Ushauri wa kisheria kuhusu notisi nyumba ya kupanga

Kayenga jr

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
443
348
Kama kichwa cha habari hapo kinavyosema naomba ushauri nimepanga chumba mwenye nyumba anaishi hapo hapo ila yeye ana nyumba yake tofauti na wapangaji na na anajitegemee luku yake na wapangaji wana luku yako lakini za hivi karibuni kama wapangaji tumekuwa na matumizi mkubwa ya umeme tukajaribu kufatilia tukagundua kuna waya umeingia ndani ya mwenye nyuma tulipo jaribu kuhoji mwenye nyumba akacharuka anasema kwa madai ya kumdhalilisha kwa madai yeye hawezi kutuibia umeme na akaandika notisi kwa wapangaji wote sie tuliokuwa vimbelembele kufatilia kwanini tutumie units 35 toka units 13 kwa 24 hours akatupa notisi kodi ikiisha tuhame kisheria imekaaje Hii.
 
mwenye nyumba anaitaka nyumba yake na amefata sheria pia.. ya kukupa notisi ya kuindoja pale kodi itakapoisha..
bas huna ujanja we muachie nyumba yake kodi yako itakapoisha..
 
Kama kichwa cha habari hapo kinavyosema naomba ushauri nimepanga chumba mwenye nyumba anaishi hapo hapo ila yeye ana nyumba yake tofauti na wapangaji na na anajitegemee luku yake na wapangaji wana luku yako lakini za hivi karibuni kama wapangaji tumekuwa na matumizi mkubwa ya umeme tukajaribu kufatilia tukagundua kuna waya umeingia ndani ya mwenye nyuma tulipo jaribu kuhoji mwenye nyumba akacharuka anasema kwa madai ya kumdhalilisha kwa madai yeye hawezi kutuibia umeme na akaandika notisi kwa wapangaji wote sie tuliokuwa vimbelembele kufatilia kwanini tutumie units 35 toka units 13 kwa 24 hours akatupa notisi kodi ikiisha tuhame kisheria imekaaje Hii.
Hahahaha hao jamaa hapo juu wamenichekesha usiogope kurogwa, ila ni hivi Ukishapewa notes na mwenye nyumba kama taarifa ya wewe kusepa kisheria inatikiwa iwe ni kabla ya miezi miwili,muda iliyotolewa ndo concern kubwa, kama amekupa notes kwa wakati ni heri uhame,
 
Dah Mkuu si Bora yenu hamshei Luku. Huku kwetu situesheni ni kama yenu ila Tunashea Luku. Sasa Luku Ikiisha hata kama tarehe 20 haongezi hadi mwisho wa mwezi. yaani ni Kero na Umeme tunalipia gali. 10 kwa Rumu aisee. Tumemchunguza baada ya yeye kutuhumu kuwa mingoni mwetu kuna wanaoovauz umeme tukagundua kuwa yeye huwa hanunui umeme kwa mujibu wa hela tuliyochanga bali hukata kidogo na hili suala hutokea kila inapohitajika ada ya wanae. Sasa la kufanya hatuna huyu mzee alikuwa Bodigadi wa Meya aliyepita na sasa kazi hiyo hana inabidi atafute mbadala. Ni mwanakaratee na anaweza hata kupiga mpangaji. kuna mmoja aliwahi vunjwa meno ya barazani.. Sema Mie nimepitia mambo ya Tae Kwon Do na anajua maana waliwahi kutembelea club yetu yeye na Meya basi ananiogopa lakini kwa suala la Umeme nimekwama. Hapa nishaanza kudunduliza kwa ajili ya Ujenzi nihamie kwangu. Na nyie Hameni ila "kila Mwenye nyumba ana udhaifu wake"
 
Ingekuwa vyema kutupatia makubaliano ya mkataba wa upangaji ulikuwa wamuda gani na notisi umepewa lini?
 
Back
Top Bottom