Ushauri wa Kikwete kupima saratani, mzuri lakini una mashaka

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,823
2,000
Jana Jumamosi ya tarehe 29 Nov. 2014, Rais wa JMT Mh JK, alisikika akiwashauri Watanzania kuwa na desturi ya kupima afya zao Mara kwa Mara.

Ushauri huu ni mzuri ila unatia SHAKA kwenye namna alivyoufikisha. Huku akitolea mfano wa saratani ya tezi dume alisema kwamba vipimo vya kugundua kama una saratani hata Muhimbili vipo.

Sasa je, kama vipimo hivyo vipo Muhimbili, yeye alikwenda kufanya nini USA?

Au kwanini hakuanzia Muhimbili? Je haiamini Hospitali ya Nchi yake?

Naombeni mnisaidie kupaelewa hapa!
 

matasha

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
378
0
Pia aliitaja maabara ya lancet ipo pale moroko ni ya watu wa south afrika ina vipimo vya hali ya juu sana
 

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,111
2,000
Bila kwenda nje ya nchi utakufa siku si zako,hawa jamaa wameharibu mfumo wa afya nchini vibaya sana.

Mi siku hizi hata nikiugua mafua,nafunga na kukesha nikiomba Mungu.
 

BAOBAO

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
1,874
1,250
Wakuu ! Mpaka sasa sijaelewa rais Kikwete ana kansa kwenye uume (mshipa) au kokwa(korodani) ?
JK NYAMA IPI AMEONDOLEWA ?
 

BAOBAO

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
1,874
1,250
Si busara kama baba uwaruhusu watoto au raia wako kutazama lo lote kwenye sehemu za siri mzazi ! Hekima ni nje ya nchi
 

MSHERWAMPAMBA

JF-Expert Member
May 22, 2014
342
0
Sikieni hiyo kitu hivi hivi kijuu juu tu sio kitu ya kufanya nayo mchezo inahitaji technology ya hali ya juu sana pia na daktari aliyebobea ktk hiyo shughuli na kama ikiwa imeenea sana hata kokwa ndani ya korodani hutolewa hata kuzalisha tena mtu hutoweza hata wakifanya utaalam wa aina gani haitowezekana kukurudisha ktk hali yako ya kawaida.Wanaume nakuombeni mjipime huo ugonjwa wanasema the earlier the better ukijijua ka unao ni rahisi sana kuwa reversed na kuondolewa msisubiri sana mpaka kitu kijiibue chenyewe hapo ngoma inakuwaga ngumu sana ka iliyomtokea kiongozi wetu JK yeye alisubiria sana,msijidanganye sijui kwenda India or China western countries ni wao wenye utaalam bora wa kupambana na hiyo cancer.
Sasa swali ni je watu wakisha pima na kugundulika wanao wataweza pelekwa nchi zilizoendelea wakafanyiwe hiyo operation yenyewe kwa fedha za serikali?au ndio itakuwa rukhsa ya watanzania kutegemea nguvu za giza kama vile kupiga manyanga na kumtegemea sengoma peke yake.Kwa wahindi msitegemee huko sio kuzuri mtarudi hata hizo korodani zenyewe zimeng'olewa hakuna kitu mtabakia na mkwaju peke yake ukiwa peku peku tuu.Tumuombeni mwenyezi mungu atuepushe na hilo gonjwa baya.M/Mpamba.
 

babuwaloliondo

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
378
195
Yaani nimeshangaa sana, amerudi anasifia matabibu wa nje kuwa wanashona kwa kutumia chuma na unapona. Hivi kwanini anashindwa kuwawezesha hawa wakwetu. Unawezaje kusifia kwa watu unaacha familia yako inaangamia?.
Hii ni busara ya wapi, hakua madawa, hakuna vifaa ila anaongea kirahisi kama vile ni rahisi kwa babu yangu aliyeko kisarawe kwenda kupimwa.
 

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,823
2,000
Yaani nimeshangaa sana, amerudi anasifia matabibu wa nje kuwa wanashona kwa kutumia chuma na unapona. Hivi kwanini anashindwa kuwawezesha hawa wakwetu. Unawezaje kusifia kwa watu unaacha familia yako inaangamia?.
Hii ni busara ya wapi, hakua madawa, hakuna vifaa ila anaongea kirahisi kama vile ni rahisi kwa babu yangu aliyeko kisarawe kwenda kupimwa.
Tunahitaji committed President atakayekuwa na Ujasiri uliotukuka katika kuleta Teknolojia ya kielimu, hasa Afya (Health) na Engineering ( Electrical, biological, Mechanical, Petroleum & Gas Minerals,) ili kila kitu kiwezekane hapa hapa Tanzania. Tupunguze Majanga ya magonjwa hatari kama Saratani na Gharama kubwa za kupeleka viongozi nje ya nchi, Gharama kubwa na Ufisadi wa Makampuni ya kigeni kwenye Umeme na madini mfano scandal ya Escrow, watanzania wawekeza wenyewe kwenye Gas, mafuta na madini na kilimo cha kisasa (Mashine za maana za kulima, kuvuna, kusindika na kuzalisha) ili kukuza kipato cha mtanzania pia uchumi wa nchi.
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Jana Jumamosi ya tarehe 29 Nov. 2014, Rais wa JMT Mh JK, alisikika akiwashauri Watanzania kuwa na desturi ya kupima afya zao Mara kwa Mara. Ushauri huu ni mzuri ila unatia SHAKA kwenye namna alivyoufikisha. Huku akitolea mfano wa saratani ya tezi dume alisema kwamba vipimo vya kugundua kama una saratani hata Muhimbili vipo, sasa je kama vipimo hivyo vipo Muhimbili, yeye alikwenda kufanya nini USA? Au kwa nini hakuanzia Muhimbili? Je haiamini Hospitali ya Nchi yake?
Naombeni mnisaidie kupaelewa hapa!
Kupima na kutibu ni vitu tofauti.
 

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,823
2,000
Kupima na kutibu ni vitu tofauti.
Sawa, lakini Je, hata hatua na vipimo vya awali ilishindikanaje kuanzia Muhimbili na pale Lancet mtaa wa Moroko Dsm ambayo alidai ina wataalamu waliobobea kutoka South Afrika??? au hata kupima tu lazima uende Marekani??
Kwa maana hiyo Hospitali zetu zote mpaka za rufaa ni maabara tu kwa ajili ya kupima na hazina uwezo wa kutibu???
Tuzunguke tuwezavyo JK kaondoa Imani ya Hospitali zetu kwa wananchi!
 

hippocratessocrates

JF-Expert Member
Jul 1, 2012
3,600
1,225
Kupima na kutibu ni vitu tofauti.
Nakubaliana na wewe, kuwa 'kupima na kutibu' ni vitu viwili tofauti, lakini unajua wether ni Ukuaji wa tezi dume(usio saratani) na ule wa saratani unaweza kufanyika hapa nchini katika hospitali za hapa hapa(chache sana).

Pili, hata kama kutibu ni tofauti, na ndiyo maana yeye JK alikwenda nje, anategemea hospitali za hapa nchini nani wa kuziboresha? Tafsiri/taswira ni ipi huko nje ya nchi? Yaani 'baba mwenye nyumba kutokuwa na choo nyumbani kwake na anafurahia kuiacha familia kujisaidia pooote huku yeye akienda choo cha jirani' napo unaona hiyo ni sawa kwako!

Then you must be more idiot that you were,mkuu!
 

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,823
2,000
Mengine ni heri zaid ukayaacha yakapita!!!
Washauri na waandishi wanamuingiza Rais katika mitafaruku bila sababu sababu ya mambo kama haya!!
Bora zaidi angeshuka Airport na kwenda zake Nyumbani/Ikulu kupumzika. Unplanned speech ni hatari sana kwa Kiongozi wa Nchi
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Nakubaliana na wewe, kuwa 'kupima na kutibu' ni vitu viwili tofauti, lakini unajua wether ni Ukuaji wa tezi dume(usio saratani) na ule wa saratani unaweza kufanyika hapa nchini katika hospitali za hapa hapa(chache sana).

Pili, hata kama kutibu ni tofauti, na ndiyo maana yeye JK alikwenda nje, anategemea hospitali za hapa nchini nani wa kuziboresha? Tafsiri/taswira ni ipi huko nje ya nchi? Yaani 'baba mwenye nyumba kutokuwa na choo nyumbani kwake na anafurahia kuiacha familia kujisaidia pooote huku yeye akienda choo cha jirani' napo unaona hiyo ni sawa kwako!

Then you must be more idiot that you were,mkuu!
Jee, hili hujaliona:Hujaona maboresho pale Muhimbili awamu ya Kikwete? Kikwete hilo la "kuziboresha" hospitali za hapa nchini, hakuna aliyefanya zaidi ya Kikwete toka tupate Uhuru. Kumbuka hilo.
 

Dibwela

Senior Member
Jun 29, 2013
106
195
Dah! Kula ni tabu kwa wa tz.je atawalipia gharama za uchunguzi wa afya?au alikuwa anawaambia wenzie?yeye ameenda usa.sisi tuende muhimbili.pimeni kauli yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom