Ushauri wako fundi kwa ujenzi wa nyumba bila linta

Lundavi

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
327
320
Habari! Kama ilivyo mada tajwa hapo juu.

Kama mjuavyo ujenzi ni gharama sana hasa ukifuata kanuni zote za ujenzi. Binafsi nataka kujenga lakini katika hesabu zangu za kusimamisha boma, nimekutana na gharama ya ufungaji wa linta hasa ukizingatia bei ya nondo, Kokoto na cement.

Kutokana na bajeti yangu kuwa finyu nafikiria kuachana na linta ila niwe na matumizi ya cementi sehemu kubwa ya boma la nyumba yangu. Tafadhali naomba uzoefu katika hili najua kuna waliotumia hii mbinu.

Katika majibu yako ningeomba nifahamishwe juu ya;
i. Urefu wa kimo cha ukuta kiwe na kipimo kipi?
ii. Madirisha yawe na kipimo cha feet ngapi?(hasa kimo).
iii. Maeneo maalum ya kuta ya kutumia cement badala ya tope.

Nakaribisha mawazo mengine pia ambayo yatasaidia. Lengo ni kupunguza gharama ya linta ila nyumba yangu iwe angalau imara.
Natanguliza shukrani.
 
Safi kwa kuhitaji ushauri. Kwanza eleza matope kivipi badala ya cement?, Linter ni lazima hasa maeneo ya mlango na dirisha upo uwezekano wa kuweka upande mmoja mmoja, ni wapi au ni mkoa upi?.
 
Safi kwa kuhitaji ushauri. Kwanza eleza matope kivipi badala ya cement?, Linter ni lazima hasa maeneo ya mlango na dirisha upo uwezekano wa kuweka upande mmoja mmoja, ni wapi au ni mkoa upi?.
Ni matope, nikimaanisha udongo. Nipo Iringa
 
Ni matope, nikimaanisha udongo. Nipo Iringa
Ok, ujenzi wako inatakiwa upate coze 9 kuanzia juu ya msingi, upana wa dirisha inategemea na matakwa yako Kama ni ft nne au 5, urefu weka ft5 itapendeza, kuhusu linter weka maeneo yatakayo pita mlango na madirisha Ila mbele ya nyumba linter weka kote ili nyumba iwe na nguvu ya kubebe coze 3 za juu ya linter Jambo lingine usichanganye cement sehemu nyingine uweke udongo si sawa, tumia cement sehemu zote.
 
Shukrani
 
Zungusha ring beam Kuta za nje tuu afu Kuta za ndani jengea cement zote kwa sababu kiujumla mifuko 9 ya saruji inamaliza nyumba ya vyumba 3 kujengea na hiyo zege ya nje.

Mondo za ring ya nje unaweka za 8mm au 10 mm
 
Back
Top Bottom