Ushauri wa kielimu kuhusu vijana wa Sekondari

Wildlifer

JF-Expert Member
May 12, 2021
1,882
5,186
Salaam wanaJF.

Kutokana na uzoefu wangu binafsi wa maisha hadi sasa na uelekeo wa dunia unavyokwemda, nina washauri vijana waliopo Sekondari, wazazi au walezi tunaowafanyia maamuzi, au mtu yeyote uliye kwenye nafasi ya kushawishi maamuzi, ni vyema kijana atakapomaliza kidato cha Sita, ajiunge na chuo cha ufundi wowote mfano Magari, Useremala, Umeme [ na yanayofanana na hayo], kisha ndio aendelee na elimu ya Chuo kikuu kwa masuala ayatakayo kama Udaktari, Sheria, Ualimu n.k.

Hii faida zake ni mbili,

Moja unapokuwa Chuo unaweza kuwa unafanya vijikazi viwili vitatu [vinakupa hela ya kujikimu na pili inakuongezea ujuzi].

Pili; Utakapomaliza Chuo ukiwa mtaani walau unakuwa na ujuzi wa kuingizia pesa kabla hujapata ajira ya ndoto yako. Lakini pia hata ukiwa na ajira ya ndoto zako, haiharibu kitu unapokuwa daktari huku una kampuni yako ya ufundi seremala.

Inawezekana ikiwa tu utaweka aibu za kijinga pembeni na ukaamua kusimamia kile kinachokufaa.
 
Mkuu unamaanisha kijana aliyemaliza kidato cha sita asitishe kwenda chuo kikuu[Degree] aende diploma. Huoni kama atakua amerudi nyuma?
 
Hapo ni kumrudisha nyuma umri unazidi kusogea
Yes, ndio maana watoto leo hii wanaanza shule wana miaka mitano. Umri bila Maendeleo ya kimaisha una maana gani? Pia what is miaka miwili kwenye kutengeneza maisha?
 
Back
Top Bottom