Ushauri wa kibiashara kwa Lulu michael. Nifikishieni

Mangi flani hivi

JF-Expert Member
Jan 2, 2016
2,026
3,100
Kwanza pole sana Lulu kwa matatizo,

Ila ili upate uhuru wa moyo na nafsi nitakuomba utulize akili umalize time yako urudi nyumbani ili watesi wako wasipate sababu ya kukunanga tena.

Ila sasa Wakati ukiwa huko gerezani, fanya hili:

Wewe ni mtu maarufu na una jina kubwa katika sector ya Sanaa na ulimbwende. Fanya mawasiliano na watu wa hapo gerezani wanaozalisha vifaa mbalimbali na kuviuza huku nje.... Mf: wanatengeneza viatu, mabegi, kofia, makapeti nk.

Tafuta Meneja masoko wako wa huku nje, apeleke brand Huko gerezan na uchague moja ya bidhaa unayotaka kuibrand kwa jina lako, then zalisha na utuletee huku nje..... (Ushauri huu unategemea na namna magereza ya TZ yanavyofanya kazi) but najua hutokosa la Kufanya ukiwa Huko ndani.

Nimeshauri nikirejea namna ambavyo wasanii wa nchi nyingine wanavyotumia time zao za jela Kuandaa project na wakitoka ni mwendo wa kupiga hela tu.....

Rejea: lil wyne, Chris brown, na wengine wengi.....


NB: ushauri huu una hati miliki.
 
Hivi jela unapajua or unapasikia mkuu? Yani utumie muda wa serikali (kifungo) kufanya biashara zako binafsi tena kwenye facility ya serikali (gereza)? Acha utani KABISA.

NB: Joseverest don't take it personal bro.
 
Hivi jela unapajua or unapasikia mkuu? Yani utumie muda wa serikali (kifungo) kufanya biashara zako binafsi tena kwenye facility ya serikali (gereza)? Acha utani KABISA.

NB: Joseverest don't take it personal bro.
Naamini umesoma yote niliyoandika..... Kwanza sijasema afanye yeye na pili nimetoa room kwa wanaohusika na magereza Kufanya kwa mujibu wa kanuni zao.
 
Mkuu kwanza kuna kupambana na hali yake.kwa jinsi hali halisi ilivyo hii kitu ni ngumu kutekelezeka. Watanzania tuna wivu sana wasije muua binti wa watu huko gerezani kwa hizo project.

Uraian tu kajizolea maadui tele kisa alikua anavaa nguo nzuri,simu bei mbaya picha matata anapiga
 
Watanzania ni wanafki nakumbuka Kwenye msiba wa Kanumba watu wengi lawama zote kwa Lulu Leo mtoto kawekwa ndani wanamuhurumia .Muacheni mtoto wa watu Kah Wasije wakamzulia lingine picha za kuedit tu zilikuwa zinawatoa povu sembuse hilo ni ngumu.
Mkuu umecomment kwa hisia kali sana...... Anyway, ninachojua ni kwamba hata awe na maadui vipi ni lazima afanye kitu maisha yaende. Ni ushauri tu.
 
Ushauri wangu huu umepokelewa vizuri na nimeambiwa tayari kuna watu wanaufanyia kazi. Ni vyema.
 
Ushauri wangu huu umepokelewa vizuri na nimeambiwa tayari kuna watu wanaufanyia kazi. Ni vyema.
Safiiiii, nilichelewa kuiona hii post.... good idea bro na hongera kwa Lulu na watu kwa kukubali maana ni bonge la idea umewapa.... good luck guys.
 
Aendelee kusoma online kama magereza zetu zinaruhusu maskini lulu ipo siku utakua huru
 
Duh! Yaani watu kwa sifa, kwanini usimfate huko gerezani ukamshauri? Kule hana smartphone mkuu
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom