Ushauri wa mtumishi wa Mungu...!

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,107
2,504
Kuna hiki kisa ambacho nilikipata jana baada ya jamaa yangu kujieleza kuhusu shida yake inayohusiana na mambo ya mapenzi, chanzo cha jamaa kujieleza ni kufuatia habari ya mwenzetu mmoja kutangaza uchumba na mchumba wake.

Ni hivi: Jamaa ana wasichana watatu, mmoja wa miaka karibu 8, mwingine wa mwaka mmoja na zaidi mwingine wa miezi karibu 8 hivi.

Kwa maelezo ya jamaa anasema, huyu wa miaka 8 (wamepishana miaka 6) ni kama wamezoeana sana na wamefikia hatua kama vile ni wachumba ila wasiwasi wake ni kwamba ni msichana wa nyumbani kwa dada yake, ni penzi la siri lkn ndugu zake wanajua kuhusu uhusiano wao (maana penzi halina pazia), aliwatonya ndugu zake kadhaa mpaka marafiki zake wanajua kuhusu hilo na hata wazazi wake alishawaeleza, lkn wazazi wake walimwambia asiseme mpaka huyo dada amalize shule kwanza maana akisema (kuweka wazi) shule yake itasimama. Tatizo ni kwa ndugu zake, ni kama vile wanajaribu kumzuia jamaa yangu asiwe karibu naye (huyo msichana) kwa maana ni mfanyakazi wa ndani na akiwa karibu naye atawaletea aibu katika familia yao. Kinachompa shida ni jamaa kutangaza uhusiano wakati ndugu zake wameonekana kuupiga vita dhidi ya uhusiano wake. Kimahusiano wanaendlea vizuri sana na kinachofurahisha kila wakiachana lazima wasali pamoja then wanaachana kila mtu na njia yake katika kuhangaikia maisha ila hawaishi pamoja lkn huwa wanaonana mara kwa mara na wanawsiliana sana.

Huyu wa mwaka mmoja na zaidi wao ni kama ndugu vile wa kutoka kijiji kimoja, familia zao ni familia marafiki, lkn huyu binti alionesha kumpenda jamaa toka zamani yaani binti alipokuwa mdogo,jamaa alikuwa hajui kama binti alikuwa anampenda na binti alimchokoza kupitia kwenye mtandao wa kijamii, uhusiano ulikomazwa kuanzia hapo,wao wamepishana takriban miaka kama 13 hivi, binti ameonesha nia ya kuwa naye karibu, tatizo jamaa anatatizwa na huyu binti kwenye mawasiliano, kila jamaa akipanga kwenda kumwona binti anakuwa kama anamkwepa, hadi mawasiliano yao yakasuasua, alipomuuliza kulikoni binti alimjibu shule inambana ikabidi jamaa apunguze kuwasiliana naye kiasi cha binti kuona kama amemtupa vile, jamaa yangu alitaka kujua msimamo wa binti upoje juzi juzi alimtumia ujumbe binti akamjibu kwamba ana "deni kubwa sana la kumwona jamaa". Sasa hapo jamaa hamwelewi binti anamaanisha nini? (ingawa jamaa yangu hakunieleza bayana kama ameenda kumuona au ila nitawajuza lkn)

Tukija huyu wa tatu wa miezi 8 huyu alimpata kupitia kwenye mitandao ya kijamii, waliwasiliana sana tena kwa muda mrefu sana, jamaa yangu anasema ana deni moja tu kwa huyu binti ya kwenda kumuona maana yupo nje ya mkoa anakoishi jamaa, (kinachomfanya ashindwe kwenda ni nauli), jamaa anasema tatizo la hapa ni mawasiliano pia ila tofauti kidogo na la wa mwaka mmoja na zaidi, tatizo la hapa ni huko huko kwenye mtandao wa kijamii, huyu binti aliweka bandiko la mambo ya kimapenzi na mtu mwingine kitu ambacho kilimwingia wivu jamaa yangu, alipomuuliza binti akamjibu kwa kumuomba msamaha na kuongeza kwamba kuanzia hapo hatarudia tena kucheza huo mchezo, lkn siku mmoja katika mawasiliano binti aliwahi kumjibu kwamba "hata tusipokuwa lovers tunaweza kubaki kuwa kama marafikiwa kawaida!" kitu ambacho jamaa alijiuliza kulikoni? juzi juzi jamaa alimuuliza unataka nikusaidie nini binti akamjibu "Nataka nisikie kilichoko kwenye moyo wako" jamaa akamjibu kwamba "Kilichoko kwenye moyo wangu ni hii: unataka nini kutoka kwangu?" binti akamjibu "Nataka amani na faraja katika maisha yangu" sasa hapo ni kama anampa taarifa kamili kuhusu msimamo wa binti.

