Ushauri wa mwisho kwa CHADEMA: Wafukuzeni Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Itumieni nafasi hiyo kurudi kwenye mstari!

Vipi kuhusu ACT NA CUF?Je,chanzo ni akina lowasa?Hoja yako haina fikra yakinifu hata
punje moja,bali hoja yako imejaa mapokeo ya ushabiki.shabiki yeyote logic kwake ni mwiko.
Hivi Mkuu umesahau kuwa hao ndo walikuwa wagombea na viongozi wakuu wa UKAWA mwaka 2015 wakati wa uchaguzi? Basi hao ndo wamepelekea migogoro CUF na sasa CHADEMA chama kubwa la matapeli kuanza kuparaganyika.
 
Inamana katika siasa hakuna hoja zingine zaidi ya UFISADI? Hakuna haja ya kushikana uchawi, opposition parties ought to be creative and know how to dance with the current beat. Only innovation and creativity can rescue them
Shallow reasoning! Unapoona dola inaanza kuua wapinzani kwa risasi unafanyaje? Amin alifanya hivi hiv! Ukombozi wao ulitoka nje ya Uganda, not within maana aliua wapinzani indiscriminately! Mtu mwenye majeshi yote anaeema bila kupepesa kuwa atahakikisha by all means anaua upinzani, kama mpinzani unafanyaje? Anasema wadhibiti bungeni, wakija huku nje ya bunge nawamaliza, unafanyaje?
 
Shallow reasoning! Unapoona dola inaanza kuua wapinzani kwa risasi unafanyaje? Amin alifanya hivi hiv! Ukombozi wao ulitoka nje ya Uganda, not within maana aliua wapinzani indiscriminately!
Nimeuliza swali kuwa katika upinzani hoja ni UFISADI pekee? Jibu hapo then twende sawa, mimi si mwanasiasa so jitahid kuweka focus kwenye fact rather than being pathetic
 
Hakika umenena vyema... Chadema lazima warudie misingi yao kama ilivyokuwa wakati wa Dr. Slaa. Ni miujiza kuamini Lowasa, Sumaye, Nyalandu na wafuasi wao wateleta mageuzi ya kweli.
 
CHADEMA msisake mchawi mbali na chama chenu. Mchawi mnaye, tena ndani kabisa. Mnaye Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Wafukuzeni hao chamani mwenu ili muimarike na mrudi katika misingi na mstari wenu. Ingawa mtakuwa mmechelewa, lakini mtakuwa mmekiponya chama chenu na gharika inayokikumba.

Kwa jicho la tatu, tangu Lowassa na wafuasi wake wahamie CHADEMA mambo yamebadilika. Hoja kuu ya CHADEMA ya ufisadi ima imeachwa au inazungumziwa kwa aibu kubwa. Kuhamia kwa Lowassa na wafuasi wake CHADEMA ni kama kuwafunga mdomo CHADEMA mliokuwa mkijipambanua kama wapambanaji wa ufisadi na hata kuwataja akina Lowassa kama mafisadi.

Tangu CHADEMA imkaribishe Lowassa, Sumaye na wafuasi wao na hata kuwaamini kwa kuwapa nafasi za uongozi za chama, CHADEMA imegeuka kituko kwa kuonekana kama vigeugeu na wasiosimamia maneno yao dhidi ya Lowassa na wengineo. Ndiyo maana hata mpango wa Wabunge na Madiwani wenu wanaohama umesukwa katika mtazamo huo.

Mpango huo kabambe wa kisiasa umesukwa katika namna ya kuuaminisha umma kuwa kwasasa mpiganaji wa rushwa na ufisadi ni Rais Magufuli na chama chake cha Mapinduzi na si CHADEMA tena. Wahamaji wanasema kuwa wanajiunga na CCM kwa kumuunga mkono Rais Magufuli katika vita ya ufisadi na kupigania rasilimali za taifa. Kisiasa, ni sawa na kusema kwasasa CHADEMA haina ajenda hiyo kwakuwa Lowassa yupo huko.

Jitafakarini muone mabadiliko ya kichama,kisera, kiitikadi na kiutendaji ya CHADEMA tangu kujiunga kwa Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Hakika, Lowassa hakuwahi kuwa mwanasiasa wa mfumo. Yeye hujijenga binafsi kwa ajili yake binafsi. Muda huu, anapigia mahesabu kugombea 2020 na hayo yanayoendelea wala hayamsumbui. Lakini, CHADEMA inapaswa kuimarika na kujirekebisha.

Muda wa uamuzi mgumu wa kumfukuza ndani ya CHADEMA Lowassa, Sumaye na wafuasi wao ni sasa. Mmepata penati dakika za lala salama. Ni do or die! Rejea zangu:

1.Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

2.Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA

3.Kadiri Lowassa anavyojiimarisha CHADEMA, ndivyo chama kinavyofifia na kupotea
NYINYI NYENYENYENYE,UKIFIKA BEI MKUU NAWE NENDA TU MAANA KWA SASA MMEAMUA KUJIAJIRI KWA STAILI YA AINA YAKE,KWENDA TU MKUUU HATA MSANDO NAYE KAENDA NA KWA NAMNA YAKE PIA
 
Mimi nadhani siku hizi umechuja sana, hoja zako zinakosa mashiko. Labda tuangalie mazingira ya siasa kabla na baada ya ujio wa Lowasa and Company:
1. Kabla ya Lowasa kuingia CDM, hii ikimaanisha wakati wa Mh Kikwete, democrasia ilikuwa pana. Watu waliweza kwenda Mwembe Yanga na kutangaza orodha ya mafisadi hadharani na hakuna mtu anakamatwa wala kupigwa risasi.

2. Wakati wa Kikwete CDM uliweza kufanya maandamano nchi nzima mpaka serikal ikaogopa, lakini hakuna akiyekamatwa wala kufunguliwa mashtaka.

3. Wakati wa Kikwete na Marehemu Sitta akiwa speaker na baadaye Mama Makinda, bunge lilikuwa ni bunge, tulishuhudia mara ngapi baraza la mawaziri kufumuliwa kwa kuwa wabunge wametoa maazimio.

4. Zama hizi za bullozer, Bwana mkubwa, hakuna mikutano ya kisiasa, hakuna maandamao, hakuna hata kukosoa kwenye mitandao ya kijamii? Sasa hizo agenda za ufisadi wazisemee wapi? Bunge ndilo hilo tena linaendeshwa gizani.

Sasa sijui Lowasa afukuzwe kwa kukosa nini? Hivi akili ya kibinadamu inakutuma kwamba Lowasa na wenzake ndio wamesababisha mkwamo huu wa kisiasa? Nawaza tu kwa sauti, je kama uhuru wa vyama vya siasa ungeendelezwa unadhani CDM ingekuwa kama hivyo unavyofikiria?

Pia nawaza ufisadi wa Lowasa ni upi? Na kwa nini hachuliwi hatua? Unataka kumfukuza Sumaye kwa nini hasa? Nini alichokosea?

Nadhani ili uheshimike zungumza mambo kiuhalisia na sio ki- ccm, ccm.

Utafanya jambo la maana kwa nchi hii kama utaingana na watanzania wapenda haki kudai mabadiliko ya katiba. Tanzania iwe huru zaidi, wanasiasa wafurahie kufanya siasa, pawe na taasisi zinazofanya kazi kuliko maonyesho ya mtu mmoja. Hofu iondoke miongoni kwa wa Tanzania. Ili uonnekana wa maana kama utawaambia ccm na washirika wao waache kulitia hasara Taifa kwa kurubuni wabunge na kulazimika kurudi kwenye uchaguzi. Utaonekana wa maana kama utawaasa wakuu wa dini kukemea hii hali inayofanya Taifa letu kutumbukia kwenye giza.

Kwa mwendo huu tuendako sio salama. Watu wako kimya na machungu myoyoni, na kuna siku isiyo na jina nchi italipuka (God forbid).

Mkuu

Andiko lako linaakisi fasiri tofauti tofauti sana.

Kwa mfano, Mh Kikwete wakati wa utawala wake alibatizwa jina la "Dhaifu" pale Bungeni Dodoma. Kama haitoshi wengine wakadiriki kutangza hadharani kwamba "tunataka raisi dikteta".

Kwa muktadha huu nafikiri ni Watanzania wachache sana wenye uelewa thabiti kuhusu nini hasa nchi inataka toka kwa viongozi wa kuchaguliwa ama kuteuliwa.
 
CHADEMA msisake mchawi mbali na chama chenu. Mchawi mnaye, tena ndani kabisa. Mnaye Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Wafukuzeni hao chamani mwenu ili muimarike na mrudi katika misingi na mstari wenu. Ingawa mtakuwa mmechelewa, lakini mtakuwa mmekiponya chama chenu na gharika inayokikumba.

