NAFIKIRE
JF-Expert Member
- Sep 5, 2014
- 660
- 454
Salaam kwako;
Nianze kwanza kwa kukupongeza kwa kazi kubwa unayoifanya ya kuingoza nchi yetu.Hongera sana ; kazi ni nzuri kwa taarifa za huku mtaani.
Mkuu naomba nikushauri kuyafanyia kazi mambo matatu au matano ambayo yatakufanya uzidi kukubalika na kuwa juu na zaidi kuwasaidia wanafamilia wanyonge katika kaya yako:
1.Elimu
Mkuu kwa waalimu ukiwapa tu monthly allowance kama askari utakuwa umefanya kitu kikubwa sana na uchaguzi ujao watakupitisha kwa kishindo.
Mkuu waalimu ukiwajengea nyumba za waalimu nzuri utatisha mkuu
Mkuu ukilipa madeni ya waalimu utazidi kufunika mkuu.
Mkuu ukiboresha shule za walemavu ambazo hali yake kwa sasa ni dhoofu hali utatisha mkuu.
Mkuu ukirudisha shule za ufundi kama zamani katika ubora wake utatisha mkuu.
Mkuu boresha na mahabara na masilai kwa walimu wa sayansi uone tz itakavyopaa kwenye fani ya sayansi
2.Usalama
Mkuu jenga nyumba za polisi hali yake kwa sasa inatisha..
Mkuu ongeza maslai yao na vitendea kazi
Mkuu mgambo wape ajira kamili utakuwa umeongeza ajira kwa watu wanaomaliza msingi na kushindwa kuendelea na masomo na kuongeza usalama kwa kiwango cha kata,kijiji na mtaa
Mkuu ongeza kambi za Jkt ikiwezekana kila mkoa au wilaya
Mkuu hawa bodaboda na madereva wote kuwapa uzalendo amuru wapitie jkt kama kigezo cha kufanya hiyo kazi.
3.Utendaji serikalini
Mkuu wenyeviti wa mitaa na vijiji walipwe mishahara.
Wazee maskini vijijini walipwe angalau elfu hamsini kwa mwezi.
Mkuu amuru kila wilaya iwe na kiwanja kikubwa cha watoto na watu wazima kustarehe wakati wa sikukuu.wakati wa sikuu pawepo sehemu ambayo imetengenezwa vizuri na mamlaka ya mji kwa watoto kufurai na watu kupumzika..mfano Nyerere squre Dodoma..ila iwe kubwa zaidi.
4.Michezo
Mkuu tunakuomba uanze kujenga viwanja vya michezo kwenye miji mikubwa kama Mwanza, Moshi, Tanga,Mbeya,Mtwara, Dodoma ...miaka michache ijayo ukiwa madarakani tuweze kuandaa...michuano mikubwa kama kombe la africa au kombe la dunia.
Mkuu jenga sasa chuo kikubwa cha mziki...mziki unalipa sana ila sasa hivi wanamziki wengi hawana taaluma ya mziki.
Mkuu somo la mziki lifundishwe kuanzia shule ya msingi kwa msisitizo mkubwa na masomo mengine ya sanaa.
5.Viwanda
Mkuu anzisha VETA kila wilaya na viwanda vidovidogo kila wilaya hapa utakuwa umelenga kundi kubwa la vijana.
Mkuu kama inawezekana anzisha viwanda vya magari,pikipiki,bajaji, baskeli na vifaa vingine hapa nchi.unaweza kufanya kwa kuingia ubia na viwanda vya nje vije Tz kutengeneza hizo bidhaa zao hapo.kulinda soko lao bidhaa zao unazuia uingizaji wa magari,pikipiki,na vifaa vingine kama ulivyofanya kwenye sukari.soko letu ni kubwa sana.
Mkuu kulinda soko la viwanda vyetu vya nguo piga marufuku kuingiza mitumba..
Mkuu ninakutakia mafanikio katika kuiongoza kaya yako ya awamu ya tano.
Mimi ni mmoja wa wanaokuunga mkono katika utendaji wako hasa huu wa kurekebisha mishahara mwenye milioni 36 na wa laki tatu..Kila la kheri.Mungu ibariki Tanzania.