Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Amani iwe kwenu.
Sasa imebidi Mbowe aelewe bila kificho kuwa amepwaya kuwa KUB. Imefika wakati lazima ajue KUB ni mtumishi wa umma kama mawaziri hivyo tunalazimika kumwambia ukweli kwa manufaa ya taifa.
Hivi sasa upinzani bungeni umejigawa katika pande mbili; wanaojiita Ukawa chini ya Mbowe na ACT Wazalendo chini ya mbunge pekee Zitto Kabwe. Imedhihirika dhahiri shahiri wabunge wa "ukawa" michango yao imejikita kwenye kushambulia watu na sio hoja ukilinganisha na Zitto ambaye michango yake imejikita kuleta fikra mbadala katika kuharakisha maendeleo ya wananchi.
KUB Mbowe anahitaji "back up" ambayo Zitto alimpa bunge la 10 iliyoficha mapungufu yake lukuki ikiwemo kiueledi. Kushirikiana na Zitto sio tu itamwezesha kutumia kipaji chake bali itaziba ombwe la uongozi kambi ya upinzani. Amethibisha uwezo wa kushawishi kambi zote bungeni kuacha itikadi na kusimamia serikali ambapo mara kadhaa mawaziri waliwajibika.
Mbowe wabunge wengi ulionao ni mizigo waliojaa ubishi na uongo.
Pia nawaeleza wabunge kuwa vijembe, bunge live na matusi havileti maji, barabara, madawa nk kwa wananchi hivyo mjikite kwenye mijadala yenye tija.
Hoja hii ni ya ushauri wa lazima japo una hiyari ya kuchukua ama kuacha, ila muda ndio jibu.
Nawasilisha.