vicdala55
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 1,009
- 1,638
Kwa heshima na Utii naomba kumshauri Mheshimiwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kufanya mabadiliko katika nafasi ya katibu Mwenezi. Nafahamu ni vigumu sana kumshauri Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi bila kumshauri Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati umefika wa kufanya mabadiliko kwenye nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa. Chama Cha Mapinduzi ni Chama kikongwe Afrika na duniani kwa ujumla, ni Chama Mama miongoni mwa vyama vya siasa Afrika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni aibu Chama cha Mapinduzi kuwa na msemaji wa aina ya huyu aliyepo sasa. Duniani na Afrika bila shaka wanajiuliza kama huyu ndiye msemaji wa CCM ya Mzee Kikwete, Mzee Warioba, Mzee Butiku na Mzee Mkapa? Si ajabu wanajiuliza kama huyu ndiye msemaji wa CCM aloiacha Mwalimu Nyerere? Bila shaka wanajiuliza kama huyu ndiye msemaji wa CCM inayoongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM, nafahamu kuwa kuna kauli nyingi za ajabu zitokazo kinywani kwa Katibu Mwenezi Taifa hata wewe huwa huzifurahii, lkn pengine huwa unazivumilia kwa kuwa huwa zinaelekezwa kwa wapinzani wa CCM kisiasa. Lkn Mheshimiwa Mwenyekiti, kauli hizi hazina matokeo chanya katika mustakabali wa kisiasa kwa Chama Cha Mapinduzi.
Kauli ya hivi karibuni kwamba Taifa haliwezi kuzuia wageni kuja Nchini kwa muda kisa Corona ni kauli isiyo ya kizalendo kwa Taifa, inaonyesha jinsi CCM isivyojali usalama wa Watanzania kiafya na kimaendeleo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa linaloumwa ni Taifa ambalo kamwe haliwezi kujenga uchumi wake, haliwezi kulinda mipaka yake na kamwe haliwezi kujitegemea.
Kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi ikiachwa ipite, tafsiri yake ni kwamba CCM haina shida na matatizo ya Watanzania, bali ipo tayari Watanzania wafe lkn Taifa lipate pesa.
Kauli hiyo imeambatana na kauli kwamba Wapinzani wa CCM kisiasa ni sawa na Corona na watashughulikiwa sawa na Corona. Kauli hatari kama hiyo haiwezi kutolewa na Msemaji wa CCM.
Nchi nyingi zilizoathirika na Corona pengine zaidi kuliko Tanzania zina mfumo wa vyama vingi, zina ushindani mkubwa kisiasa pengine kuliko Tanzania, mfano Kenya na Marekani, lkn katika Nchi hizo huwezi kusikia chama tawala kikiwafananisha wapinzani wake kisiasa na ugonjwa wa Corona.
CCM inabidi ijitenge na ujinga huu hatari. Mheshimiwa Mwenyekiti, ni busara iliyo na haki kumwondoa Katibu wa Itikadi na Uenezi aliyepo, hajui uzito wa nafasi aliyonayo, imemwelemea, haiwezi, na zaidi anakichonganisha chama na kukichafua mbele ya jamii ya wastaraabu wa ngazi za Kitaifa na Kimataifa. Anaitangazia Dunia kwamba CCM ya sasa ni mbaya zaidi ya makaburu.. Ni aibu CCM kutazamwa katika mizania hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ipe CCM msemaji atakaeifanya CCM irudishe heshima yake kwa Umma wa Watanzania na jumuiya y Kimataifa.
CCM imara ndio msingi wa Serikali imara na inayoheshimika.
Sent using Jamii Forums mobile app