ram
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 9,252
- 8,340
Mwingine yuko kule MMU, yeye mke wake ana uvimbe uliosababishwa na sindano/vidonge vya majira, wamezunguka weeee kwa madaktari, hadi sasa option ni kutoa kizazi kwani hawezi kuzaa tena, nawaonea huruma hawa wadada jamani. Lakini kwa uelewa wangu mdogo fibroid, huwa zinawapata wamama wenye umri wa kati miaka 34 - 40 waliochelewa kuzaa na huwa zinatolewa, sasa huyu mdada sijui ni vipi, lol!
Kamsongole,
Pole na changamoto.
Katika swali/shida yako kuna mambo mawili kama nimekuelewa: 1. Kutibia fibroid 2. Kusave ndoa kwa kupata mtoto.
1. Kwavile daktari alishakufanyia tathmini na kuona kuwa ni lazima utolewe kizazi, inakuwa vigumu kupitia mtandao kutoa tathmini tofauti. Hii inaashiria kuwa umefanyiwa ultrasound na uvime umeonekana kuwa aidha ni mkubwa sana au upo mahali ambapo hauweyi kutolewa na kuacha kizazi au pengine jinsi unavyoonekana umempa hofu daktari kuwa uvimbe huo una hatari ya kuwa kansa. Kwahiyo ushauri ninaokupa kwenye hili, hakikisha daktari anayekushauri ni gynecologist mzoefu na itakuwa vizuri kama gynecologist huyo anakufanyia ultrosound yeye mwenyewe na sio kusoma repost ya ultrasound iliyofanywa na mtu mwingine.
2. Kusave ndoa. Inagwa hujaandika hapa, lakini napata hisia kuwa kilichosababisha kugunduliwa kwa uvimbe ni wewe kwenda hospitali kwa tatizo la kukosa mtoto kwa miaka minne. Kwa vile imeshauriwa utoe kizazi, uwezekano wa wewe mwenyewe kubeba mimba hautakuwepo ukishatoa kizazi, lakini hii haimaanishi kuwa hauna uwezo wa kupata mtoto. Maendeleo ya sayansi ya kitabibu yamefikia hatua ya kuweza kuchukua yai lako na mbegu ya mmeo na kuziunganisha kutengeneza mtoto atakayekulia kwenye tumbo la mwanamke mwingine. Sijajua upatikanaji wa huduma ya namna hii nchini kwetu ukoje na unafuata sheria zipi, lakini iwapo utaamua kutoa kizazi basi ulizia uwezekano huu. Natambua pia kuwa gharama yake ni kubwa.
Upo pia uwezekano wa kuadopt mtoto. Mkiandaliwa vizuri kisaikolojia mnaweza kuendelea kuishi kwa furaha na mtoto wenu mliyemuadopt.
Kuhusu kutoa mimba kama alivyosema mdau hapo juu, chukulia kama changamsha baraza tu. Naamini hata yeye hakuwa serious, alikuwa anatania...