Ushauri wa Serikali ya Magufuli jiji la Dar

MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,947
1,500
Serikali ya JPM naamini inaweza na nimeona nitoe Ushauri mdogo kwenye kubadili muundo wa jiji la Dar es Salaam kwa Gharama na lazima.
Tumeona na tunashuhudia mitaa imejengwa kiholela mno mpaka aibu ambapo huduma za kijamii pia imekuwa ni Shida mno kwa walengwa. Mabadiliko ya kufumua mazingira kama haya huwa yanataka utashi mkubwa na waina yake kama ikiwa ni lazima.

Ushauri wangu kwa JPM kama wakiamini mawazo yangu mafupi yatafaa ingekuwa njema sana kulifanya jiji kuwa la kisasa.
Serikali iangalie mitaa ambayo ni holela lakini ardhi yake ina thamani japo imejengwa,

Serikali iamue kuingia na wadau au yenyewe kukaa na wakazi wa mtaa husika kwa lengo la kuitaifhisha ardhi yao na kufanya mfumo mbadala wa makazi, hii ina maana eneo husika lijengwe Apartment kubwa yenye japo gorofa zaidi ya kumi kwenda juu japo kila floor iweze beba kaya 5 mpaka sita na ilijenge sehemu husika yenye makazi holela kwa kuwatoa watakaoachia maeneo yao kwa muda ili kupisha ujenzi huo na jengo likikamilika basi kila mwenye nyumba chini apende juu kwa lazima kama hataki pole yake na nyumba za chini zote zivunjwe na kuacha maeneo wazi kwa malengo ya baadae.

ujenzi kama huu ukifanyika na maeneo fulani ya jiji serikali kwa mwaka ikijenga majengo kama hayo makubwa uwezekano wa miaka 5 kuwa na majengo makubwa kumi utakuwa umevunja majumba mengi na kupandisha watu kwenye magorofa na kujikuta tunakuwa na maeneo wazi mengi kwa maamuzi mengine.

Hili naona kama lingekuwa jema japo kufanya majaribio hata hapo manzese likaporomoshwa gorofa la ukweli watu wapande juu. gharama ya ujenzi itajifidia kwa maeneo wazi yatakayopatikana kwa sababu kutakuwa hakuna fidia ya pesa kwa yeyote.

Baadhi ya miji mikubwa duniani serikali humiliki majengo na kuwapa wakazi wake kwa gharama.
Natamani utashi huu uonekane kama wa maana kwa walio juu japo tuiondoe taswira ya jiji kwa sasa.
Nawakilisha..............................................................
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom