USHAURI: Wabunge wa CHADEMA wanaweza nunua mitambo ya umeme

Sijadandia bali nauliza swali la msingi kwanini mpewe madaraka wakati hamsemi mtawafanyia nini watanzania?
Loo, yaani kuna watu hawajasikia Chadema watafanya nini tofauti na CCM ! Kweli CCM imewapofusha na kuwaziba masikio wengi.
Unajua Mag3 ushabiki pembeni watu wanaoisupport Chadema ni watu wasio na chama chochote je nikuulize ikija kutokea CCM wakabadilika mmeshajiandaa?
Duh, yaani bado kuna watu wanaitegemea CCM kubadilika ! Kweli CCM imewapumbaza na kuwalemaza wengi, pole Mdondoaji.
 
Thread zingine sijui huwa zinaanzishwa na watu wakiwa usingizini!! Yaani hiyo milioni 90 times 40 something inaweza kununua mitambo ya kuzalisha umeme? Kwa nini Meremeta, Kagoda, Deep Green, Dowans wasirudishe pesa yetu tutumie kwa kadri tupangavyo? Kumbuka 50% ya hiyo milioni 90 ni mkopo na nyingine ni grants. Wezi wakubwa waachiwe pesa waliyoiba eti wabunge wa CHADEMA wanunue mitambo kwa pesa yao ya mikopo!! By the way, hiyo mitambo haihitaji kununuliwa, tunatakiwa kutumia sheria zetu halali kutaifisha hiyo mitambo ili iwatumikie wananchi na si kundi dogo.
 
Kwa nini mleta mada asiwaombe cdm wamgang'anie jk tugawe mshahara wake,na mawaziri wapate mshahara wa mbunge tu,na wale walio wabunge hapo hapo ni wakuu wa mikoa,apo apo ni wanakamati wa bunge,apo apo ni wajumbe wa chama,apo apo ni member wa district council. Posho zote hizo wangeweza kununua mitambo unayoitaka wewe. Mi binafsi sishauri ivo mana ni kazi ya serikali,labda serikali itangaze kushindwa ndo isaidiwe,si kwa kiburi walichonacho watawala alaf wananchi ndo waanze iyo kazi.
 
Lyatonga Mrema alitaka kuleta umeme wa bei poa toka USA, kumbuka jinsi CCM walivyozima mpango huo, licha wawekezaji toka Marekani walishafanya utafiti wao na kukubali kuwekeza.

Kumbuka vitimbi alivyofanyiwa Slaa wakati ameanzisha mradi wa maji kwa wananchi wa jimbo la Mbulu.

Serikali ya ccm sifa yake ni kuona Watanzania wa wanaishi kwenye maisha ya kifukara maisha yao yote.

Nimekusoma hot-water; Mi nafanyakazi kwenye moja ya mashirika ya umma hapa nchini. Kama mhandisi kitaaluma, najua TANESCO inaweza kufanya vizuri na kuwahudumia wananchi kama hakuna ufisadi. Wala halitahitaji vi-mkopo vya wabunge wa CDM kuingiza umeme kwenye grid. Ukweli ni kwamba haya mashirika ya umma yanahujumiwa sana na serikali iliyoko madarakani. Labda niweke mifano michache tu:
1. Taasisi ya Teknolojia DSM (DIT) inatengeneza taa za barabarani kwa gharama nafuu (about 10M) na zenye ubora wa hali ya juu, lkn serikali ilikataa kuzinunua na badala yake wakaagiza nje kwa 45,000USD (about 60M).
2. CARMATEC - Arusha wanatengeneza matrekta mazuri sana ya gharama nafuu lkn serikali inaagiza Power Tiller za kichina ambazo kiukweli zimeshindwa kufanya kazi kwa mazingira yetu. Pia wana mradi wa Biogas ambao ungefaa kwa ajili ya "Rural Electrification" na kuwezesha kuendesha mitambo ya "irrigation" lkn wamejenga mtambo huo Bagamoyo kwa JK tu halafu basi.

Pia, kuna mzungu wa Kamanga ferry alitaka kuweka barabara ya lami kutoka Sengerema - Kamanga lkn serikali ilimzuia kwa wivu kwamba ferry ya serikali ya Busisi ingekosa mapato. Na, niliwahi kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa mh. Ndesamburo (mbunge wa Moshi mjini - CDM) alinunua Ambulance kwa ajili ya kuhudumia wananchi wake serikali ikakataa kuitumia.

Hivyo, wabunge wa CDM siyo rahisi kujihusisha na miradi ambayo serikali ya CCM imeshindwa kufanya kwa kuendekeza ufisadi. Hata wakichanga na kuchangisha umma je, watawalazimisha TANESCO waingize umeme huo kwenye grid? Mi naona CCM waachie ngazi kwa sababu wameshindwa kuondoa kero za wananchi, CDM wachukue madaraka ili waweze ku-implement sera zao kwa uhuru.
 
Loo, yaani kuna watu hawajasikia Chadema watafanya nini tofauti na CCM ! Kweli CCM imewapofusha na kuwaziba masikio wengi.

Duh, yaani bado kuna watu wanaitegemea CCM kubadilika ! Kweli CCM imewapumbaza na kuwalemaza wengi, pole Mdondoaji.
Kuuliza kwani kupofuka Mag3 kweli ushabiki mwengine kwa taarifa yako watanzania wengi hawana vyama na wanawaunga mkono yeyote anayeweza kuwatoa ktk mkono Wa hali Ngumu ya maisha
 
Gsana,

Tuanze kwanza kugawana mshahara wa Dr Slaa kabla hamjashauri kugawana mshahara Wa rais
 
Back
Top Bottom