Ushauri Wangu kwa Mhe. Kikwete Kuhusu Baraza la Mawaziri

  • Thread starter Gosbertgoodluck
  • Start date

Gosbertgoodluck

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
2,865
Likes
32
Points
0
Gosbertgoodluck

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
2,865 32 0
Mhe. Rais,

Awali ya yote ninaomba nitangaze rasmi kwamba nimeamua kukubaliana na matokeo yaliyokuwezesha kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya pili tena. Malalamiko yapo mengi mitaani kwamba chama chako kimeitumia serikali kuwezesha ushindi wako. Mimi binafsi nimetafakari sana suala hili. Hatimaye nikakumbuka neno moja muhimu nalo ni kuwa hakuna mamlaka hapa duniani isiyotoka kwa Mungu. Kwa hiyo, nimeamua kuamini kwamba ushindi wako umetokana na matakwa ya Mungu.

Nikiwa mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi yangu na ninayefuatilia kwa ukaribu sana mwenendo wa maisha ya watanzania kijamii, kisiasa na kiuchumi, ninaomba nitoe ushauri wangu kwako kuhusu baraza la mawaziri utakaloliunda hivi karibuni. Kumbuka kuwa baraza la mawaziri ndiyo "machinery" yako itakayokuwezesha kutimiza lundo la ahadi zako kwa wapiga kura waliokupatia ushindi. Kwa hiyo, unapoteua timu (baraza la mawaziri) ni vizuri uweke pembeni urafiki, undugu, ukabila na udini na badala yake zingatia zaidi uwezo wa mtu. Mhe. Rais, kwa nini ninasema hivi. Nitaeleza. Kumbuka kuwa hii ni awamu yako ya mwisho kuongoza nchi yetu. Nina hakika kabisa kwamba katika awamu yako ya kwanza umefanya mambo mengi ambayo usingependa uyarudie na kuendelea kuchafua sifa yako. Ni ukweli usiokwepeka pia kwamba katika uongozi wako nchi imeshuhudia kashfa nyingi ambazo kwa kiwango kikubwa zimeharibu sura ya serikali na chama chako. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amekupatia tena miaka mitano ya kuongoza nchi yetu, nina imani kwamba hutaifanyia mzaha fursa hii ya mwisho kwani ndiyo itakayoamua heshima yako mbele ya jamii, baada ya kustaafu. Wapo viongozi wastaafu wanapopita barabarani wananchi wanawazomea na vilevile wapo viongozi wastaafu wanapopita barabarani wananchi wanawashangilia. Yote hiyo inatokana na rekodi zao wakati wa utumishi wao kwa umma.

Sasa basi, kama nilivyosema, nikiwa mwananchi mpenda nchi yangu ninakushauri uunde baraza la mawaziri lenye sifa zifuatazo:

(i) Liwe na idadi ndogo ya mawaziri, kadri inavyowezekana.
(ii) Idadi kubwa ya mawaziri itokane na wabunge 10 utakaowateua ili kuendana na msimamo wa wanazuoni wengi kwamba mawaziri ambao ni wabunge wa majimbo wanakosa muda wa kuwawakilisha wananchi wao.
(iii) Liwe na sura ngeni ili kuleta matumaini mapya kwa wananchi. Natambua itakuwa vigumu sana kutekeleza hili lakini jitahidi kadri uwezavyo kubadili sura. Mawaziri ambao bado wana nafasi nzuri ya kukusaidia ni pamoja na Mhe. Prof. Mark Mwandosya, Mhe. Dr. Pombe Magufuli, Mhe. Mizengo Pinda na Mhe. Prof. Mwakyusa. Wapo wengine, maana wewe ndiye unayewafahamu zaidi lakini mawaziri hao niliowataja utumishi wao ni wa kutukuka. Mawaziri wengine wa awamu iliyopita ni vizuri uwapumzishe.

Mhe. Rais suala la "sura ngeni" ni vizuri pia ukalizingatia hata katika uteuzi wako wa wakuu wa mikoa na wilaya. Ukweli ni kuwa sura hizohizo zinawachosha wananchi na kupoteza matumaini. Nchi yetu ni kubwa na wananchi wake ni wengi. Haingii akilini kuona baadhi ya viongozi tulio nao leo walikuwepo tangu wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Kama ni uwezo wa kupambana na changamoto za kujenga nchi utakuwa umepungua kama siyo kwisha kabisa.

Kwa heshima na taadhima, naomba kuwasilisha.
 
Bob_Dash

Bob_Dash

Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
91
Likes
4
Points
0
Bob_Dash

Bob_Dash

Member
Joined Nov 1, 2010
91 4 0
Nimesoma ubeti wa kwanza, nitarudi tena kumalizia beti zilizobaki
 
C

chelenje

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Messages
554
Likes
2
Points
0
C

chelenje

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2010
554 2 0
Mkuu ushauri wako mzuri japo siyo lazima kuutekeleza, tuonane 2015...
 
