Ushauri wako: Ungetumia namna gani kumwambia mpenzi wako kuwa umegundulika una HIV? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wako: Ungetumia namna gani kumwambia mpenzi wako kuwa umegundulika una HIV?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nasema, Oct 31, 2012.

 1. Nasema

  Nasema JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wadau wa MMU naomba ushauri wenu.Kuna dada ana miaka 23, ana mpenzi ambaye alianza naye uhusiano miezi minne iliyopita. Kabla ya hapo alikuwa na uhusiano na mvulana mwingine ambao ulivunjika, akakaa mwaka mmoja na nusu ndipo akaanza uhusiano na huyu mpenzi wa sasa.Hivi karibuni alienda kupima akagundulika ana HIV. Kiukweli hajui kama ameambukizwa na mpenzi wa kwanza au huyu wa sasa. Anapenda kumfahamisha mpenzi wake kuhusu status yake ili ikiwezekana waanze kufuata ushauri na dawa za kupunguza makali ya ugonjwa.Naomba ushauri wenu atumie mbinu gani kumwambia mpenzi wake bila kuharibu uhusiano wao?Tafadhali naomba ushauri wa kusaidia, sio kashfa, kushushua, nk.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Asiseme chochot
  amwambie tu hataweza ku sex nae bila kwenda kupata ushauri nasaha
  na kupima VVU
  ajifanye na yeye hajui status yake

  waende wote akapate 'breaking news' huko huko
   
 3. Billie

  Billie JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 13, 2011
  Messages: 5,325
  Likes Received: 2,313
  Trophy Points: 280
  Aongeze stori za ukimwi nyingi kila akutanapo na mpenzi wake.
   
 4. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,418
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hasiumize Kichwa Amwambie Tu, Kwani Mpenzi Wake Nae Anatafuta Mbinu Ya Kumwambia!!
   
 5. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,978
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kha..mbona kavaa miwaya ata very young age!! ama kweli utamu huu utatumaliza. ah yeye awe mbogo kwa kumlaumu jamaa kuwa wewe umeniambukiza ngoma...yaani awe mkali kweli kweli.
   
 6. m

  movichboy JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 212
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 45
  Ku diclose status ya HIV/AIDS ni process ambayo ki msingi inahitaji utaalamu ili usije waumiza wengine kisaikolojia. Unajua tatizo kubwa tulilonalo hasa kwa hawa watoa huduma za afya ni kutofanya kazi vizuri kwa kufuata taaluma hasa ya ushauri nasaha na upimaji wa VIRUSI VYA UKIMWI.

  Ki msingi ni ngumu huyu dada kumwambia mwenzie kwamba yeye tayari ana maambukizi, inawezekana kweli lengo lake likawa ni kumlinda mwenzie aidha asipate maambukizi kwan kuna uwezekano mkubwa tu kitaalam wewe kuwa na VVU na usiweze kumuambukiza mwenzako hata kama hamtumii KINGA kwan maambukizi kutokea mara tu baada ya kuwa na blood contact kati ya mwenye VVU na siye na VVU.

  Cha msingi hapa ni kumshauri yeye na mwenzie waende kupatiwa ushauri nasaha wa pamoja (Group counselling) wenye lengo la kupima VVU ili kila mmoja aelewe status ya mwenzie kwa kupitia mtaalam ambapo kutakuwa pia na room ya ushauri nasaa zaidi kama wote wataonekana wana maambukizi au mmoja na kujua jinsi ya kuishi na VVU. From there utaungaunganishwa na huduma zingine za UKIMWI kama kuanza CTC clinics endapo kinga zako (DC4) zintakuwa zimeshuka mpaka (350-200) ili kuanza kutumia dawa za kufubaza VVU.
   
 7. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,317
  Likes Received: 2,603
  Trophy Points: 280
  ni vyema wakakaa chini na kuongea huwezi jua labda huyo aliyenaye ndiye aliyemwambukiza hiyo makitu na alikuwa akiogopa kusema....
  kitendo cha kukaa kimya hakitawsaidia wote wawili...
   
 8. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Ningekuwa mimi, ningemwambia mzee, nasikia ARV's ni tamu sana na ni nzuri kwetu, hivi twaweza zipata wapi, ili tuzitumie kuimarisha penzi letu?? Maana naona umepungukiwa sana na nguvu za kiumeni family
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,737
  Trophy Points: 280
  Nadhani kama anaweza kumshawishi wakapime virus japo yeye ana jijua alaf wata share majibu wakikubaliana!

  Na kwa ushauri watakao pewa kabla na baada ya majibu itakuwa njia rahisi sana kuliko kumwambia tu kwa mdomo!

  Hapo ni kutumia ushawishi wakapime afya!

   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  The Boss nakubaliana sana na ushauri wako
  Amweleze may be kuwa anataka wafanya may be mipango ya ndoa na ili kuwa on safe side wakapime HIV status zao na ikajulikane huko huko kuliko kumwambia wazi itamuumiza sana
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. ram

  ram JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,194
  Likes Received: 898
  Trophy Points: 280
  Ammwambie mpenzi wake waende Angaza/hospital kupima na kupewa ushauri nasaha, majibu yakitoka maadamu bidada anajijua, kama yeye mkaka kaathirika au hajaathirika ataamua mwenyewe kama waendelee kuwa wapenzi au la! Yeye bidada atakuwa keshautua mzigo
   
 12. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Amwambie tu kwani siku hizi kunifichana.
   
 13. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,852
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  ushauri wa The Boss ni mzuri, lakini what if mkaka akawa hajaathirika baada ya kupima? je anaweza kuendeleza mahusiano, je anaweza kutomnyanyapaa mpenzi wapi. hilo pia anapaswa kujiuliza kabla hawajaamua kwenda kupima. . .
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Nasema

  Nasema JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nawashukuru sana kwa ushauri mzuri. Nimemshauri bidada amshawishi kijana waende kupima.
   
 15. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  mh haya mambo mazito atii
   
 16. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #16
  Nov 2, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Kabla ya kuendelea unaomba tukusaidie umwambie mwenzako ama uko kwenye research wengine wale sie tuotoe macho?
   
 17. mgeni10

  mgeni10 JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 1,112
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Siku zote kweli uitakuweka huru

  Amwambie tu ukweli kwamba ameenda kupima na majibu ndio hayo, hivyo amwambie huyo mpenzi wake nae akapime ili kama ameambukizwa hatua zichukuliwe. ie afuate ushauri atakaopewa
   
Loading...