Ushauri wangu kwa JK kuhusu tatizo la Z'bar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wangu kwa JK kuhusu tatizo la Z'bar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Userne, May 30, 2012.

 1. U

  Userne JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 895
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakubwa! Hamkani si shwari!
  Ushauri nautoa kwako Mh sana JK!
  Kwa MAMLAKA ULIYONAYO AMUA hili leo kwa ajili ya utulivu wa nchi yetu;

  1 TANGAZA HALI YA HATARI ZENJ au VUNJA MUUNGANO!
  Zaidi ya hapo MUDA UTASEMA!
  Kwa hilo UTAKUMBUKWA!
   
 2. Atabase Agaya

  Atabase Agaya Senior Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Extempore!
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Tena muda hii hii
   
 4. W

  Welu JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 815
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Nitaulinda muungano! (katiba) sasa avunje muungano, je wale wanaoushughulikia watakula wapi? Huoni unabuni kitu hata kama hakina manufaa kwa sera ya nchi ya kuongeza ajira ili maisha bora kwao yawezekane? Kalagabaho! Je ni nchi ipi duniani yenye MARAIS WATANO (5) ? 2+3 ama Tz kila kitu kinawezekana.
   
 5. U

  Userne JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 895
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkubwa! Ni ushauri tu! Anaeshauriwa ana haki ya kukubali ima kukataa!
   
 6. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  wale jamaa ni kupeleka JWTZ wapigwe bakora mpaka wakome, hakuna kuvunja muungano hapa, watatusumbua sana zanzibar itakuwa njia ya magaidi, Dar es salaam,Tanga na Mtwara hazitakuwa sehemu salaaam tena
   
 7. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  I beg to differ mkuu

  Wahenga wanasema mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni

  1. Huko kwenye machafuko kuna serikali kamili with full mandate sasa hapo huyu JK atangaze hali ya hatari vipi?????
  2. Mihadhara mpaka imerekodiwa na kuwekwa humu hiyo serikali yao imefanya nini ku control the direction and magnitude ya intended effects...............muted


  Kwa mnaosema ukivunjika muungano hatutakuwa salama.....i do hope and wish for that....you are not mocking our Forces...!!!!!! Yaani leo Anjuwan....Sudan Kusini.....Darfur.....just to name a few tunaweza hukoooo. Then tushindwe kujilinda wenyewe?????? Please please spare the Tasks just this moment

  Paka na afungwe kengele tumjue......shida haiko na "muungano" bali huko Visiwani wanalo wanalolitaka na wawe wazi ili kujulikane mbivu na mbichi.

  Viongozi wa nchi hii kwa heshima na taadhima..........ukweli na uhalisia uchukue mkondo wake kwanza halafu busara itafuatia pindi ukweli na uhalisia utakapokuwa umefahamika....ule Utanzania wa mapenzi na umoja nadhani haupo au unatoweka kwa kasi kubwa sasa, inabidi kuweka mambo bayana na tuanze upya kwa yale yenye kuridhiwa na kila mshiriki katika umoja wowote ule uwao. Dalili ziko wazi kuwa kuna baadhi ya wenzetu yawezekana wana ajenda ambayo haiwapendezi wengi lakini ndo ukweli wanaoutaka na wameamua kuusimamia kwa vitendo

  I love my country but unfortunately not all of my country men.......be blessed my lovely country TANZANIA
   
 8. U

  Userne JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 895
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkubwa! JK ameapa kulinda muungano! Na MAMLAKA yake ni hadi Zenj! Hivyo basi ni kweli kabisa hawezi kukwepa mamlaka yake kama Raisi wa Muungano kulingana na kiapo chake! Mbona Said Mwema yuko kule?
  Naomba Mkuu mshauri JK ili tatizo la Zenj liishe na kuwa historia, mimi binafsi nimeona ktk hayo niliobandika pana ufumbuzi wa kudumu!
   
