Ushauri wangu; CHADEMA fanyieni kazi mambo haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wangu; CHADEMA fanyieni kazi mambo haya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Feb 29, 2012.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kuna mambo na vitu vitokeapo katika Jamii huwa na ushawishi mkubwa na mara nyingine huacha alama au urithi (Legacy) kubwa katika maisha ya mtu au Jamii. Wanadamu na Taasisi (kwa kuwa huongozwa na wanadamu) huacha urithi (legacy) ambayo itadumu katika maisha yote hata baada ya Mtu au Taasisi hiyo kuondoka, ingawa alama hiyo yaweza kuwa ya kuigwa au ya kupuuzwa.

  Sio siri, CHADEMA (kama Chama cha Siasa na Taasisi) kina m chango mkubwa katika siasa za nchi yetu, CHADEMA (kama Vyama vingine vya siasa) kina ufuasi mkubwa katika nchi hii; hasa kwa wapenda mabadiliko.

  Mambo yaliyotokea na yanayotokea na kukikuta CHADEMA, yanaiachia CHADEMA somo la kujifunza na pengine mambo yapasayo kufanyia kazi ili kuendeleza ushawishi kwa wananchama na wapenzi wake kama Chama cha Siasa. Mambo mengi hutokea na kuandikwa sana kuhusu CHADEMA au Viongozi wake.

  Mimi Ibrah, kama mshabiki na mwenye kuiwazia mema CHADEMA na Tanzania, kwa kuzingatia mambo yaliyojiri na yatayoendelea kujiri na kuiathiri CHADEMA kwa njia chanya ama hasi, napendekeza CHADEMA kuyafanyia kazi mambo yafuatatayo (kama hayajafanyiwa kazi):-

  1. CHADEMA wafikirie kuanzisha Taasisi au (Wakfu) ya Uongozi wa Vijana ya Regia Mtema (Regia Mtema Youth Leadership Institute/ Foundation)
  Hii ni kumuenzi Mwanasiasa kijana Regia, aliyefariki mapema mwaka huu. Nazingatia maelezo au nasaha fupi za Mwenyekiti Mbowe siku ya kuuga mwili pale Karimjee Hall Dar es salaam, kuwa Regia aliandaliwa na Chama kiuongozi. Pia kwa kuzingatia mchango mkubwa wa marehemu Regia Mtema katika Chama, Nchi na Vijana wa Tanzania na alivyokuwa tayari kukusolewa na kukiri udhaifu pale inapobidi. Vijana wana nafasi ya kuiga na kujifunza kutoka kwa Marehemu Regia.

  2. Nishani ya Uongozi wa Vijana ya Regia Mtema (Regia Mtema Youth Leadership Award)
  Kama wazo la hapo juu halifai kwa sababu yoyote ile basi hili la Nishani linaweza kufaa kuwaenzi Vijana au Kijana yeyote, wa Chama chohote, au asiye na Chama ambaye ameliachia urithi mwema taifa hili au amelifanyia jambo Taifa letu.

  3. Kuanzisha Idara/ Kurugenzi ya Sera, Itikadi na Oganaizesheni ya CHADEMA.
  Jana, kuna Mdau anaitwa Tuntemeke, alikuja na bandiko lake kutuhumu CHADEMA kutumia shilingi 19,000,000/- na kumkabidhi mwanachama mmoja John Mrema afanye Visibility/ Feasibility Study katika Jimbo la Arumeru Mashariki. Kilichonishangaza ni mashambulizi aliyorushiwa na baadhi ya Vijana wa BAVICHA (naamini ni wao) kwa kashfa na kubandikwa majina yasiyo yake. MAjeraha ya Uchaguzi wao yakahamishiwa kwake! Yawezekana alikuwa na lengo baya au zuri, lakini majibu ya hoja za baadhi ya Vijana wa BAVICHA yalinishangaza sana na yalionyesha upungufu mkubwa wa uvumilivu na hoja za baadhi yao kiasi cha kunifikirisha kuwa Uongozi wa CHADEMA una kazi ya ziada ya kufanya kuhusu BAVICHA; kuwaelimisha na kuwalea katika misingi bora ya Kiachama badala ya misingi ya rika.

