyotukukuka siyo kufanya kazi kwa kujionyesha kwenye macamera kila siku.
 
Hivi Kupiga piga kelele hovyo ndio utendaji kazi? mwache afanye kazi iliyotukukuka siyo kufanya kazi kwa kujionyesha kwenye macamera kila siku.

Hahahaa naona utofauti wa KIGANI na RC Mpya!! KIGANI anapenda MAKAMERA nikajua na yeye atafuata nyendo za KIGANI.
 
Back
Top Bottom