hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,539
Mkuu, hilo nalitambua binafsi niko katika mpango wa kufanikisha jhilo hapo juu, lakini turudi katika hoja ya msingi(Usitake kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu)
Hospitali si Jengo,, unapoongelea Hospitali tunaongelea huduma stahiki inayopaswa kutolewa! Jambo tunalo lisema hapa ni la Mkuu wa Nchi kupata matibabu nje kwa jambo linalowezekana hapa nchi(na usije na majibu rahisi eti anaweza kuchagua daktari yeyote) hilo tunatambua, lakini kama Taasisi(ana washauri, ana daktari wake n.k) walioweza kumuongoza katika hilo! Pili tunaongelea Raisi kama Public figure and not a mere person!
Sasa, tuje kwenye masuala ya msingi; Mwaka juzi madaktari walipogoma kudai baadhi ya madai, walionekana ni watu wenye 'uchu/tamaa ya fedha'! Leo hii Hospitalini ni hali mbaya kuliko ilivyokuwa hapo miaka miwili iliyopita., Na kwa kusema Hospitaki nina maanisha Hospitali ya Taifa(MNH), Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili(MOI), Taasisi ya Saratani Ocean Road(ORCI), Hospitali ya Rufaa Bugando(BMC), Hospitali ya Rufaa Mbeya(Mbeya Referral) na kitu ni hicho hicho huko Tanga, Tabora, Kigoma n.k
Hakuna madawa, hakuna vifaa vya vitendea kazi, hakuna kinga dhidi ya magonjwa(vitu ambavyo ni vile vile madaktari walivitaka).
Tunaweza kufika mbali kwa hospitali hizi hizi tulizonazo iwapo tutajizatiti kufanya yanayopaswa kufanyika! "Si kila shati likiwa na doa linatupwa mkuu". Gharama za maisha ndiyo hizo zinazoongezeka kila leo, Na bado hospitali zinajengwa pale pale zilipo(badala ya kuboresha hosoitali zilizopo na ku_recruit watoa huduma za afya katika maeneo husika), So kwa hili hebu weka u_chama pembeni tuongee facts mkuu.