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2008
Messages
7,113
Likes
1,308
Points
280
B

Bulesi

JF-Expert Member
Joined May 14, 2008
7,113 1,308 280
Mhe. Rais,

Awali ya yote ninaomba nitangaze rasmi kwamba nimeamua kukubaliana na matokeo yaliyokuwezesha kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mara ya pili tena. Malalamiko yapo mengi mitaani kwamba chama chako kimeitumia serikali kuwezesha ushindi wako. Mimi binafsi nimetafakari sana suala hili. Hatimaye nikakumbuka neno moja muhimu nalo ni kuwa hakuna mamlaka hapa duniani isiyotoka kwa Mungu. Kwa hiyo, nimeamua kuamini kwamba ushindi wako umetokana na matakwa ya Mungu.

Nikiwa mtanzania mwenye mapenzi mema na nchi yangu na ninayefuatilia kwa ukaribu sana mwenendo wa maisha ya watanzania kijamii, kisiasa na kiuchumi, ninaomba nitoe ushauri wangu kwako kuhusu baraza la mawaziri utakaloliunda hivi karibuni. Kumbuka kuwa baraza la mawaziri ndiyo "machinery" yako itakayokuwezesha kutimiza lundo la ahadi zako kwa wapiga kura waliokupatia ushindi. Kwa hiyo, unapoteua timu (baraza la mawaziri) ni vizuri uweke pembeni urafiki, undugu, ukabila na udini na badala yake zingatia zaidi uwezo wa mtu. Mhe. Rais, kwa nini ninasema hivi. Nitaeleza. Kumbuka kuwa hii ni awamu yako ya mwisho kuongoza nchi yetu. Nina hakika kabisa kwamba katika awamu yako ya kwanza umefanya mambo mengi ambayo usingependa uyarudie na kuendelea kuchafua sifa yako. Ni ukweli usiokwepeka pia kwamba katika uongozi wako nchi imeshuhudia kashfa nyingi ambazo kwa kiwango kikubwa zimeharibu sura ya serikali na chama chako. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amekupatia tena miaka mitano ya kuongoza nchi yetu, nina imani kwamba hutaifanyia mzaha fursa hii ya mwisho kwani ndiyo itakayoamua heshima yako mbele ya jamii, baada ya kustaafu. Wapo viongozi wastaafu wanapopita barabarani wananchi wanawazomea na vilevile wapo viongozi wastaafu wanapopita barabarani wananchi wanawashangilia. Yote hiyo inatokana na rekodi zao wakati wa utumishi wao kwa umma.

Sasa basi, kama nilivyosema, nikiwa mwananchi mpenda nchi yangu ninakushauri uunde baraza la mawaziri lenye sifa zifuatazo:

(i) Liwe na idadi ndogo ya mawaziri, kadri inavyowezekana.
(ii) Idadi kubwa ya mawaziri itokane na wabunge 10 utakaowateua ili kuendana na msimamo wa wanazuoni wengi kwamba mawaziri ambao ni wabunge wa majimbo wanakosa muda wa kuwawakilisha wananchi wao.
(iii) Liwe na sura ngeni ili kuleta matumaini mapya kwa wananchi. Natambua itakuwa vigumu sana kutekeleza hili lakini jitahidi kadri uwezavyo kubadili sura. Mawaziri ambao bado wana nafasi nzuri ya kukusaidia ni pamoja na Mhe. Prof. Mark Mwandosya, Mhe. Dr. Pombe Magufuli, Mhe. Mizengo Pinda na Mhe. Prof. Mwakyusa. Wapo wengine, maana wewe ndiye unayewafahamu zaidi lakini mawaziri hao niliowataja utumishi wao ni wa kutukuka. Mawaziri wengine wa awamu iliyopita ni vizuri uwapumzishe.

Mhe. Rais suala la "sura ngeni" ni vizuri pia ukalizingatia hata katika uteuzi wako wa wakuu wa mikoa na wilaya. Ukweli ni kuwa sura hizohizo zinawachosha wananchi na kupoteza matumaini. Nchi yetu ni kubwa na wananchi wake ni wengi. Haingii akilini kuona baadhi ya viongozi tulio nao leo walikuwepo tangu wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Kama ni uwezo wa kupambana na changamoto za kujenga nchi utakuwa umepungua kama siyo kwisha kabisa.

Kwa heshima na taadhima, naomba kuwasilisha.
Hao unaowapendekeza kuwa ni watendaji wa kutukuka mbona wamekaa kwenye uwaziri miaka chungu nzima lakini wananchi kero za maji ni zile zile si mijini bali hata huko vijijini!!
 
Utotole

Utotole

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
6,528
Likes
3,340
Points
280
Utotole

Utotole

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
6,528 3,340 280

Mkuu, pamoja na mengine unayoweza kuwa umesema, nimeamua kuishia hapo kwanza nipumzike maana hiyo Red inatia mashaka. Kuna mamlaka nyingine ni za mabavu na hazistahili kuvumiliwa. Na kuna nyingine hata kama mabavu yake hayakuwa wazi, hila inaweza kuwa imetumika kufanikisha hilo. Hata hivyo kwa kuwa mtekelezaji wa ushauri huo si mimi, naamimi rais atasoma (au atasomewa) na atatekeleza kama atapenda kukusikiliza.
 
Forum statistics

Threads 1,237,971
Members 475,809
Posts 29,308,317