Ushauri wa kiafya jinsi ya kuishi na mpenzi mwenye UKIMWI na kuanzisha familia

mputura

Member
May 20, 2013
7
45
Habari wadau,

Nahitaji nipate ushauri wa mawazo na wakitaalam pia juu ya hili jambo ambalo linaniumiza kichwa.

Nipo katika mahusiano na msichana takriban miezi 3 sasa gheto anakuja vzr ila kila nikimuomba mchezo anakataa huku akinipa visingizio kibao mpaka nikawa nakasirika na nikafikiria hata niachane nae ila nikawa namvumilia anakuja geto tunaishia kupiga story tu na ananiruhusu nimshike popote ila sio sex.

Sasa nilipojaribu kumuhoji zaidi akanambia "mimi nahitaji tujuane zaidi pia nikwambie historia kidogo ya maisha yangu" hivi juzi ndo akaniambia ukweli sasa kwamba yeye amezaliwa na virusi vya ukimwi na wazazi wake wote walikufa na ukimwi hivyo akutaka mimi aniue akaamua aniambie ukweli sababu ananipenda na kiukweli hata mimi nampenda huyu binti hakika ila kwa jambo hili limenistua sana.

Msaada wangu kwenu niweze kupata ushauri je nawezaje kuishi na mwanamke kama mpenzi wangu na nikaenjoy sex na tukaweza kupata watoto wakati yeye ni positive, na siko tayari kumuacha sababu nampenda na anajisikia furaha sana kuwa na mimi sasa labda nikisema nimuache si ataona kama nimemnyanyapaa baada ya kuniambia ukwel juu ya hali yake ya kiafya.

Naombeni msaada wa mawazo juu ya jambo hili nimekuwa na mawazo sana sijui nifanyaje
 

Dreadnought

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
1,774
2,000
Kama huyo mpenzi wako ameshatumia ARV kwa miaka kadhaa na kwa ufasaha basi hawezi kuambuzika, virus vimeshakuwa "hybernated" dawa za siku hizi ni more advanced.

Kama unampenda waweza endelea naye. Yataka moyo lakini.
 

Ndaghine

Senior Member
Mar 12, 2018
158
250
Wajuvi wa mambo waje, hili swala nahic ni kupata ushaur zaidi kwa madokta, naamin pia wapo wengi wakusaidie kwa mim ambaye can taaluma ya udokta naezq kwambia uoe, wapo wengi ambao tunatoka nao lakn hawajatuambukiza mungu ametuepusha, Zaid yataka moyo, nawasilisha!
 

mputura

Member
May 20, 2013
7
45
Kama huyo mpenzi wako ameshatumia ARV kwa miaka kadhaa na kwa ufasaha basi hawezi kuambuzika, virus vimeshakuwa "hybernated" dawa za siku hizi ni more advanced.

Kama unampenda waweza endelea naye. Yataka moyo lakini.

Asante mkuu unanipa matumain sasa kuhusu kipata watoto inakuwaje hapo???
 

lamaa

JF-Expert Member
Nov 2, 2018
652
1,000
Mtoa Mada Umekwisha waka!!! Sema tu!!

Unatafuta namna ya kujipoza Any way///// ngoja wataalam waje!!!
 

mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
11,547
2,000
Habari wadau,

Nahitaji nipate ushauri wa mawazo na wakitaalam pia juu ya hili jambo ambalo linaniumiza kichwa...
Dah...katika watu wenye bahati duniani wee mmoja wapo. Demu kakwambia ukweli kuwa ana ngoma. Huyu braza bila kuuliza mumowe fasta
 

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
6,609
2,000
Kwanza tafakari kwa uzito upime je upendo wako kwake ni kwasababu ya urembo wake? Vipi hali ya urembo ukibadilika bado utaendelea kumpenda?

Jipime upendo wako kwakwe unaongozwa na hisia za kimapenzi au hali halisi?

Kuna mahali umenitatiza kidogo umetupiga mkwara tusikwambia habari ya kumuacha maana yake mapenzi yako yanaongozwa na hisia za kimahaba zaidi ya uhalisia.
 

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Jan 12, 2018
15,138
2,000
Mkuu unaanza mahusiano mapya bila kujuana hata afya unaanza kuomba papuchi? Daaah aisee, inawezekana mkapata mtoto mzima kabisa ila kuna mambo mengi ya msingi inatakiwa myafuate,nenda kwenye kituo cha ushauri Mtapata mwongozo.
 

mputura

Member
May 20, 2013
7
45
Kwanza tafakari kwa uzito upime je upendo wako kwake ni kwasababu ya urembo wake? Vipi hali ya urembo ukibadilika bado utaendelea kumpenda?..
Asante kwa ushauri mkuu,ushauri wowote napokea mkuu utanisaidia hata kama utakuwa unapingana na mawazo yangu
 

renamaizo

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
1,527
2,000
Nakuonea huruna sn na hata ukienda kwa washaur nasaha km mm ndie doctor ningeishia tu kukuzaba makofi yaan vitu vengine unaomba ushaur unataka tukishaur ujinga ili uje useme sisi ndio tumekupoteza jipoteze.

Ushaur wangu ni huu uyo dada abaki kuwa rafik ukijitia mtoto wa mjin kumfanya moenz ucrud na thtead apa kumtus tutakutukana ww watu wanavunja mpaka ndoa zao kisa ayo mambo ww unayakimbilia utu wa mtu una dhaman kubwa MONEY cant buy life.
 

X-12

JF-Expert Member
Sep 23, 2020
433
1,000
Tumia akili bro move-forward acha na mambo ya hisia utapotea ukiwa kijana mdogo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom