Ushauri wa wazi kwa Rais na Waziri wa Utumishi na Utawala Bora kuhusu utekelezaji wa stahiki za watumishi

EZJ

Member
Jun 25, 2021
49
48
Kwanza niwapongezeni nyote kwa kazi kubwa sana na ngumu mnayoifanya ya kulitumikia Taifa hili.Pili niwapongeze kwa juhudi mbalimbali mnazozifanya za kuhakikisha vilio vya muda mrefu vya watumishi wa serikali vinafanyiwa kazi.Sasa ningependa niende moja kwa moja kwa ushauri wangu:

Kwako Mh Rais : Kwa mamlaka uliyonayo naamini kabisa unaweza ukafuatilia na ukabaini watumishi ambao wametumikia serikali na nchi kwa ujumla kwa muda mrefu ,lakini bado wapo chini mno katika ngazi zao za mishahara,na maanisha walistahili kupandishwa kwa madaraja ya mserereko ili waendane na hali halisi ya gharama za maisha zilivyo.Najua wewe ni Mama,na kwa hakika hili ukimwagiza Waziri wa Utumishi alisimamie,ukweli utaufahamu.Na haki za watumishi wa serikali unayoiongoza hazitapotea.

Kwako Mh Waziri wa Utumishi na utawala bora: Kwanza nikupongeze tena kwa kazi nzuri unazozifanya za kuendelea kusimamia utekelezwaji wa msingi wa haki za watumishi hapa nchini.Sasa katika hili,kuna zoezi ulilolisema hapa majuzi ukiwa Mkoani Kigoma.Kuwa kuanzia Jumatatu ya tarehe 20/12/2021 serikali italipa malimbikizo kwa wafanyakazi 18,000 nchi nzima yenye thamani ya 30 bilion.Kwenye hili ndipo nilipotaka kutoa ushauri wangu kuwa,kama kweli mmepanga hivyo basi wewe kama Waziri mwenye dhamana usimame kidete kuhakikisha stahiki hizo zinalipwa kwa wote wenye kustahili.Nasema hivi kwa sababu,mimi ni mmoja wapo wa wafanyakazi waliopandishwa daraja mwezi wa Tano,2019 wilaya ya Hai, Kilimanjaro.Niliopanda nao,baadhi wakati wa likizo ya korona mwaka jana wakalipwa malimbikizo yao.Wengine mshahara wa mwezi huu wa kumi na mbili tayari na wao wamekuta malimbikizo yao ,mimi Mh sijakuta malimbikizo yangu.Hali hii wakati mwingine inakatisha sana tamaa kiukweli.Lakini panapokuwa na usawa angalau amani inatawala kote.Miaka yote mitatu kweli wanashindwa vipi kuhakiki taarifa za watumishi wa chini wa nchi hii na kuhakikisha tunapata haki zetu???Ni imani yangu kwamba ushauri huu utaenda kiufanyia kazi,na kama wanaendelea kuweka hayo malimbikizo kuanzia hiyo jumatatu iliyopita kama ulivyosema,basi watuwekee sote.Maana hakuna asie na uhitaji wa hela.Hususani katika kipindi hiki ambacho kiukweli thamani ya bidhaa na huduma mbalimbali zimepanda sana.Nina imani na wewe Mh Waziri,kijana mwenzetu na mchapakazi pia.Ni imani yangu kuwa katika hili utalisimamia kidete.Ili sote 18,000 ndani ya siku hizi zinazoendelea za mwezi huu sote tuwe tumelipwa stahiki zetu ambazo wengine tumezisubiri kwa takribani miaka mitatu Sasa.

KWA PAMOJA NIWATAKIENI NYOTE MH RAIS NA MH WAZIRI WA UTUMISHI NA UTAWALA BORA UTEKELEZAJI MWEMA WA MAJUKUMU YENU.NA NI IMANI YANGU KWAMBA USHAURI WANGU MTAUZINGATIA,ILI KWA PAMOJA TUENDELEE KUITUMIKIA NCHI YETU.

ALUTA,CONTINUA!
 
Mhe Waziri wa Utumishi,nakuomba sana ufuatilie kwa ukaribu zoezi hili la ulipaji wa malimbikizo kwa watumishi.Wasije wakawa wanakuletea tu takwimu za waliolipwa.Vilio vya ambao hatujalipwa ni vingi sana.Hivyo zoezi hili zuri lisije likatiwa dosari!
 
Kabisa alafu ni uku tu ivi sector zingine hawalipwi kama elimu
Mkuu wakati mwingine kunakuwa na mkanganyiko sana.Na mara nyingi unasababishwa na watendaji waliopo kwenye halmashauri kuchelewa kupeleka taarifa au uzembe unaofanana na huo.Nasema hivi kwa sababu taarifa za watumishi wanaoenda likizo za malipo na zisizo za malipo huwa zinatolewa mapema sana.Kwa ajili pia ya kuandaa fedha za likizo kwa wanaostahili.Hivyo pesa ya likizo inapaswa Mtumishi alipwe kabla ya kwenda likizo,na sio baada.Maana sasa ukija kumlipa kama madai baadae inakuwa inathamani gani?Na kwingine unakuta wanalipwa hivyo kwa wakati.Wengine ndio mnaambiwa mtadai.Kwa sababu tu ya uzembe au makusudi tu fulani ya watumishi wachache wasio waaminifu katika halmashauri zetu.inatia hasira sana
 
Back
Top Bottom