  Wakatabahu,
  Ibrah,
  JF
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ibrah subiri tu haki yako.

  Wakatabahu,
  Kimbunga
  JF.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ibrah,

  Yako Ni mawazo murua sana, na bila kuweka ushabiki wowote yatasaidia sana kuimarisha chama kwa siku za usoni!

  Lakini pia 1,2 na 3 vikitekelezwa, dhana inayopigiwa propaganda na wapinzani wa cdm kuwa kuna ni chama cha ukabila/udini itaondoka, maana nafasi zote muhimu ndani ya chama zitakamatwa na watu wanaostahili kwa merits na si vinginevyo.
   
 4. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kila linaloshauriwa ni la kucopy toka chama tawala! kweli wamethubutu, wameweza!
   
 5. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Point less!!!
   
 6. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Ibrah,
  Asante kwa ushauri. Tutambue kuwa uwe mzuri au mbaya umetumia muda wako na akili zake. Umetumia haki yako ya ushauri. Kama desturi yetu utafanyiwa kazi, na ushauri si deni. Asante sana
   
 7. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #7
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Acha Ushabiki mbona inaonekana unaweza kufikiri zaidi ya hapo, tumia akili yako hata robo, utaheshimika mkuu...
   
 8. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #8
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,482
  Likes Received: 5,556
  Trophy Points: 280
  Asante Rais wangu wa moyoni kwa kujali maoni yetu.Tuntemeke ni mtoto wa Marehemu Tuntemeke Sanga,huyu dogo si wa kutengwa,nakuomba Mh Dr Slaa umuite personally umpe ushauri wa namna ya ku handle mambo ya siasa.ni kijana mdogo na mpiganaji anaehitaji ukombozi wa fikra! Sasa hivi anasema yupo Arumeru kwa gharama zake! Hebu mkuu wangu muite kijana umpe busara zako na wanacdm wasimtenge kama msaliti hasa John Mrema anayehisi kachafuliwa.
   
 9. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #9
  Feb 29, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  napita wajamii!
   
 10. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #10
  Feb 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vyema kuapriciate ushauri,nimependa hii kwamba ushauri si deni
   
 11. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #11
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wazo la baadaye sana baada ya ukombozi.
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Ni mawazo yanayojenga!!!!!
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Shukrani. Nimetumia akili yote mkuu. Huenda huo ndio mwisho wangu wa kufikiri. Nadhani nimepata haki yangu
   
 14. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  ushauri mzuri nazani raisi wetu kakujibu vyema.
   
 15. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 160
  Mimi Ibrah, kama mshabiki na
  mwenye kuiwazia mema
  CHADEMA na Tanzania,...Na mimi nikushauri Ibrah,ebu piga hatua moja mbele,toka ktk kuwa mshabiki wa Chadema,jiunge kikamilifu ktk harakati za chama za kuikomboa hii nchi.Ninavyo-jua mimi washabiki ni watu wa maneno mengi vitendo sifuri,ni waudhuriaji wazuri kwenye mikutano lakin hawajiandikisha kupiga kura...
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Paka Jimmy unajibu vizuri sana hapa

  lakini ww ni mmoja wa wanachama wa chadema na member humu ambaye post zako nyingi zimejaa kinyaa na majibu ya hovyo hayana hoja wala kichwa

  wengi wana CDM wako kishabiki zaidi na huwa nasema kuwavuta wale wa upande ule , jenga hoja, sema kwa hekima na wanabadilika, hii si yanga na simba thing

  CCM wengi wanaweza wakawa converted to chadema ila kuwe na hekima na nguvu ya hoja, matusi , kejeli n.k humfanya binadamu kuwa na kiburi

  kwa hiyo ubadilike mzee
   
 17. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #17
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Mzee Slaa majibu kama haya kwa wana JF-CDM ni nadra sana kuyatoa

  wengi wenu hata ww nyakati fulani mmekuwa mkijibu kejeli na kujilinda linda

  Please let it be like this and encourage others to do so
   
Loading...