 9. u

  utenguleone Senior Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 150
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  :evil:
   
 10. B

  BOTOPLAM Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna kipindi fulani hivi kama mwaka na zaidi ulopita, nilisikia hotuba ya huyu MKUU ikionyesha kutokupendezwa na mambo yanayozungumzwa kwenye MIHADHARA na ilikuwa kama event ya Ki-dini fulani hivi na akacomment kwamba maadili na ustaarabu wa wananchi ufuatwe, ila sijui iliishia wapi.
  Hivi vitu ndo vinahitaji ufuatiliaji wa karibu zaidi kuliko kusubiri kutangaza hali ya hatari, sababu ukipita sehemu ambako mihadhara inafanyika daily, kama una roho nyepesi unaweza kuhisi nchi imeshagawanyika (WAKAZI WA DAR HAPO NI MASHAHIDI HASA WA SEHEMU ZA MAGOMENI, BIG BROTHER, SINZA, n.k.) Pale kuna watoto, vijana, wazee, viongozi wa kidini na watu wasio na dini rasmi! Mfano inaposikika kwamba MUNGU wa watu fulani hafai kuitwa Mungu kwa kuporomosha msululu wa mabaya yake ya KUTENGENEZWA, kila anayesikia anajenga hali fulani ya kutaka kujitenga na wale wenye imani chafu kwa njia yoyote, sasa tusipothibiti tabia hii tangu chini tukasubiri watu wameshalishwa sumu kwenye mihadhara na kujiona wao ndo wenye imani hapa duniani, unadhani haya yataacha kutokea?
  Mimi kama ningepata nafasi ya kumshauri huyo MKUU, nisingesema atangaze hali ya hatari Zenji, badala yake yeye na wizara zake zinazohusika na mambo ya Ulinzi, Jamii, Sheria, Elimu, n.k wawe na ufuatiliaji wa karibu wa mambo yanayozungumzwa huko kwenye mihadhara. Na pengine katiba zetu zipunguze huu uhuru wa kuabudu kiasi kwamba hata lugha zinazotumika kwenye nyumba za Ibada zilenge kuwafanya waumini kumpenda MUNGU zaidi kuliko kujadili madhahifu ya imani nyingine, sababu Tanzania tunayoijenga si ya kuyeyuka kama barafu baada ya miaka 10 au 20, ni taifa litakalozidi kuwepo kwa vizazi vijavyo. Ni bora waumini wafundishwe Upendo na kuvumiliana kwa wenye imani SAHIHI na zile nyingine wanazoziona FEKI, yaani kama Biolojia inavyo eleza juu ya Ikolojia kwamba viumbe wote wanategemeana kwenye zile CHAINS (Cycles). Nasi binadamu tuko hivyo LAZIMA WAWEPO WASIO NA IMANI NDO UONEKANE WEWE MWENYE IMANI, LAZIMA WAWEPO WANAOONGOZWA NDO UWEPO WEWE KIONGOZI, LAZIMA WAWEPO WASOMAJI NDO TUWEPO SISI WACHANGIAJI, VIVYO HIVYO HATA KWA TAJIRI NA MASIKINI (ingawaje hakuna anayependa kukaa na hali hiyo).
  Nayasema haya 7bu mi binafsi naishi kando ya Msikiti, kuna siku ambazo anaalikwa jamaa mmoja anaitwa msemaji (sijui msemaji au mswalishaji hodari), sifa yake kubwa ni kuwa anajua kuutetea uislam Tanzania nzima (siwezi kujua kama ni mmoja au wako wengi watetezi). Sasa siku akija pale kwetu, kwanza volume ya vipaza sauti inaongezwa na sina hakika kama wote wanaofika siku hiyo ni wenye kujiandaa kwa swala na kutimiza nguzo 5 kila siku, kwani sauti za kushangilia zingekuwa ndo za kuswali kila siku hasa Ijumaa, majirani tungekwisha hama kwa kupisha vishindo hivyo.
  Leo yako Zanzibar tutangaze hali ya hatari, ambako waliochomewa nyumba za ibada ni rahisi kuwanyamazisha na wao kuogopa na kukimbia kimya kimya kwa idadi yao ni kati ya asilimia 1 hadi 3, na kesho ikiwa bara ambako wanasema wao ni fifty-fifty na ikatangazwa hali ya hatari, itakuwaje?
  Kama UAMSHO ni muhimu Tanzania, na tunastahili kuendelea kuusajili kama njia ya kukuza imani kama inavyofanyika mikutano ya Injili na dhana ya UPONYAJI WA KIROHO na MAOMBEZI, basi ubadilishe mtazamo, watakaofika waelezwe umuhimu wa kumjua Mungu na kuwa na mapenzi mema kwa wale ambao hawajawa na mwamko wa kiimani including makafiri.
  Naomba kuwasilisha!
   
Loading...