Ushauri wa mwisho kwa CHADEMA: Wafukuzeni Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Itumieni nafasi hiyo kurudi kwenye mstari!

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,524
2,000
CHADEMA msisake mchawi mbali na chama chenu. Mchawi mnaye, tena ndani kabisa. Mnaye Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Wafukuzeni hao chamani mwenu ili muimarike na mrudi katika misingi na mstari wenu. Ingawa mtakuwa mmechelewa, lakini mtakuwa mmekiponya chama chenu na gharika inayokikumba.

Kwa jicho la tatu, tangu Lowassa na wafuasi wake wahamie CHADEMA mambo yamebadilika. Hoja kuu ya CHADEMA ya ufisadi ima imeachwa au inazungumziwa kwa aibu kubwa. Kuhamia kwa Lowassa na wafuasi wake CHADEMA ni kama kuwafunga mdomo CHADEMA mliokuwa mkijipambanua kama wapambanaji wa ufisadi na hata kuwataja akina Lowassa kama mafisadi.

Tangu CHADEMA imkaribishe Lowassa, Sumaye na wafuasi wao na hata kuwaamini kwa kuwapa nafasi za uongozi za chama, CHADEMA imegeuka kituko kwa kuonekana kama vigeugeu na wasiosimamia maneno yao dhidi ya Lowassa na wengineo. Ndiyo maana hata mpango wa Wabunge na Madiwani wenu wanaohama umesukwa katika mtazamo huo.

Mpango huo kabambe wa kisiasa umesukwa katika namna ya kuuaminisha umma kuwa kwasasa mpiganaji wa rushwa na ufisadi ni Rais Magufuli na chama chake cha Mapinduzi na si CHADEMA tena. Wahamaji wanasema kuwa wanajiunga na CCM kwa kumuunga mkono Rais Magufuli katika vita ya ufisadi na kupigania rasilimali za taifa. Kisiasa, ni sawa na kusema kwasasa CHADEMA haina ajenda hiyo kwakuwa Lowassa yupo huko.

Jitafakarini muone mabadiliko ya kichama,kisera, kiitikadi na kiutendaji ya CHADEMA tangu kujiunga kwa Lowassa, Sumaye na wafuasi wao. Hakika, Lowassa hakuwahi kuwa mwanasiasa wa mfumo. Yeye hujijenga binafsi kwa ajili yake binafsi. Muda huu, anapigia mahesabu kugombea 2020 na hayo yanayoendelea wala hayamsumbui. Lakini, CHADEMA inapaswa kuimarika na kujirekebisha.

Muda wa uamuzi mgumu wa kumfukuza ndani ya CHADEMA Lowassa, Sumaye na wafuasi wao ni sasa. Mmepata penati dakika za lala salama. Ni do or die! Rejea zangu:

1.Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

2.Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA

3.Kadiri Lowassa anavyojiimarisha CHADEMA, ndivyo chama kinavyofifia na kupotea
 

Jaimee

JF-Expert Member
Aug 4, 2017
2,632
2,000
Hivi sikuhizi watu wanatumia nini kufikiri? Maana ukisikiliza hoja zinazotolewa utakuta wala hazina uhusiano na kinachoitwa chanzo cha tatizo.Hivi Lowasa,Sumaye na wengineo ndiyo chanzo cha mawakala kutolewa ktk vituo vya kupigia kura?Je hizi kamata kamata za viongozi wa chadema zinasababishwa na akina lowasa?Je nguvu kubwa itumiwayo na mamlaka inasababishwa na akina lowasa?Je zuwio la mikutano ya kisiasa chanzo ni akina lowasa?Je akina lowasa ndiyo walioapa kuilinda katiba?
 

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,524
2,000
Hivi sikuhizi watu wanatumia nini kufikiri? Maana ukisikiliza hoja zinazotolewa utakuta wala hazina uhusiano na kinachoitwa chanzo cha tatizo.Hivi Lowasa,Sumaye na wengineo ndiyo chanzo cha mawakala kutolewa ktk vituo vya kupigia kura?Je hizi kamata kamata za viongozi wa chadema zinasababishwa na akina lowasa?Je nguvu kubwa itumiwayo na mamlaka inasababishwa na akina lowasa?Je zuwio la mikutano ya kisiasa chanzo ni akina lowasa?Je akina lowasa ndiyo walioapa kuilinda katiba?
Mkuu, think big. Wake up!
 

G4rpolitics

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
3,766
2,000
Nalo wazo mkuu, nakuunga mkono, ni bora uwe imara hata kma una wafuasi wachache wenye msimamo kuliko kuwa na mamluki ambayo hujui kesho yatakuja na wazo gani.
 

Jaimee

JF-Expert Member
Aug 4, 2017
2,632
2,000
Vipi kuhusu ACT NA CUF?Je,chanzo ni akina lowasa?Hoja yako haina fikra yakinifu hata
punje moja,bali hoja yako imejaa mapokeo ya ushabiki.shabiki yeyote logic kwake ni mwiko.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom