Ushauri wa kuichangia JF


Mupirocin

Mupirocin

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
1,601
Likes
44
Points
145
Mupirocin

Mupirocin

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
1,601 44 145
wana JF habari za asubuhi. naomba kutoa ushauri kwa invisible namna kuichangia JF ukwaa ambalo linazidi kukua na kuwa msaada sana kwa Watanzania. nisiwe muuzaji wa chai sana, niende moja kwa moja kwenye point.

Ni hivi nmshauri invisible kama ataweza afungue namba ya simu ambayo mtu binafsi anaweza kujiunga ili kila siku aingizapo vocha awe anakatwa labda Tsh 200 kwa siku ambapo kwa members 50,401 kama kila mtu atajiunga tutakuwa tunachangia 10,080,200/= kwa siku, kwa mwezi sawa na 30,240,600/= naamini hii itasaidia kuuwezesha mtandao wetu ujiendeshe kwa michango ya members, likini hii iwe open hata kwa wale ambao si member.

Yaani mfano iwepo namba kama hii 1557 na ili kujiunga tuseme unatuma neno JF kwenda kwenye hii namba na automatically utakuwa umejiunga na utachangia Tsh 200 kwa siku. Ujumbe uwepo kwenye first page kabisa ili kila mtu akifungua ausome badala kwa sasa mtu mpaka atafute ofisi au atumie account.

Ukiangalia kwenye majina ya members ambao waekuwa bolded na inasaikiwa kuwa ndo wachangiaji kwa kweli ni wachache sana tukifanya hivi naamini mtandao huu utaboreka na utatusaidia sana kufikia mabadiliko.

Nakuomba invisible uongee na mitandao ya simu naamin members hawana shida watachangia tu.

Naomba kuwasilisha, nipotayari kurekebishwa.
 
ndetichia

ndetichia

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Messages
27,735
Likes
2,004
Points
280
ndetichia

ndetichia

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2011
27,735 2,004 280
hii iliyopo tu watu wanaipokea kishingo upande je hiyo ya kukatwa daily we unataka watu wakimbie jamvi kiaina fikiria tena..
 
ndetichia

ndetichia

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Messages
27,735
Likes
2,004
Points
280
ndetichia

ndetichia

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2011
27,735 2,004 280
Kwanza na wewe umechangia kama bado namba hii hapa 0713444649 ndio uandike hiyo topic
 
Caroline Danzi

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2008
Messages
3,613
Likes
59
Points
145
Caroline Danzi

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2008
3,613 59 145
tehe tehe kusema rahisi sana!
 
Husninyo

Husninyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Messages
23,814
Likes
647
Points
280
Husninyo

Husninyo

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2010
23,814 647 280
Nikiweka vocha ya jelo sh 200 hiyooo. Nisipoweka vocha wiki nzima inakuwaje?
Hiyo idadi yako ya members nayo ujue kuna watu hapo wana IDs zaidi ya 2. Hebu kajipange upya meeeeen!
 
HAZOLE

HAZOLE

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2011
Messages
1,375
Likes
103
Points
160
HAZOLE

HAZOLE

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2011
1,375 103 160
maswali kwa mtoa mada;
1. kwani JF founders wamesema kwamba hawawezi kuiendesha JF au wanamatatizo?
2. je kwa wale tunaoweka e.g 2500 bundle ya airtel, TCL broadband, vodacom 250MB je huoni ni usumbufu??
3. huoni pia kuingia mikataba na makampuni ya simu ni complications tu?
swali langu la kwanza ndo lamuhimu, huwezi pendekeza kumsaidia mtu wakati hujui kama anashida.
pia sioni gharama au changamoto za ajabu za kuiendesha JF.
 
MIUNDOMBINU

MIUNDOMBINU

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2010
Messages
452
Likes
25
Points
45
MIUNDOMBINU

MIUNDOMBINU

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2010
452 25 45
Mkuu. Kwa hili umekurupuka tu, bila ya kufanya tathimini .
 
Apollo

Apollo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2011
Messages
4,892
Likes
1,473
Points
280
Age
28
Apollo

Apollo

JF-Expert Member
Joined May 26, 2011
4,892 1,473 280
maswali kwa mtoa mada;
1. kwani JF founders wamesema kwamba hawawezi kuiendesha JF au wanamatatizo?
2. je kwa wale tunaoweka e.g 2500 bundle ya airtel, TCL broadband, vodacom 250MB je huoni ni usumbufu??
3. huoni pia kuingia mikataba na makampuni ya simu ni complications tu?
swali langu la kwanza ndo lamuhimu, huwezi pendekeza kumsaidia mtu wakati hujui kama anashida.
pia sioni gharama au changamoto za ajabu za kuiendesha JF.
kuna gharama kubwa sana ndugu yangu. Usiongee tu. JF inategemea michango yetu. Tafuta kuna topic inayoelezea kwa undani.
 
Apollo

Apollo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2011
Messages
4,892
Likes
1,473
Points
280
Age
28
Apollo

Apollo

JF-Expert Member
Joined May 26, 2011
4,892 1,473 280
Naahidi kutoa 5000 kila mwezi. Nitaanza wiki ijayo kwa kutumia pesa ya 'zap'
 
Apollo

Apollo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2011
Messages
4,892
Likes
1,473
Points
280
Age
28
Apollo

Apollo

JF-Expert Member
Joined May 26, 2011
4,892 1,473 280
maswali kwa mtoa mada;
1. kwani JF founders wamesema kwamba hawawezi kuiendesha JF au wanamatatizo?
2. je kwa wale tunaoweka e.g 2500 bundle ya airtel, TCL broadband, vodacom 250MB je huoni ni usumbufu??
3. huoni pia kuingia mikataba na makampuni ya simu ni complications tu?
swali langu la kwanza ndo lamuhimu, huwezi pendekeza kumsaidia mtu wakati hujui kama anashida.
pia sioni gharama au changamoto za ajabu za kuiendesha JF.
hii ni post kutoka kwa wenyewe
Mkuu wangu Sikonge,

Ukweli ni kuwa siku za nyuma tulijaribu sana kuwafahamisha members kuwa JF haiendeshwi kwa fedha za watu flani bali kwa kujitolea.

Tukatanabaisha wazi kuwa wanachama na wote wenye mapenzi mema inabidi watambue kuwa tuna mzigo mkubwa wa kubeba kwa niaba yao.

Nyakati hizo tulikuwa na wanachama waliojisajili karibia 2,000 hivi na tukasema endapo kila mwanachama (aliyejisajili) angechangia Tshs 10,000/= basi ilimaanisha kuwa tungepata Tshs 20,000,000/= ambayo kwa wakati huo ingetosheleza kuiendesha JF kwa karibia mwaka mzima bila wasiwasi.

Maisha yakabadilika, Server tuliyokuwa nayo ilikuwa ndogo sana kumbe kulinganisha na uhitaji wa watanzania, balaa lilionekana wazi Mwezi Februari 2008 pale Mhe. Lowassa alipokuwa akijieleza Bungeni... Server ikachemsha kubeba mzigo mkubwa.

Kwa wakati huo tukaona ni vema tukaangalia namna ya kuweza kuwashirikisha wanachama juu ya ugumu tunaokumbana nao... Tukalazimika kununua server kubwa zaidi mbili na zenye back up za kila baada ya masaa 6 kwa nyakati tofauti.

Hilo likasaidia japo kwa gharama ambazo zilitoka mfukoni mwa mwanachama mmoja! Ndiyo, kulipia server hizo kila mwezi ni $940 na ameendelea kufanya hivyo kwa imani kuwa kuna siku mambo yataenda sawa.

JF inahitaji SANA michango ya watanzania na wote wenye mapenzi mema.

Kuna wanachama ambao humu mnawaona wana usernames ambazo ni bolded, hawa ni Premium Members. Hawa walau wamechangia kwa kiwango cha kuanzia $5 na wawili walau $300 tangu JF inaanzishwa mwaka 2006 (ikijulikana kama JamboForums).

Tangu JF inaanza (2006) mpaka sasa Januari 9, 2009, tumekwishapokea jumla ya US$ 1,450/= toka kwa wanachama waliojisajili na wasiojisajili.

Wengi wa waliohitaji kuchangia walikuwa wanatuma barua pepe nasi tunawapa maelekezo juu ya namna ya kutufikishia michango hiyo.

Ukweli ni kwamba kwa wasio wanachama wa JF wakiwa wanasoma hapa wanaona matangazo mengi ya Google kuliko wanachama waliojisajili.

Dhamira yetu si kuweka matangazo haya ya Google kwani hayaingizi kwa kiwango kikubwa hivyo, watu hawabonyezi matangazo hayo na hivyo income yake inategemea pale mtu atakapokosea akabonyeza tangazo ndipo tupate vijisenti kidogo kwa clicks hizo. Gharama za uendeshaji bado zinatoka mfukoni mwa mtu mmoja mpaka sasa na baadhi ya Premium Members ambao wameendelea kuona umuhimu wa kufanya hivyo.

Mpaka sasa JF ina wanachama waliojisajili zaidi ya 35,000. Endapo waliojili hawa wangechangia walau Tshs 10,000/= kwa mwaka basi inamaanisha JF ingetengeneza Tshs 350,000,000/= kwa mwaka na hivyo tusingeweka matangazo KABISA na tungejitahidi kupata moderators ambao watakuwa wanalipwa kwa kazi yao na wangeifanya kwa umakini mkubwa zaidi.

Ukiangalia katika historia ya Forums nyingi, huwa zinashindwa kuhimili traffic inapokuwa kubwa kutokana na servers kuhitaji umakini zaidi na Forum owners hujikuta wanaona ni mzigo usio na faida hivyo forums hizo kufa.

Tumshukuru Maxence kwa kuendelea kulipia gharama hizi kila mwezi kwa kujitolea mpaka sasa huku akilipia na Chat Server (IRC Server).

Wapo wanachama kama Ogah, Nyambala, SteveD, FairPlayer, Mchukia Fisadi na Phillemon Mikael ambao huchangia walau kila wanapopata wasaa... Hawa nao wamesaidia kwa kiwango kikubwa katika jitihada za kuhakikisha JF inakuwa hewani. Bila kuwasahau wadau waliochangia walau $200 hivi initially kama Mtanzania, Field Marshal ES na Halisi.

Ninachoamini binafsi ni kitu kimoja, Tshs 5,000/= kwa mwaka (12months, walau 450 kwa mwezi) inawezekana kabisa kwa watanzania tulio na uwezo wa kuingia mtandaoni. Na uzuri, benki zetu Tanzania zinaruhusu mtu ku-deposit Tshs 5,000/= kama kiwango cha chini.

Endapo kuna mwanachama anaguswa (kutoka moyoni) na angependa kuiwezesha JF kuendelea kusimama imara na kufanya vema zaidi bila mizengwe ya kifedha, basi anaweza kukubali kuchangia Tshs 5,000/= walau kwa mwaka.

Benki zetu (hapa naongelea walau NBC na CRDB kwa haraka) hazikulazimishi unayetuma hela kuandika jina lako la kweli bali lile ambalo ungependa mpokeaji alitambue.

Kwa walio Tanzania wanaweza kuichangia JF kwa kutuma katika akaunti za NBC au CRDB.

Akaunti ambazo tangu awali tulipendekeza zitumiwe ni za Maxence Melo (as the JF Founder) na tukawaomba wanaotuma waandike Nicks za kuweza kutanabaisha kuwa wao ndio walotuma.

=================================


Michango inaweza kutumwa kwa njia kuu nne:


1. Kwa walio nje wanaweza kutumia PayPal au Credit Cards au Debit Cards kwa kufuata link hii ( https://www.jamiiforums.com/payments.php) iliyo kwenye sahihi yangu (linapoonyesha dole gumba) na pindi mchangiaji anapoweka chochote tunakuwa notified nasi tunafanya kuwasiliana na mhusika ili aweze kupandishwa kwenda katika group la Premium Members.

Paypal users:

Details will follow

2. Njia ya pili ni kutumia Western Union au Money Gram na kutuma kwenda kwa Maxence Melo Mubyazi wa Dar es Salaam.

3. Njia ya tatu ni kutumia Bank accounts za Maxence kama ifuatavyo:

NBC:

Acc #: 033201064359
Jina: Maxence Melo Mubyazi

CRDB:

Account Name: Maxence Melo Mubyazi
Bank: CRDB Pugu Road Branch
Swift Code: CORUTZTZ
Acc No: 01J2092391800

4. Njia ya nne:

Unaweza kutuma recharge vouchers za tiGO, Zain, VodaCom au Zantel au ZAP (0784526444), M-PESA (0755642929), tiGO PESA, Z-PESA n.k kwenda kwa Maxence - 0713444649 naye atakufahamisha kuwa kazipokea. Namba za ZAP, M-PESA na Z-PESA anaweza kukupa ukiwasiliana naye.

=================================


Ikumbukwe, SI LAZIMA kuandika jina lako la kweli na SI LAZIMA kwenda mwenyewe bank kutuma pesa hizo (kwani unaweza kumpa unayemwamini na kumpa account details na jina lako ambalo ungependa aandike).

Tunaweza kuandika mengi lakini ukweli unabakia pale kuwa JF inahitaji michango yenu kwa sana tu.

Kwa wenye maswali zaidi wanaweza kuwasiliana na Maxence kupitia namba yake ya simu +255713444649.

Nasikitika kuwa yawezekana hata hivi natembeza bakuli
smile.png

 

Forum statistics

Threads 1,236,764
Members 475,220
Posts 29,267,958