Ushauri wangu kuhusu ajira zinazotolewa na Serikali

Ego is the Enemy

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
7,406
14,169
Habari zenu wanajukwaa!

Haya ni maumivu makubwa sana kwa umma sijui ni private issue ila ninaliona kuwa ni janga kubwa sana tuendako.

Yaani nineshangaa sana ajira nafasi 21 kanda ya Engineer two TANROADS, wameitwa kwenye usaili takribani watu 1223 exactly. Hili linaashiria nini?

Kuwa vijana hawana ajira ama wana ajira wasiyoitaka. Ama kweli kaa tayari watu wameshajulikana halafu hawa wote wasumbuke mpaka Dar ni laana sana kwa hao watu na iwatafune mpaka kizazi chao cha NNE.

Nina imani sasa hivi hata huko kwetu Muriba, Keisangora, Nyamwaga, Kimusi, Liwale Ngorongopa, Misasi, Lupaso, Songea walikokuwa wakichunga ng'ombe wamesoma nako jamani sio kama kipindi kile walijazana Wa Tigray tu wakatuamianisha kuwa wao pekee ndo wamesoma.

Haki iwatendekee vijana ambao wazazi wao walicheza ngoma na kuomba taarabu Leo hii wanaitafuta hii ajira. Mana tuliaminishwa kuwa kuna mikoa Iko nyuma kimaendeleo sijui huko Mtama, Ruangwa, Lindi, Mtwara, na kwingineko pia ambako mnakaa mnaaminishwa ivyo.

Wapewe pia nafasi kama watafaulu na ile baba kanituma isiwepo ama kisa MTU amejitolea iwe kigezo.
 
Pia vijana mlioko vyuoni kuweni makini na kozi mnazochagua usichague kozi kisa na wewe uonekane kama mtabe umefaulu PCM points 3 one division.

Mana huko bado mnaenda kwa crowd judgment. Ila ukiingia mtaani hakuna mtaa unaotambua wani yako.

Nashauri serikali ipunguze miaka ya kusoma ili hata kijana akimaliza degree yake anaweza akaja akaanza sifuri mtaani hata anachoma mahindi na bado akatoboa.

Nchi nyingi wanasoma miaka 11 baada ya hapo ni chuoni. Yaani wanamaliza wakiwa na miaka kama 21-23 kwa degree ya miaka mitatu mpaka mitano respectively.

Ya kwangu ni Hayo tu mwenye maoni namna ya kuiboresha nchi yetu alete.

Sio mitano tena ni 20 tena mana wapinzani walituchelewesha sana. Saivi ni mwendo Wa spidi mia kidogo kufikia dona kantri
 
Umenichekeshaje mkuu. Yaani tokea mwaka umeingia sijacheka ujue wee umenifungua mwaka kwa kucheka jamani.
Nikuulize kidogo ni kwa nini akili yako imekuwa hasi sana ukaishia kuiona hasi tu ndugu. Ina mana yote wewe umejikita tu hapo. Haya bana ni kichwa chako mie sitii neno
Sasa wapinzani wameingiaje kwenye uzi wako, au lengo ni FUTUHI?
 
Mkuu hata usilalamike sana
Cha muhimu we jiandae tu vizuri, mwombe Mungu sana na nenda kapige pepa idadi ya watu isikutishe.
 
Back
Top Bottom