Ushauri wa mwisho kwa CHADEMA: Wafukuzeni Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Itumieni nafasi hiyo kurudi kwenye mstari!

Nitakuwa wa kwanza kuwasamehe kina Mbowe na kuwaunga mkono TENA.
Kina Salary Slip sio kabisa. Nawakumbuka hawa 4uM wakiwa sisiemu waliunanga upinzani na yeyote aliyempinga lowasa, wao walimpambania Lowassa leo wamekuja nae upande wa pili na kuharibu kabisa chama.
Umeongea kweli kabisa mleta uzi.
 
CHADEMA msisake mchawi mbali na chama chenu. Mchawi mnaye, tena ndani kabisa. Mnaye Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Wafukuzeni hao chamani mwenu ili muimarike na mrudi katika misingi na mstari wenu. Ingawa mtakuwa mmechelewa, lakini mtakuwa mmekiponya chama chenu na gharika inayokikumba.

Kwa jicho la tatu, tangu Lowassa na wafuasi wake wahamie CHADEMA mambo yamebadilika. Hoja kuu ya CHADEMA ya ufisadi ima imeachwa au inazungumziwa kwa aibu kubwa. Kuhamia kwa Lowassa na wafuasi wake CHADEMA ni kama kuwafunga mdomo CHADEMA mliokuwa mkijipambanua kama wapambanaji wa ufisadi na hata kuwataja akina Lowassa kama mafisadi.

Tangu CHADEMA imkaribishe Lowassa, Sumaye na wafuasi wao na hata kuwaamini kwa kuwapa nafasi za uongozi za chama, CHADEMA imegeuka kituko kwa kuonekana kama vigeugeu na wasiosimamia maneno yao dhidi ya Lowassa na wengineo. Ndiyo maana hata mpango wa Wabunge na Madiwani wenu wanaohama umesukwa katika mtazamo huo.

Mpango huo kabambe wa kisiasa umesukwa katika namna ya kuuaminisha umma kuwa kwasasa mpiganaji wa rushwa na ufisadi ni Rais Magufuli na chama chake cha Mapinduzi na si CHADEMA tena. Wahamaji wanasema kuwa wanajiunga na CCM kwa kumuunga mkono Rais Magufuli katika vita ya ufisadi na kupigania rasilimali za taifa. Kisiasa, ni sawa na kusema kwasasa CHADEMA haina ajenda hiyo kwakuwa Lowassa yupo huko.

Jitafakarini muone mabadiliko ya kichama,kisera, kiitikadi na kiutendaji ya CHADEMA tangu kujiunga kwa Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Hakika, Lowassa hakuwahi kuwa mwanasiasa wa mfumo. Yeye hujijenga binafsi kwa ajili yake binafsi. Muda huu, anapigia mahesabu kugombea 2020 na hayo yanayoendelea wala hayamsumbui. Lakini, CHADEMA inapaswa kuimarika na kujirekebisha.

Muda wa uamuzi mgumu wa kumfukuza ndani ya CHADEMA Lowassa, Sumaye na wafuasi wao ni sasa. Mmepata penati dakika za lala salama. Ni do or die! Rejea zangu:

1.Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

2.Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA

3.Kadiri Lowassa anavyojiimarisha CHADEMA, ndivyo chama kinavyofifia na kupotea
mimi naona ushauri huu hauna tofauti sana na ule wa kumshauri mchungaji/padri amfukuze kanisani malaya aliyeamua kwa hiari yake kumrudia Mungu na kuokoka.
 
Naamini kujitoa kwa wabunge kadhaa wa Chadema ndiyo chachu ya ushauri huu wa kuwafukuza Lowasa na Sumaye Chadema,

Hivi hawa wabunge wanaojitoa Chadema wamesema wanajitoa kwasababu ya Lowasa na Sumaye??

Ufisadi wa ujenzi wa Chato International Ariport ni Magufuli ndiyo ameuibua?

Vitendo vya rushwa alivyorekodiwa Mnyeti akivifanya ni Magufuli ndiyo alirekodi na kufichua?

Ndege ya nchi iliyokamatwa Canada kwa uzembe wa serikali ya CCM ni Magufuli ndiyo aliibua hoja husika?

Ufisadi kwenye ujenzi wa hostel za UDSM ni Magufuli ndiyo ameibua hizo hoja au ndiyo yeye kapiga deal?

Watanzania ni wajinga, ila wasomi wa nchi hii ni wajinga zaidi kwasababu wanashiriki kuwajaza raiya ujinga zaidi kutokana na uoga na kutojiamini.
 
Facts kabisa mkuu ila subiria matusi kutoka kwa vijana wa ufipa maana kuwakosoa na kuwashauri wao watakuona msaliti.
Hakuna logic hapo,bali kuna dhana ya mapokeo tu.Jiulize kuhusu ACT na CUF,je hao akina lowasa wapo kwenye hivyo vyama?
 
Hivi hawa wabunge wanaojitoa Chadema wamesema wanajitoa kwasababu ya Lowasa na Sumaye??

Ufisadi wa ujenzi wa Chato International Ariport ni Magufuli ndiyo ameuibua?

Vitendo vya rushwa alivyorekodiwa Mnyeti akivifanya ni Magufuli ndiyo alirekodi na kufichua?

Ndege ya nchi iliyokamatwa Canada kwa uzembe wa serikali ya CCM ni Magufuli ndiyo aliibua hoja husika?

Ufisadi kwenye ujenzi wa hostel za UDSM ni Magufuli ndiyo ameibua hizo hoja au ndiyo yeye kapiga deal?

Watanzania ni wajinga, ila wasomi wa nchi hii ni wajinga zaidi kwasababu wanashiriki kuwajaza raiya ujinga zaidi kutokana na uoga na kutojiamini.
Mkuu, nakuheshimu na naheshimu hoja zako. LAKINI, Lowassa na Sumaye et al si watu sahihi CHADEMA. Kumbuka, siasa ni propaganda.
 
CHADEMA msisake mchawi mbali na chama chenu. Mchawi mnaye, tena ndani kabisa. Mnaye Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Wafukuzeni hao chamani mwenu ili muimarike na mrudi katika misingi na mstari wenu. Ingawa mtakuwa mmechelewa, lakini mtakuwa mmekiponya chama chenu na gharika inayokikumba.

Kwa jicho la tatu, tangu Lowassa na wafuasi wake wahamie CHADEMA mambo yamebadilika. Hoja kuu ya CHADEMA ya ufisadi ima imeachwa au inazungumziwa kwa aibu kubwa. Kuhamia kwa Lowassa na wafuasi wake CHADEMA ni kama kuwafunga mdomo CHADEMA mliokuwa mkijipambanua kama wapambanaji wa ufisadi na hata kuwataja akina Lowassa kama mafisadi.

Tangu CHADEMA imkaribishe Lowassa, Sumaye na wafuasi wao na hata kuwaamini kwa kuwapa nafasi za uongozi za chama, CHADEMA imegeuke kituko kwa kuonekana kama vigeugeu na wasiosimamia maneno yao dhidi ya Lowassa na wengineo. Ndiyo maana hata mpango wa Wabunge na Madiwani wenu wanaohama umesukwa katika mtazamo huo.

Mpango huo kabambe wa kisiasa umesukwa katika namna ya kuuaminisha umma kuwa kwasasa mpiganaji wa rushwa na ufisadi ni Rais Magufuli na chama chake cha Mapinduzi na si CHADEMA tena. Wahamaji wanasema kuwa wanajiunga na CCM kwa kumuunga mkono Rais Magufuli katika vita ya ufisadi na kupigania rasilimali za taifa. Kisiasa, ni sawa na kusema kwasasa CHADEMA haina ajenda hiyo kwakuwa Lowassa yupo huko.

Jitafakarini muone mabadiliko ya kichama,kisera, kiitikadi na kiutendaji ya CHADEMA tangu kujiunga kwa Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Hakika, Lowassa hakuwahi kuwa mwanasiasa wa mfumo. Yeye hujijenga binafsi kwa ajili yake binafsi. Muda huu, anapigia mahesabu kugombea 2020 na hayo yanayoendelea wala hayamsumbui. Lakini, CHADEMA inapaswa kuimarika na kujirekebisha.

Muda wa uamuzi mgumu wa kumfukuza ndani ya CHADEMA Lowassa, Sumaye na wafuasi wao ni sasa. Mmepata penati dakika za lala salama. Ni do or die! Rejea zangu:

1.Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

2.Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA

3.Kadiri Lowassa anavyojiimarisha CHADEMA, ndivyo chama kinavyofifia na kupotea
Mimi nadhani siku hizi umechuja sana, hoja zako zinakosa mashiko. Labda tuangalie mazingira ya siasa kabla na baada ya ujio wa Lowasa and Company:
1. Kabla ya Lowasa kuingia CDM, hii ikimaanisha wakati wa Mh Kikwete, democrasia ilikuwa pana. Watu waliweza kwenda Mwembe Yanga na kutangaza orodha ya mafisadi hadharani na hakuna mtu anakamatwa wala kupigwa risasi.

2. Wakati wa Kikwete CDM uliweza kufanya maandamano nchi nzima mpaka serikal ikaogopa, lakini hakuna akiyekamatwa wala kufunguliwa mashtaka.

3. Wakati wa Kikwete na Marehemu Sitta akiwa speaker na baadaye Mama Makinda, bunge lilikuwa ni bunge, tulishuhudia mara ngapi baraza la mawaziri kufumuliwa kwa kuwa wabunge wametoa maazimio.

4. Zama hizi za bullozer, Bwana mkubwa, hakuna mikutano ya kisiasa, hakuna maandamao, hakuna hata kukosoa kwenye mitandao ya kijamii? Sasa hizo agenda za ufisadi wazisemee wapi? Bunge ndilo hilo tena linaendeshwa gizani.

Sasa sijui Lowasa afukuzwe kwa kukosa nini? Hivi akili ya kibinadamu inakutuma kwamba Lowasa na wenzake ndio wamesababisha mkwamo huu wa kisiasa? Nawaza tu kwa sauti, je kama uhuru wa vyama vya siasa ungeendelezwa unadhani CDM ingekuwa kama hivyo unavyofikiria?

Pia nawaza ufisadi wa Lowasa ni upi? Na kwa nini hachuliwi hatua? Unataka kumfukuza Sumaye kwa nini hasa? Nini alichokosea?

Nadhani ili uheshimike zungumza mambo kiuhalisia na sio ki- ccm, ccm.

Utafanya jambo la maana kwa nchi hii kama utaingana na watanzania wapenda haki kudai mabadiliko ya katiba. Tanzania iwe huru zaidi, wanasiasa wafurahie kufanya siasa, pawe na taasisi zinazofanya kazi kuliko maonyesho ya mtu mmoja. Hofu iondoke miongoni kwa wa Tanzania. Ili uonnekana wa maana kama utawaambia ccm na washirika wao waache kulitia hasara Taifa kwa kurubuni wabunge na kulazimika kurudi kwenye uchaguzi. Utaonekana wa maana kama utawaasa wakuu wa dini kukemea hii hali inayofanya Taifa letu kutumbukia kwenye giza.

Kwa mwendo huu tuendako sio salama. Watu wako kimya na machungu myoyoni, na kuna siku isiyo na jina nchi italipuka (God forbid).
 
Naamini kujitoa kwa wabunge kadhaa wa Chadema ndiyo chachu ya ushauri huu wa kuwafukuza Lowasa na Sumaye Chadema,

Hivi hawa wabunge wanaojitoa Chadema wamesema wanajitoa kwasababu ya Lowasa na Sumaye??

Ufisadi wa ujenzi wa Chato International Ariport ni Magufuli ndiyo ameuibua?

Vitendo vya rushwa alivyorekodiwa Mnyeti akivifanya ni Magufuli ndiyo alirekodi na kufichua?

Ndege ya nchi iliyokamatwa Canada kwa uzembe wa serikali ya CCM ni Magufuli ndiyo aliibua hoja husika?

Ufisadi kwenye ujenzi wa hostel za UDSM ni Magufuli ndiyo ameibua hizo hoja au ndiyo yeye kapiga deal?

Watanzania ni wajinga, ila wasomi wa nchi hii ni wajinga zaidi kwasababu wanashiriki kuwajaza raiya ujinga zaidi kutokana na uoga na kutojiamini.
Aliyewahi kuwa raisi wa Afrika kusini enzi za ubaguzi wa rangi bwana Peter Botta alisema"Mwafrika hata akisoma hawezi kuacha upumbavu wake kwakuwa amejawa na ubinafsi wa kuangalia tumbo lake.
 
Naamini kujitoa kwa wabunge kadhaa wa Chadema ndiyo chachu ya ushauri huu wa kuwafukuza Lowasa na Sumaye Chadema,

Hivi hawa wabunge wanaojitoa Chadema wamesema wanajitoa kwasababu ya Lowasa na Sumaye??

Ufisadi wa ujenzi wa Chato International Ariport ni Magufuli ndiyo ameuibua?

Vitendo vya rushwa alivyorekodiwa Mnyeti akivifanya ni Magufuli ndiyo alirekodi na kufichua?

Ndege ya nchi iliyokamatwa Canada kwa uzembe wa serikali ya CCM ni Magufuli ndiyo aliibua hoja husika?

Ufisadi kwenye ujenzi wa hostel za UDSM ni Magufuli ndiyo ameibua hizo hoja au ndiyo yeye kapiga deal?

