Kutokana na namna ambavyo imedhihirika kwamba sasa Spika hawezi kuwa na uhuru wa kuruhusu mijadala yenye afya kwa watanzania ndani ya bunge kwa hofu ya "kushughulikiwa" na chama (kwa vyama vyote) sasa ni muda muafaka kwa wabunge hasa wa CCM walio wengi bungeni kumpigia kura ya Ndiyo mgombea wa kiti cha Spika asiye na chama.
Wakiweza hili litakuwa na faida kubwa sana kwa taifa pia kwa wabunge wenyewe maana nao pia watakuwa huru kuishauri na kuisimamia serikali.
Wito wangu kwa wabunge wote wanaopigania uhuru wa mhimili huu wa bunge na wale wenye uwezo wa kuliongoza bunge ambao si wabunge njia pekee iliyobaki ni hiyo, chonde chonde tuitumie nafasi hii vizuri tutakuwa tumepiga hatua nzuri kuelekea kupata katiba mpya.