Ushauri: Wanawake jengeni utamaduni wa kutembea na japo kanga moja kwenye pochi zenu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri: Wanawake jengeni utamaduni wa kutembea na japo kanga moja kwenye pochi zenu.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mkeshaji, Jan 10, 2012.

 1. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni ushauri tu kwa akina dada:
  Leo nikiwa njiani kuelekea kwenye deiwaka kulitokea jambo ambalo kidogo ni la kusikitisha.
  Akiwa kwenye daladala ambayo ilijaza kupita kiasi dada mmoja alianguka ghafla ndani ya gari hiyo. Wakati huo daladala hiyo ilikuwa imesimama kwenye foleni. Basi konda pamoja na abiria wengine waliokuwemo humo wakamsaidia kumtoa dada huyo na kumlaza pembezoni mwa barabara.

  Kimavazi, dada yule alikuwa amevaa kitopu kifupi kinachobana sana pamoja na kimini.
  Kutokana na tukio lenyewe lilivyotokea wakati wa kumbeba kwa kweli ilikuwa kama vile yuko mtupu (try to imagine). Basi watu waliokuwa karibu ilibidi kila mtu aanze kusema lake (hasa kuhusiana na mavazi). Wengi walilaumu kuwa akina dada wa siku hizi wanavaa nguo zinazowashika mwili lakini kwa nini wanashindwa kuweka japo kaupande kamoja ka kanga ili kiwasetiri pindi watakapopata emergence. Walikuwepo pia akina mama ambao nao walishiriki katika lawama hizo dhidi ya "mabinti" zao.

  Wakati huo mimi pia nilikuwa karibu na tukio. Dada yule ilikuwa kama vile hapumui. Basi nikajaribu kuwashauri wale watu ambao walikuwa wamejikita zaidi katika kulaumu kwamba kwa wakati huo lawama haikuwa kitu cha muhimu. Badala yake tujikite katika kuhakikisha kuwa tunaokoa maisha ya binti yule huku tukihakikisha kuwa tunamsetiri utu wake. Kitu cha kwanza nilimuomba mama mmoja ambaye alikuwa amejifunga kanga atuazime kanga moja tumsetiri. Mama alikubali.

  Wakati huo dada mmoja alikuwa akimpepea kwa kitambaa chepesi. Mimi niligundua kuwa hiyo isingesaidia kitu kama nitakavyoeleza hapa chini.
  Kwa kuwa dada yule ali-faint katika gari ambayo ilikuwa imejaa pomoni ni dhahiri kuwa alikosa oxygen ya kutosha hivyo moyo wake kushindwa kufanya kazi sawasawa na kupelekea ubongo kukosa oxygen ya kutosha. Kitabibu, inasadikika kuwa ubongo ukikosa oxygen ya kutosha mtu anaweza akapoteza maisha ndani ya dakika 5.

  Kwa kuwa mimi nina idea ya huduma ya kwanza nikaona si vibaya nikampatia yule dada huduma ya kwanza kwa kadri ninavyoweza. Kitu cha kwanza nilijitambulisha kwa watu ambao sasa walikuwa wamejaa kumzunguka yule dada bila msaada wowote na kuwaeleza kuwa ninayo mafunzo ya huduma ya kwanza.
  Baada ya hapo nikamfanyia kitu kinaitwa Cardio-Pulmonary Rescusitation (CPR) kwa ajili ya kuustua moyo wake na kumwongezea oxygen. Wakati huo nilimuomba jamaa mmoja aende kutoa taarifa kwa Traffic Police ambao walikuwa upande wa pili wa barabara wakiangalia usalama wa magari. Nilimpatia jamaa mwingine achukue simu ya yule dada na ajaribu ku-search namba za jamaa zake wa karibu na kuwataarifu juu ya mkasa huo.
  Mimi niliendelea na CPR hadi nilipohakikisha kuwa yule dada amepata nafuu nikamweka kwenye "Recovery Position" halafu nikamkabidhisha kwa akina mama wawili ambao walikuwepo eneo la tukio na walikuwa wakitoa msaada wa hapa na pale then na mimi nikawahi kwenye "kijiwe changu cha kuponda kokoto".

  Nikiwa njiani nilijaribu kutafakari mambo mengi sana kichwani lakini kikubwa ambacho niliona si vibaya nikawashauri akina dada:
  Jamani, pamoja na kupiga mapigo makali ya viwalo si vibaya kwenye hayo mapochi yenu mkaweka japo kaupande ka kanga. Huwezi jua njiani!

  Note: Kisa hiki kimetokea kweli leo asubuhi kama nilivyokielezea.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Nakupongeza sana kwa msaada uliotoa...ni kisa cha kusisimua.

  Naamini hujaomba au kusearch contact za huyo dada!(joke)

  Wadada wajifunze kuwa pamoja na ujana na fasheni zinazotamba, lakini UANAMKE upo palepale, na unahitaji kuwa na staha na yahadhari zake
  .
   
 3. S

  SUWI JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ahsante kwa story/taarifa.. pia kwa ushauri/// pia hongera kwa kumpatia dada huduma ya kwanza maana watu wakiona hata ajali wanajazana kushangaa huku mgonjwa akiendelea kuwa katika hali mbaya.. Hongera sana.. ubarikiwe
   
 4. u

  utantambua JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Well done Mkeshaji, umeplay your part, ushauri kwa wenye sikio la kusikia watauchukua.
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mwanamke wa kileo,wala c ajabu kuikosa khanga hata anapoish
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Hongera, kama mdau mmojawapo wa huduma ya kwanza, umefanya kazi vyema na umewakilisha haswaa. Nikutahadharishe tu juu ya hao wamama waliokuwa wanachonga, je walipekua mkoba wa huyo mdada na wakakuta hakuna khanga? Manake hakujua angepoteza fahamu, angejifunga khanga yake vema. Japo mkiki wa kuzimia na kubebwa mzobe mzobe hata kama ni dera watazamaji wangufaudu japo chabo ya mapaja.
  Asante kwa utu wako na uzalendo.
   
 7. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Duh!Hili ni somo kwa wale wanaoshabikia mavazi mafupi!
   
 8. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #8
  Jan 10, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Kwani mwanaume akizimia inakuaje hzo ni ajali tu na yaweza mtokea hata mwanaume
  anzeni nyie kutembea na kanga
  upuuuzi tu huo
   
 9. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #9
  Jan 10, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  niliacha siku nyingii sana kutumia khanga!!
   
 10. mkonomtupu

  mkonomtupu JF-Expert Member

  #10
  Jan 10, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hongera mkuu. Kwangu imekuwa very touching story kwangu kwa kweli hongera. Wenye kusikia watafuata ushauri wako maridhawa
   
 11. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  sawa tumesikia....
   
 12. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #12
  Jan 10, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  King'asti umenichekesha sana hapo kwenye red!
   
 13. Yummy

  Yummy JF-Expert Member

  #13
  Jan 10, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,801
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Lol....hii kali!!
   
 14. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #14
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kweli mke mweza, unaeza kuta mdada wa watu alikuwa na kanga ndani ya pochi yake ila vile binadamu tumezoea kusema ndio hivyo tena. Isijekuwa hata hao waliokuwa wanakazana kumzunguka sio kwa kumsaidia but ni ili waendelee kuokoteza maneno ya kusema...watu wengine bana hovyo kabisa mtu anapata tatizo badala ya kumsaidia kwanza wanaanza Ooh umeona nguo aliyovaa? Inahuu? Ajali ni ajali haijalishi umevaa nguo gani unaeza kuanguka umejipigilia kanga mbili na ukamwaga radhi pia...

  Pole kwa mdada na hongera kwa mleta mada kwa msaada ulioutoa. Wenye masikio wataufuata ushauri wako.
   
 15. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #15
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Aaahhhh, sijaomba mkuu!
  Kwanza wanoko walikuwa kibao...lol!
   
 16. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #16
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waambie wasikie, maana mie huwa nikiwaambia hata hapa ofisini kwangu tembeeni na khanga kwenye handbag zenu wananiambia mie mshamba. eti " akipata tatizo atanunua hapo atakapokuwa" nachoka mie.
   
 17. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #17
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asante.
  Wazo kuu ni kuwa tuwe tunajiandaa kwa lolote, walau kwa kubashiri kabla.
   
 18. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #18
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kana kwamba hayo maduka yapo hadi kwenye magari, na kwamba anajua aina ya matatizo yatakayomkuta.
   
 19. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #19
  Jan 10, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hongera sana mkuu,
  Nnimuhimu kuwa na kanga kwenye pochi hata km si kwa ajili ikusaidie ukianguka,
  Yapo mengi yanaweza kutokea na ikasaidia,
  Hata hiyo kwan ina uzito gani?
  Hapa na malezi yanakua applicable.
   
 20. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #20
  Jan 10, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ahsante mkuu na hongera kwa kweli toka mdogo mama yangu alinipiga marufuku kutoka nyumbani bila khanga au mtandio,mwanamke yoyote mi nijuavyo ni lazima abebe, bila kujali amevaaje,
   
Loading...