Watanzania ni wajinga, ila wasomi wa nchi hii ni wajinga zaidi kwasababu wanashiriki kuwajaza raiya ujinga zaidi kutokana na uoga na kutojiamini.
Mmepewa ushauri mzuri sana, tena root cause ya matatizo yenu.
TAKE IT OR LEAVE IT AT YOUR OWN PERIL.
Kamanda Mwanahabari Huru aje huku.
 
Hoja yako ni nyepesi sana, ACT Wazalendo pia wana Sumaye na Lowassa? CUF pia wana Sumaye na Lowassa.

Wapinzani wote kwa sasa wanapitia wakati mgumu mno kuliko wowote ule tangu kuasisiwa kwa vyama vingi, CCM wanafanya kila wawezalo kwa kutumia vyombo vyao vya ki dola kuwavunja nguvu wapinzani.

Awamu ya nne (Awamu ya Demokrasia ) ilitoa room kubwa sana kwa wapinzani kujitanua na kwa CCM ya awamu ya tano imeliona hili kama ni kosa kwani wao wamekuja kivingine kabisa - ACT wanalia, CDM wanalia CUF wanalia kwa hujuma za waziwazi, hakuna mikutano ya kisiasa, migogoro inayopandikizwa kwenye vyama kila kukicha hasa CUF.

Uchaguzi ukifika ni vita kati yao na vyombo vya dola; kila kiongozi wa upinzani anachokisema ni uchochezi, Wabunge wa Upinzani ni kesi kesi kila uchao sasa badala ya kujenga chama kwenye maeneo yao wao wanashinda mahakamani kujitetea wasifungwe.

Mbunge anapobamwa Bungeni anapobanwa Uraiani apumulie wapi kisiasa? Pumzi ya siasa ni kurushusu viongozi kujenga vyama vyao katika kila ngazi. Tangu uasisi wa vyama vingi hapa nchini kwa sasa wapinzani wanapitia wakati mgumu mno.

Ushauri:
Ni muda huu sasa wanatakiwa kuonesha ukomavu kisiasa - wanaoondoka waruhusiwe kuondoka; wabuni njia nyingine ya kuimarisha vyama vyao; ni kweli wana wakati mgumu sana lakini hapa ndipo watakapokoma zaidi kama wapishapita hiki kiunzi salama.

Ni muda muafaka kwao kuanza harakati za kudai Tume huru ya uchaguzi, hilli nalo si jambo jepesi, ni vita nyingine.
 
Wamfukuze kwa kosa gani? Emotional over facts? Kuna aliyemlalamikia Lowasa ?
Ukuu wa wilaya unatafutwa kwa nguvu zote.

Sijasikia mtu yoyote akimlalamikia lowassa au sumaye, huyu anataka afukuzwe, unamfukuza mtu bila sababu?

Waliohama chadema sijawahi kusikia wakimtuhumu Lowassa na wafuasi wake.

Haya ndio matatizo ya njaa. Njaa mbaya sana.
 
Hivi sikuhizi watu wanatumia nini kufikiri? Maana ukisikiliza hoja zinazotolewa utakuta wala hazina uhusiano na kinachoitwa chanzo cha tatizo.Hivi Lowasa,Sumaye na wengineo ndiyo chanzo cha mawakala kutolewa ktk vituo vya kupigia kura?Je hizi kamata kamata za viongozi wa chadema zinasababishwa na akina lowasa?Je nguvu kubwa itumiwayo na mamlaka inasababishwa na akina lowasa?Je zuwio la mikutano ya kisiasa chanzo ni akina lowasa?Je akina lowasa ndiyo walioapa kuilinda katiba?
Je kushambuliwa kwa risasi kwa Mh Lissu kulitokana na akina Lowassa kuja chadema?
 
Inamana katika siasa hakuna hoja zingine zaidi ya UFISADI? Hakuna haja ya kushikana uchawi, opposition parties ought to be creative and know how to dance with the current beat. Only innovation and creativity can rescue them
 
Wasliti ni wanachama wao. Mimi si mwanachama wa yeyote. Mimi ni mwanachama wa ukweli na uwazi tu.
Msaliti ni nani na amefanyaje usaliti? Acha kujifanya hauna chama wakati umejificha nyuma ya mgongo wa ccm. Hoja yako haina mashiko kabisa. Magufuli ndiye aliyeharibu siasa za nchi hii. Lowasa hana mchango wowote na yanayotokea sasa.
 
Back
Top Bottom