Ushauri wa Wazi kwa Wizara ya Afya hususan mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF)

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,462
2,855
Ndugu zangu,

Natambua kuwa serikali na idara zake nyingi sio zote ni "wavivu" sana kujibu malalamiko, ushauri au mapendekezo. Ila tunashauri kwa mema hata yakitokea kwenye mitandao ya kijamii sio "dhambi" kutafanyia kazi kwa kuwa wafaidika ni wajamii wa Kitanzania.

Ni vema NHIF ikarasimisha mfumo wa kuwahudumia wateja wake kwa namba tu ya kitambulisho cha mwanachama akifika katika vituo vya afya/hospitali kupata huduma.

Kwa dhana ileile ya namba ya kitambulisho ya Uraia cha NIDA, au TIN TRA zote zipo kwenye mfumo. Ukifika TRA, au ukipata access ya mtandao wa kusajili kampuni BRELA, kupata passport... maadam namba ya utambulisho wa Milipakodi au namba ya NIDA iko sawa huduma unapata.

Kwa muktadha huo, huo, kwa wanachama wa NHIF kwa kuwa ID zao ziko kwenye mtandao na kwa kuwa mtu anaweza kuugua saa yoyote pengine akiwa hana ID yake ya NHIF mkononi, kama ikitokea anaikumbuka namba ya ID yake, basi akifika kwenye madawati ya huduma za bima ya AFYA ya Taifa ni vema akapata huduma.

Ni ushauri tu wa DG wa NHIF na wakubwa wa Wizarani Mhe. Ummy Mwalimu na Mhe. Dr. Ndungulile, ni busara mkawa pro-active kuli-taasisisha hili ili kuendana sambamba na matumizi ya technology kwenye karne hii ya 21 na pia kuunga mkono matumizi ya kimtandao katika ku-facilitate huduma za afya kwa wanachama wa NHIF.

Mkifanya hivi, mtaongeza chances zenu kiutendaji na sifa zitazidi kumwendea raia namba moja ambae kiuhalisia hapendi urasimu.
 
Back
Top Bottom