Ushauri wa kisheria wa jinsi ya kumchukua mtoto baada ya kutokuwa na maelewano na mzazi mwenzangu

MEDICAL RECORDS

New Member
Apr 15, 2020
1
20
Habari za mchana wote!

Kuna kaka yangu mmoja tunaheshimiana sana naye , Ana mke wake sasa ndoa imemshinda anataka kumchukua mtoto kutokana na kwamba Hana mahusiano mazuri na huyu mke mke anaishi mwanza na yeye yupo Dodoma.

Lakini mtoto alimpata baada ya kuwa kwenye mahusiano na huyo dada akiwa tayari ana ujauzito huo walikubaliana na huyo dada mtoto akizaliwa awe wake na kweli alilea huo ujauzito na mpaka sasa mtoto ana miaka 4 ila alienda mwanza kuiona familia yake , siku moja akakutana na barua za mke za kuomba rikizo kwenye cheti cha mtoto jina limeandika jina X tofauti na la kwake ndipo ugomvi ulipoanzia, akaamua kuachana na huyo dada ila kuhusu mtoto dada akamwambia kwamba kumchukua mtoto mpaka awe mkubwa.

Je kisheria hiyo imekaaje wakuu?

Nawasilisha.
 

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,069
2,000
Kisheria hapo hana nguvu sana. "Best interest" za zinachukua nafasi. Je, kwa nini anadhani ni "best interest" za mtoto kukaa na yeye, badala ya mama yake?

HINT: Mimi siyo mwanasheria-msomi.
 

Doppelganger

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
1,764
2,000
1. Ndoa yake imemshinda.

2. Anataka kumchukua mtoto.

3. Cheti cha kuzaliwa hakina jina lake (baba).

4. Huwa anaruhusiwa kwenda kumuona mtoto.

Namshauri akapime DNA tu kwa sasa. Kwa sababu mama wa mtoto amemwambia atamchukua akiwa mkubwa, basi ajiridhishe kwanza kama kweli mtoto ni wa kwake. Mengine yafuate baadaye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Doppelganger

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
1,764
2,000
Jina la mtoto likiandikwa la mama. Je inakuwaje hapo Kama jina ndo linaamua Nani baba wa mtoto

Sent using Jamii Forums mobile app
Jina la mtoto haliamui kuwa mtoto ni wa nani.

Kama unadhani mtoto ni wa kwako, na mama wa mtoto hakupi nafasi kama baba, kuna hatua zimewekwa ambazo unaweza kuthibitisha kuwa mtoto ni wa kwako.

Wasiliana na mwanasheria aliye karibu nawe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom