Ushauri wa Kipuuzi kwenu Wapinzani: Mpeni Kamba Magufuli ajinyonge mwenyewe

Kwa maelekezo wanayopewa wasimamizi wa uchaguzi sidhani hasa ikizngatiwa uchaguzi unasimamiwa na ma-DED 'wenye maelekezo' plus nec, usalama, mapolisi nk ni ngumu sana!
 
Kama kweli unaamini hivyo, uchaguzi ufanyike kwa haki mfano wasimamizi wawe kutoka nje na wala sio hawa makada wa CCM.
Hebu jaribuni wasimamizi wa Uchaguzi wa kumchagua mwenyekiti wenu atoke nje ya chadema tuone kama hamtakatana mapanga kati watu wa Kilimanjaro na mikoa mingine
 
GuDume, kwa hakika leo umetoa ushauri usiofaa.

Kususia na Kuzira haijawahi kuwa suluhisho la matatizo hata siku moja. Piga akili na utafute mfano popote walipofanikiwa kujikomboa kwa kumpa mkandamizaji nafasi ya kuzidi kukandamiza zaidi.

Ni swala la kukosa uongozi imara na wa kuaminiwa tu huko upinzani, waTanzania kwa umoja wao wapo tayari kabisa kujiondoa kwenye shida hii.

Chukulia mfano huu mmoja. Dr. Martin Luther King, Jr na wenzake wangekuwa na roho za kususa na kukata tamaa, hali ya weusi kule Marekani hadi sasa ingebaki kuwa watu wa daraja la pili.

Badala ya kususa, wapinzani sasa hivi walitakiwa wawe wanawaeleza wananchi umhimu wa kura zao na kuwahimiza wajitokeze kwa wingi kabisa kupiga kura; hata bila kujali watampigia mpinzani au mtu wa CCM. Huu ndio ujumbe mhimu ambao wapinzani wangeuwekea nguvu sana sasa hivi.

Na baada ya kupiga kura hizo, ni lazima pawepo njia ya kuhakikisha kura zinahesabiwa vizuri na matokeo kutangazwa bila hiana. Hapa ndipo panapohitajika kazi na mipango kuhakikisha hilo linatokea.

Na nadhani wakati huu hata hapa JF tungekuwa tunatafuta njia/mbinu za kuhakikisha kura za wananchi zichukuliwe kuwa ni 'takatifu' zisizoweza kuchezewa na mtu yeyote bila ya kupata matatizo binafsi kwa hao wanaopanga kuzichezea (Wasimamizi wa uchaguzi kila kituo na wenzao) wanachukuliwa kuwa 'liable' moja kwa moja kwa matendo yao hapo hapo kituoni.

Hata huko Marekani bunduki zilikuwepo, lakini watu walipoamua kubadili mwelekeo, hizo bunduki na mbwa hawakufua dafu.

Tatizo letu kubwa nadhani kwa sasa hivi ni kukosa viongozi tu wanaoweza kutuongoza tuyakatae yanayotokea sasa, tena bila ya kumwaga damu ya mTanzania yeyote.
Tupate kiongozi wa upinzani mwenye ushawishi na asiye muoga. Mizengwe ni mibgi sana
Kupokea tu form za upinzani imekuwa changamoto. Wahusika wanakimbia ofisi kuogopa kupokea form za wapinzani au kuwaapisha mawakala. Rejea kilichotokea kinondoni ,viongozi wote wana kesi hadi leo
 
Upinzani wa Nini ufe tu bhana tangu hii nchi imekuwepo wamefanya kutu gani Cha maana zaidi ya kupiga umbea tu ni Bora ufe tu ili tujue kabisa hatuna wapinzani Tanzania
 
Yaani kila nnapowawaza wapinzani na jinsi watakavyokuwa wanafanya kampeni kuomba ridhaa 2020 ni mpaka huruma, yaani wamepigika wamechoka wamechakaa, wako hoii, maskini
Zambotti huo ni uongo uliokithiri. Hakika mtu akipenda chongo huliita kengeza. Unaweza kusema wabunge wa CCM wana hali nzuri kuliko wapinzani? Huku ninakoishi mwaka 2010-2015 kulikuwa na Baraza la Madiwani lililo balance 21 wapinzani 20 wa CCM. Mambo yalikuwa mazuri na hasa kwenye maendeleo. Sasa Baraza la Madiwani lote ni CCM, hao biongozi wamebakia kama mbwa koko. Ni aibu ya hali ya juu....CCM ina wenyewe.
 
Kwanza niseme kabisa huu ushauri leo hii unaweza ukawa ni wa kipuuzi. Kwa sababu kuu kadhaa.

1. Mwaka 2020 utakuwa mwaka mbaya sana kwa wapinzani kweli kweli. Achana na wale vibaraka.

Asilimia kubwa hawatarudi hata list yao ipo na wengine kwa kugundua hili waliamua kuhamia CCM ili waweze pata riziki yao ya kila siku.

Tumeona maeneo ambayo Mh. Ametembelea pasipo unafiki akibagua walio chagua upinzani na waliochagua CCM.amesema kama una torch ukachanganya batteries na gunzi itawaka? Haiwaki.kaongea ukweli.

Kwa point hii tu wapinzani wanapitaje? Umeona maeneo ambayo amekuta wamechagua wapinzani alivyokuwa akiwajibu?lakini yeye si ndo analipa watendaji,wakurugenzi,anachagua wanahusika na uchaguzi?

WITO WANGU.
Mwaka 2020 mwachieni yeye agombee na wabunge wake. Kawaida dhambi ya Ubaguzi kama mtu anayo haitakosekana.atagundua wote ni CCM.na kuna maeneo mengi hatakuwa ametimiza ahadi.atatafuta namna ya kuwabagua.

Itafahamika kuna CCM Mag na CCM Asili. Hapo wapinzani kaeni pembeni muwe mnachochea tu moto.maana atakuja sema sehemu mmemchagua CCM mbunge lakini hafai.

Kawaida ya Ubaguzi upo kama pia. Yaani unaanzia juu kukubwa unashuka chini kudogo.level ya juu iliyopo sasa hivi ni CCM vs Upinzani. Ukiondoa Upinzani itakuwepo CCM yenyewe kwa yenyewe. Na hapo watu watakulana kwa misingi flani flani. So CCM yenyewe haitobaki salama.

Ushauri wangu wa kipuuzi kaeni chini mfikiri namna gani ya kujipanga kisayansi zaidi. Kuna kipindi semeni "sisi yetu macho tu"

"Siku watu wakigundua Adui yao Halisi ni nani Ukombozi utapatikana"

Yaani ni mara 100 kutawaliwa na CCM ya Magufuli kuliko upinzani wa kina Zitto, Mbowe, Lissu....hawafai, waachwe tu wabwabwaje.
 
Una ujasiri sana, unatoa ushauri wa kipuuzi na unapata muda wa kuandika. Sikubaliani na hili, mapinduzi hayalali. Hakuna siku oppressor atakupa uhuru kwa hiari.

Hili wazo ni potofu
 
Mnajidanganya watu watajitokeza sana kupiga kura..Meko hapati hata 50%
 
Hivi ninavyozungumza viongozi wa cdm wana kesi juu ya maandamano waliyofanya dhidi ya hujuma ya wasimamizi wao kutokuapishwa. Watu waliokamatwa baada ya maandamano yale wengi walipigwa sana na kufanyiwa ukatili mzito wakiwa kwenye vituo vya polisi, na vyombo vya habari vilibanwa visiripoti habari ile. Katika mazingira hayo unafanyiwa ukatili kisha unaambiwa uache kutumika na wanasiasa, kumbuka anayefanyiwa hayo ana familia yake anafanyiwa hivyo ili kutiwa uoga na pia hawezi kuendelea na shughuli zake kwani ataachwa na kilema. Kibaya zaidi sio ww wala wapinzani walioenda mahakamani hata kama haziaminiki kufungua mashitaka juu ya unyama na hujuma zile, bali wao sasa ndio wana kesi. Sasa jiulize, umedhulumiwa ww pamoja na wafuasi wako, na bado ww ndio una kesi ya kujibu.
Mwakijembe, haya yote unayoeleza hapa sio habari mpya au isiyojulikana. Ninakubaliana nawe kabisa kuwa hayo yametokea na dalili zipo kuwa yataendelea kutokea.
Ninachokataa na kutokubaliana nawe ni hata wewe kuzidi kuwaweka uoga hata hao wachache wanaokubali kufa wakiwa wamesismama. Unawafanyia kazi hao watesi kwa kuzidi kuwakatisha tamaa wazalendo hawa wanaokataa kuendelea kunyanyaswa.
Nikuhakikishie, wapo, ila wanakosa uongozi tu na mikakati ya kuyashinda hayo wanayofanyiwa. Na hapa, watu kama wewe ndio mnawakatisha tamaa kabisa kwa kuwapa mifano ya mateso yanayoweza kuwatokea.
 
Boss acha nadharia, unawaelimisha wananchi ukiwa wapi, kitendo tu cha kuwaambia wananchi hivyo kuhusu haki zao unakamatwa kwa uchochezi. Nakupa mfano mrahisi, juzi Mbowe kafanya kikao cha ndani, polisi walijazwa kwenye kikao kile, kwa kisingizio cha kulinda usalama wao na kujua ajenda ya kikao chake ni nini. Je mbele ya polisi unaweza vipi kuwaelimisha hao wananchi walinde kura zao au kuchukua hatua? Kumbuka wanaotumika kwenye hizo hujuma za uchaguzi nimeshakuambia ni vyombo vya dola hasa hasa polisi. Je watakuwa tayari uwajadili wao bila kukamatwa kwa uchochezi? Kumbuka polisi wanaweza kukufungulia kesi ya uchochezi kwa mlango wa jamuhuri, huku ww Muhanga ukiwekewa vikwazo vya kufungua hizo kesi na hata ukifungua kesi mahakama zinapangiwa hukumu iweje na hili unafahamu ndio lililopo. Kwa maneno maraisi huyu jamaa kaleta siasa chafu sana, ambazo kama atajiongezea muda wa kukaa madarakani naona kabisa nchi hii ikiingia kwenye machafuko iwapo wananchi wataamua kujitoa muhanga.
Nadhani inabidi nikuulize ni wapi (duniani) wenye kuhodhi madaraka waliporuhusu wapinzani wao wanaotaka kuwapora madaraka hayo wafanye hivyo kwa raha zao. Hata wakati wa kupigania uhuru, hakuna mkoloni aliyekuwa tayari kuondoka kwa furaha.

Tunachokosa sasa hivi ni watu waliojitoa maisha yao kukataa manyanyaso na wakawa na maono na mbinu za kuwaongoza wananchi.
Hivyo kwenda kushiriki hizo chaguzi kwa wapiga kura ni kutaka kuonyesha wapiga kura ni wengi na ccm inakubalika kwani watatangazwa washindi bila kujali lolote. Ni bora wananchi kutokwenda kupiga kura ili idadi iwe ndogo,
Wazo hili ndilo ninalolikataa kabisa kabisa.
Wananchi wenye kujua haki zao na umhimu wa kura zao nawasihi wajitokeze kwa wingi sana, wakapige kura kwa yeyote wanayetaka awe kiongozi wao. Ndio, kama wanaona CCM wanafanya kazi nzuri, wawachague tu kwa wingi. Kama wananchi hao wanaona CCM na viongozi wao wanawanyanyasa wananchi na hawawataki, wawanyime kura na kura zote wawape wapinzani.
Na kama unavyosema wewe, hizo kura walizopiga hazitahesabiwa, na kama wananchi hawana njia yoyote ya kuzidai zihesabike, ni bora iwe hivyo kuliko kususa kupiga kura. Kwani kususia kupiga kura kunaleta matokeo tofauti? Si hao hao CCM wataendelea kujitanua, tena kwa raha kabisa, hata roho zao hazitawasuta kujua kwamba walikataliwa kwenye kura!

Suluhisho ni kwa wapinzani kuwaelimisha wananchi juu ya haki zao na umhimu wa kura zao; na wawahimize hapo uchaguzi utakapokuja wajitokeze kwa wingi sana kupiga kura. Na kama hawa wananchi hawana uwezo wa kuhakikisha kwamba kura zao zilihesabiwa na kuheshimiwa (jambo ambalo nina hakika wananchi uwezo huo wanao), basi acha CCM wafanye dhuruma.

Samahani lakini, Mwakijembe na wengine wanaotaka wananchi wasipige kura wanawarahisishia kazi CCM.
 
Wananchi watakataa vipi wakati ni marufuku kulinda kura? Hujasikia kuwa ukishapiga kura ni marufuku kubaki vituoni kulinda kura? Kalamu 1 jitahidi kutoa mbinu zenye uhalisia sio hizo za enzi za JK aliyekuwa na soni kwa mbali ya demokrasia. Huyu wa sasa hivi anafanya lolote na umma uko kimya kabisa na mifano ya wazi na dhahiri ipo. Kushiriki kupiga kura ni kuonyesha kuwa una uwezo mdogo wa kuelewa hali halisi iliyopo.
Kwa dhati kabisa, ninakuomba tushiriki pamoja kuzitafuta hizo mbinu badala ya kuwatisha na kuwatia woga wananchi kwa faida ya wanaotaka kuendelea kutukandamiza. Inawezekana kabisa kuukataa huu ukandamizaji
 
Extremely clever thinking
Kwanza niseme kabisa huu ushauri leo hii unaweza ukawa ni wa kipuuzi. Kwa sababu kuu kadhaa.

1. Mwaka 2020 utakuwa mwaka mbaya sana kwa wapinzani kweli kweli. Achana na wale vibaraka.

Asilimia kubwa hawatarudi hata list yao ipo na wengine kwa kugundua hili waliamua kuhamia CCM ili waweze pata riziki yao ya kila siku.

Tumeona maeneo ambayo Mh. Ametembelea pasipo unafiki akibagua walio chagua upinzani na waliochagua CCM.amesema kama una torch ukachanganya batteries na gunzi itawaka? Haiwaki.kaongea ukweli.

Kwa point hii tu wapinzani wanapitaje? Umeona maeneo ambayo amekuta wamechagua wapinzani alivyokuwa akiwajibu?lakini yeye si ndo analipa watendaji,wakurugenzi,anachagua wanahusika na uchaguzi?

WITO WANGU.
Mwaka 2020 mwachieni yeye agombee na wabunge wake. Kawaida dhambi ya Ubaguzi kama mtu anayo haitakosekana.atagundua wote ni CCM.na kuna maeneo mengi hatakuwa ametimiza ahadi.atatafuta namna ya kuwabagua.

Itafahamika kuna CCM Mag na CCM Asili. Hapo wapinzani kaeni pembeni muwe mnachochea tu moto.maana atakuja sema sehemu mmemchagua CCM mbunge lakini hafai.

Kawaida ya Ubaguzi upo kama pia. Yaani unaanzia juu kukubwa unashuka chini kudogo.level ya juu iliyopo sasa hivi ni CCM vs Upinzani. Ukiondoa Upinzani itakuwepo CCM yenyewe kwa yenyewe. Na hapo watu watakulana kwa misingi flani flani. So CCM yenyewe haitobaki salama.

Ushauri wangu wa kipuuzi kaeni chini mfikiri namna gani ya kujipanga kisayansi zaidi. Kuna kipindi semeni "sisi yetu macho tu"

"Siku watu wakigundua Adui yao Halisi ni nani Ukombozi utapatikana"
 
Tupate kiongozi wa upinzani mwenye ushawishi na asiye muoga. Mizengwe ni mibgi sana
Kupokea tu form za upinzani imekuwa changamoto. Wahusika wanakimbia ofisi kuogopa kupokea form za wapinzani au kuwaapisha mawakala. Rejea kilichotokea kinondoni ,viongozi wote wana kesi hadi leo
Inasikitisha sana kwamba tumefika hapa bila ya kujitambua!
 
Mwakijembe, haya yote unayoeleza hapa sio habari mpya au isiyojulikana. Ninakubaliana nawe kabisa kuwa hayo yametokea na dalili zipo kuwa yataendelea kutokea.
Ninachokataa na kutokubaliana nawe ni hata wewe kuzidi kuwaweka uoga hata hao wachache wanaokubali kufa wakiwa wamesismama. Unawafanyia kazi hao watesi kwa kuzidi kuwakatisha tamaa wazalendo hawa wanaokataa kuendelea kunyanyaswa.
Nikuhakikishie, wapo, ila wanakosa uongozi tu na mikakati ya kuyashinda hayo wanayofanyiwa. Na hapa, watu kama wewe ndio mnawakatisha tamaa kabisa kwa kuwapa mifano ya mateso yanayoweza kuwatokea.

Mkuu nitajie kundi utakaloliongoza nije nijiunge na ww. Ukiweza niPM siku ya uchaguzi nije nikae na ww tuwe tunalinda kura.
 
Mkuu nitajie kundi utakaloliongoza nije nijiunge na ww. Ukiweza niPM siku ya uchaguzi nije nikae na ww tuwe tunalinda kura.
Hapana, mtu kama wewe huwez kuwa kundi nitakalokuwemo mimi kwa sababu ambazo nimekwisha zitaja. Wewe ni adui wa haki za waTanzania. Unaunga mkono watanzania kunyanyaswa.
 
Back
Top Bottom