Kwa jicho la tatu, tangu Lowassa na wafuasi wake wahamie CHADEMA mambo yamebadilika. Hoja kuu ya CHADEMA ya ufisadi ima imeachwa au inazungumziwa kwa aibu kubwa. Kuhamia kwa Lowassa na wafuasi wake CHADEMA ni kama kuwafunga mdomo CHADEMA mliokuwa mkijipambanua kama wapambanaji wa ufisadi na hata kuwataja akina Lowassa kama mafisadi.

Tangu CHADEMA imkaribishe Lowassa, Sumaye na wafuasi wao na hata kuwaamini kwa kuwapa nafasi za uongozi za chama, CHADEMA imegeuka kituko kwa kuonekana kama vigeugeu na wasiosimamia maneno yao dhidi ya Lowassa na wengineo. Ndiyo maana hata mpango wa Wabunge na Madiwani wenu wanaohama umesukwa katika mtazamo huo.

Mpango huo kabambe wa kisiasa umesukwa katika namna ya kuuaminisha umma kuwa kwasasa mpiganaji wa rushwa na ufisadi ni Rais Magufuli na chama chake cha Mapinduzi na si CHADEMA tena. Wahamaji wanasema kuwa wanajiunga na CCM kwa kumuunga mkono Rais Magufuli katika vita ya ufisadi na kupigania rasilimali za taifa. Kisiasa, ni sawa na kusema kwasasa CHADEMA haina ajenda hiyo kwakuwa Lowassa yupo huko.

Jitafakarini muone mabadiliko ya kichama,kisera, kiitikadi na kiutendaji ya CHADEMA tangu kujiunga kwa Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Hakika, Lowassa hakuwahi kuwa mwanasiasa wa mfumo. Yeye hujijenga binafsi kwa ajili yake binafsi. Muda huu, anapigia mahesabu kugombea 2020 na hayo yanayoendelea wala hayamsumbui. Lakini, CHADEMA inapaswa kuimarika na kujirekebisha.

Muda wa uamuzi mgumu wa kumfukuza ndani ya CHADEMA Lowassa, Sumaye na wafuasi wao ni sasa. Mmepata penati dakika za lala salama. Ni do or die! Rejea zangu:

1.Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

2.Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA

3.Kadiri Lowassa anavyojiimarisha CHADEMA, ndivyo chama kinavyofifia na kupotea
CHADEMA ni kama Hekalu/Kanisa/Msikiti wote wanakaribishwa kwa utakaso. Hata wewe mzinzi wa kisiasa unakaribishwa utakaswe.
 
Ili Mti Unawiri vizuri Sharti Majani yadondoke yaliyochoka yadondoke. (Kwa wanaojua miti). Kwa wasomaji wa Biblia Yesu akawauliza wanafunzi wake, "Je Nanyi mwataka kuondoka?" Ni vema miti ipukutike majani yaliyochoka
 
Yaani Umeniwahi leo niliamka ili niweke UZI huu kwa maneno yale yale ila content tofauti. Unatisha. haya ni maneno kuntu kwa chadema asilia.
 
CHADEMA msisake mchawi mbali na chama chenu. Mchawi mnaye, tena ndani kabisa. Mnaye Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Wafukuzeni hao chamani mwenu ili muimarike na mrudi katika misingi na mstari wenu....

Hakika, Lowassa hakuwahi kuwa mwanasiasa wa mfumo. Yeye hujijenga binafsi kwa ajili yake binafsi. Muda huu, anapigia mahesabu kugombea 2020 na hayo yanayoendelea wala hayamsumbui. Lakini, CHADEMA inapaswa kuimarika na kujirekebisha...

Petro E. Mselewa, hoja yako ya lei, hasa hayo niliyoyaacha kama nukuu, umegusa mzizi wa ugonjwa unaoisibu CHADEMA.

CCM ilisalimika ilipochukua uamuzi mzito wa kumkata Lowassa jina lake kugombea Urais. Uamuzi huo ulichukuliwa kwa kuwa CCM ni Taasisi na si chama cha mtu. Pamoja na jina lake kukatwa bado ilikuwa patashika nguo kuchanika siku ya kikao cha NEC CCM, kundi la Lowassa likitaka kushikiza jina lake lirudishwe kwenye mchakato.

Lowassa aliutaka Urais tangu enzi za Baba wa Taifa. Alipokataliwa, hakukata tamaa, aliendelea kujijenga kimakundi. Hata alipohamia CHADEMA, amehama na kundi lake - Team Lowassa.

Msikilize Baba wa Taifa

Japo Uchaguzi Mkuu 2020 hauko mbali, lakini uchaguzi Mkuu wa CHADEMA ndio utakuwa mtihani mkubwa wa uhai wa chama. Je, jina la Lowassa, akitaka kugombea Uenyekiti wa chama, litakatwa?
 
Hivi Mkuu umesahau kuwa hao ndo walikuwa wagombea na viongozi wakuu wa UKAWA mwaka 2015 wakati wa uchaguzi? Basi hao ndo wamepelekea migogoro CUF na sasa CHADEMA chama kubwa la matapeli kuanza kuparaganyika.
Kwahiyo wao ndiyo waliokataza mikutano ya hadhara?Wao ndiyo wanawatoa mawakala ktk vituo vyakupigia kura?Acha mawazo mbebesho.
 
Mkuu tujadiliane lakini usinipe uanachama wa chama chochote. Huo sina. Kama mnaukataa ushauri wangu, sawa.

Mkuu Petro kwenye hii hoja yako ya Lowassa tuko pamoja , ila sioni kumfukuza inawezekanaje maana itakuwa ni kama cdm wanafanyia kazi mawazo ya fitina. Nikiri kwamba kwa Sumaye na hasa Lowassa cdm walifanya kos la karne kumpokea. Wanachoweza kufanya tena iwe sasa ni kumfanya Lowassa na Sumaye kuwa wanachama wa kawaida na wasiwe na nafasi yoyote wala kugombea chamani. Baada ya hapo Mbowe atangaze kutokugombea tena uenyekiti msimu ujao.

Halafu wabadilishe katibu mkuu, huyo ndio awe mbele kwa kila kitu haswa majukwaani. Yeye ajikite kwenye kuuza siasa za maendeleo na siasa za madaraka aachiwe msemaji wa chama na Mbowe. Kuna mambo mengi ya kuuza kwa wananchi kama watakapoingia madarakani watashusha bei ya vifaa vya ujenzi ili kila mtu ajenge nyumba bora. Baadhi ya chombeza ni pamoja na kwamba watawalipa fidia wote waliobomolewa na kuporwa mali zao na erekali. Kwa wakulima wawaahidi kuwezesha kila familia ya mkulima kumiliki minimum heka 2 ya kilimo cha kisasa. Waahidi kuongeza ajira kwa vijana hasa kupitia kilimo cha kisasa. Upande wa elimu wasisitize ni bure mpaka chuo kikuu. Afya kila kijiji dispensary. Mikopo kwa wingi. Napendekeza ukatibu mkuu apewe mtu kama Marcus Albanie.

Kwenye siasa za madaraka msemaji wa chama na Mbowe waahidi kuleta katiba mpya tena ile ya maoni ya Warioba, chini ya miezi 6 wakiingia madarakani. Waseme demokrasia itarud kamanioivyokuwa kabla a kuharibiwa awamu hii ya tano. Wawaahidi wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa amani kama ilivyokuwa. Kwenye hayo makundi mawili ya siasa za maendeleo na madaraka wagawanyike na kuwapa wazungumzaji wazuri. Hili la sasa za madaraka pia mtu kama Lissu atafaa sana.

NB: Huku jamii forums nip mimi Tindo shabikia ambaye si mwanachama na wengineo. Ccm chini ya Magufuli lazima wakae na hata cdm wasipopata dola lazima tuwachonganishe na hizo ahadi. Mwisho hiyo itakuwa faida kwa umma.
 
ushauri mzuri , wengi walimpinga Dr , zito kuwaona wasaliti leo hii hao hao ndo wamegeuka wasaliti sishangai kuona kesho naambiwa you are now a admin,
hapo baada ya mbowe kuenda sisiem. hakuna kuaminiana tena...
 
Yanayoendelea CUF na chadema ni thibitisho kuwa mkuu kweli hakushinda 2015. Lilikuwa goli la mkono. Ndiyo maana badala ya kujenga viwanda, yeye amakazana kuvunja upinzani. Woga woga woga.
Kama alishinda kwa nini anatumia dola kushinda? Na vitisho, wizi wa kura, kununua watu??????
Woga wote ni Lowassa na Mbowe!!!!!!Seif!!!
Ebu aache awanja uwe haki kama atapata hata moja!
 
Umeandika pumba, kama Lowasa ni fisadi mbona hafikishiw mahakamani? Chenge, Geleja na Tabaijuka wako Chadema.

Mkuu Babati nadhani kama chama tunatakiwa tujitafakari nini chanzo cha haya yanayotupata? Je si kweli Lowasa tulimweka kwenye list of Shame na kumtaja hadhari pale Jangwani?

Pamoja na mkwanja wanaoutembeza ccm kuwasomba hawa njaa kali lakini chama chetu kinatakiwa kurudi kwenye line.
 
Back
Top Bottom