Jamaa alisongwa na mawazo mengi kuhusu hawa watatu na lengo lake ni kumpata wa kutulia naye maishani, kitu ambacho jamaa alidhamiria kwamba yeyote atakayempa mimba ndo atakuwa wa kwake, jamaa yangu alisita kufanya hivyo akaamua kumtafuta Mtumishi wa Mungu amuombee kuhusu shida yake na alimpatia majina ya hawa wasichana watatu.

Majibu ya mtumishi: Mtumishi alimjibu wa miaka 8 ndo wa kwake kabisa baada ya kufanya maombi, hawa wengine siyo wa kwake, jamaa aliongezea kwamba huyu wa mwaka mmoja na zaidi ni kama amemkubali zaidi ya wa miaka 8 tofauti na majibu ya Mtumishi wa Mungu. Mtumishi alimsisitizia kufuata ushauri wake kwamba abaki na wa miaka 8.

Jamaa anashindwa afuate lipi, afuate kwa ushauri wa Mtumishi wa Mungu au afuate kile kilichomsukuma yeye?

*Jamaa si memba wa humu jamiiforum. Hapa ni kama namsaidia kumtafutia ushauri.
 
Sina budi kuungana na mtumishi wa Mungu kwenye hili,wa miaka 8 ndo anamfaa zaidi kuliko hawa wengine wawili kwa sababu amekua nae kwa mda mrefu,ameshamuelewa in and out,wazazi wanamkubali...swala la ndugu ni dogo sana kwa sababu mtu kua mfanyakazi wa ndani sio mwisho wa maisha anaweza kujiendeleza kwa namna yoyote ile na maisha yake yakabadilika,mbona kuna wanawake kibao hawajasoma lakini wameolewa??hakuna haja ya kusikiliza maneno ya ndugu cause atakayeishi na huyo binti ni yeye na sio ndugu..
Kuhusu hao wengine naona wana mapungufu makubwa kuliko huyo wa miaka 8..
 
Wa miaka NANE anafaa ila msihusishe Maombi semeni ni mawazo yenu.

Kuna hiki kisa ambacho nilikipata jana baada ya jamaa yangu kujieleza kuhusu shida yake inayohusiana na mambo ya mapenzi, chanzo cha jamaa kujieleza ni kufuatia habari ya mwenzetu mmoja kutangaza uchumba na mchumba wake.

Ni hivi: Jamaa ana wasichana watatu, mmoja wa miaka karibu 8, mwingine wa mwaka mmoja na zaidi mwingine wa miezi karibu 8 hivi.

Kwa maelezo ya jamaa anasema, huyu wa miaka 8 (wamepishana miaka 6) ni kama wamezoeana sana na wamefikia hatua kama vile ni wachumba ila wasiwasi wake ni kwamba ni msichana wa nyumbani kwa dada yake, ni penzi la siri lkn ndugu zake wanajua kuhusu uhusiano wao (maana penzi halina pazia), aliwatonya ndugu zake kadhaa mpaka marafiki zake wanajua kuhusu hilo na hata wazazi wake alishawaeleza, lkn wazazi wake walimwambia asiseme mpaka huyo dada amalize shule kwanza maana akisema (kuweka wazi) shule yake itasimama. Tatizo ni kwa ndugu zake, ni kama vile wanajaribu kumzuia jamaa yangu asiwe karibu naye (huyo msichana) kwa maana ni mfanyakazi wa ndani na akiwa karibu naye atawaletea aibu katika familia yao. Kinachompa shida ni jamaa kutangaza uhusiano wakati ndugu zake wameonekana kuupiga vita dhidi ya uhusiano wake. Kimahusiano wanaendlea vizuri sana na kinachofurahisha kila wakiachana lazima wasali pamoja then wanaachana kila mtu na njia yake katika kuhangaikia maisha ila hawaishi pamoja lkn huwa wanaonana mara kwa mara na wanawsiliana sana.

Huyu wa mwaka mmoja na zaidi wao ni kama ndugu vile wa kutoka kijiji kimoja, familia zao ni familia marafiki, lkn huyu binti alionesha kumpenda jamaa toka zamani yaani binti alipokuwa mdogo,jamaa alikuwa hajui kama binti alikuwa anampenda na binti alimchokoza kupitia kwenye mtandao wa kijamii, uhusiano ulikomazwa kuanzia hapo,wao wamepishana takriban miaka kama 13 hivi, binti ameonesha nia ya kuwa naye karibu, tatizo jamaa anatatizwa na huyu binti kwenye mawasiliano, kila jamaa akipanga kwenda kumwona binti anakuwa kama anamkwepa, hadi mawasiliano yao yakasuasua, alipomuuliza kulikoni binti alimjibu shule inambana ikabidi jamaa apunguze kuwasiliana naye kiasi cha binti kuona kama amemtupa vile, jamaa yangu alitaka kujua msimamo wa binti upoje juzi juzi alimtumia ujumbe binti akamjibu kwamba ana "deni kubwa sana la kumwona jamaa". Sasa hapo jamaa hamwelewi binti anamaanisha nini? (ingawa jamaa yangu hakunieleza bayana kama ameenda kumuona au ila nitawajuza lkn)

Tukija huyu wa tatu wa miezi 8 huyu alimpata kupitia kwenye mitandao ya kijamii, waliwasiliana sana tena kwa muda mrefu sana, jamaa yangu anasema ana deni moja tu kwa huyu binti ya kwenda kumuona maana yupo nje ya mkoa anakoishi jamaa, (kinachomfanya ashindwe kwenda ni nauli), jamaa anasema tatizo la hapa ni mawasiliano pia ila tofauti kidogo na la wa mwaka mmoja na zaidi, tatizo la hapa ni huko huko kwenye mtandao wa kijamii, huyu binti aliweka bandiko la mambo ya kimapenzi na mtu mwingine kitu ambacho kilimwingia wivu jamaa yangu, alipomuuliza binti akamjibu kwa kumuomba msamaha na kuongeza kwamba kuanzia hapo hatarudia tena kucheza huo mchezo, lkn siku mmoja katika mawasiliano binti aliwahi kumjibu kwamba "hata tusipokuwa lovers tunaweza kubaki kuwa kama marafikiwa kawaida!" kitu ambacho jamaa alijiuliza kulikoni? juzi juzi jamaa alimuuliza unataka nikusaidie nini binti akamjibu "Nataka nisikie kilichoko kwenye moyo wako" jamaa akamjibu kwamba "Kilichoko kwenye moyo wangu ni hii: unataka nini kutoka kwangu?" binti akamjibu "Nataka amani na faraja katika maisha yangu" sasa hapo ni kama anampa taarifa kamili kuhusu msimamo wa binti.

Jamaa alisongwa na mawazo mengi kuhusu hawa watatu na lengo lake ni kumpata wa kutulia naye maishani, kitu ambacho jamaa alidhamiria kwamba yeyote atakayempa mimba ndo atakuwa wa kwake, jamaa yangu alisita kufanya hivyo akaamua kumtafuta Mtumishi wa Mungu amuombee kuhusu shida yake na alimpatia majina ya hawa wasichana watatu.

Majibu ya mtumishi: Mtumishi alimjibu wa miaka 8 ndo wa kwake kabisa baada ya kufanya maombi, hawa wengine siyo wa kwake, jamaa aliongezea kwamba huyu wa mwaka mmoja na zaidi ni kama amemkubali zaidi ya wa miaka 8 tofauti na majibu ya Mtumishi wa Mungu. Mtumishi alimsisitizia kufuata ushauri wake kwamba abaki na wa miaka 8.

Jamaa anashindwa afuate lipi, afuate kwa ushauri wa Mtumishi wa Mungu au afuate kile kilichomsukuma yeye?

*Jamaa si memba wa humu jamiiforum. Hapa ni kama namsaidia kumtafutia ushauri.
 
Jamaa anapenda kupitia mitandao ya jamii halafu anafika bei kabisa?? Anyway, namshauri amuoe huyo wa miaka nane, mana anamjua kiundani,,
 
Hahaha! Ati Mungu baba wa Mbinguni, kati ya hawa watatu ninaozini nao unionyeshe uliyenichagulia! Kiboko!
Mi nimemuombea rafiki yako, Mungu amejibu sample size ni ndogo sana. So aongeze wengine wawili afu turudie kutoa sadaka ya nabii.
Maaluni huyo hata nauli ya kwenda mkoa hawezi, anatembea na hgeli wa dadake! Undugu mzigo!
Wa miaka NANE anafaa ila msihusishe Maombi semeni ni mawazo yenu.
 
mtaka mengi kwa pupa......,hii inanikumbusha hadithi ya fisi ya kutaka kuhudhuria sherehe zote alizoalikwa kwa mkupuo, zote zilikuwa siku moja na wakati mmoja, na yeye alitaka kufaidi kote na akaishia kukosa kote!! huyo mwenzio ndo afanyalo... huwezi linganisha watu, kila mmoja anayo mapungufu yake, na hakuna mmoja ambaye atakuwa na vigezo vyoote unavyotaka anavyotaka yeye!! kwa mtindo huo wa kuangaza macho pote, ataambulia chongo tu..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom