Ushauri: Wakulima, Wafanyakazi na Wafanyabiashara tuungane tusifurahie matatizo yanayompata mmoja wetu

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,148
33,302
Ewe mkulima usifurahie mfanyakazi kutoongezwa mshahara,kwani mtumishi wa sekta yeyote ni mteja wa mazao yako,asipoongezwa hutauza mazao yako kikamilifu.

Ewe mfanyabiashara,usifurahi kwa mtumishi kutoongezwa mshahara ,asipoongezwa ,hatanunua bidhaa dukani mwako ,asiponunua ,hutapata pesa za kutosha kuendesha maisha yako,naye mzalishaji kiwandani hatazalisha bidhaa kwa wingi.

Nawe mtumishi usifurahie mkulima asipolipwa malipo yake kikamilifu,asipolipwa hatalima mazao zaidi,hivyo kupelekea bidhaa kupungua masokoni na kufanya bei kupanda.

Pia ewe mfanyakazi usifurahie mfanyabiashara kubugudhiwa,akibugudhiwa huacha kufanya biashara,huondoka ,hivyo husababisha bidhaa kuadimika,zikiwa chache bidhaa,bei hupanda,matokeo yake maisha huwa magumu sio kwa mfanyakazi tu,bali pia kwa mkulima na mfanyabiashara.

Madhara yake ni nini?
Madhara yake ni mifarakano,
Tuungane wafanyakazi,wakulima na wafanyabiashara kudai haki zetu,tusifurahie matatizo ya mmoja wetu.

Wenye akili wamenielewa.
 
Haki hiyo wanaidai vipi wakati wabunge walle wamegoma kumtetea mfanyakazi na mkulima?
 
cUmeongea kweli sana...tatizo hakuna nchi yenye woga km Tanzania ..hebu ona hata Sudan kanchi kadogo wametupita ..wanawake wamefanya yao Sudan..mgusr mwanamke wa kitz atakuambia yy ana watoto anaogopa vita😏😏😏
 
Back
Top Bottom